Rais wa DRC, Felix Tshisekedi awasamehe waliofungwa kwa kupanga njama za kumuua Laurent Kabila

Aliyemuua Kabila aliuawa siku ile ile!

Shekedi anajiandalia ulinzi, hawa watakuwa walinzi wa Shekedi na Kabila itampasa alale jicho 1 wazi.

Everyday is Saturday............................... :cool:
wataanza kuchinjana very soon.
 
wengi walionewa, Kabila alipokufa watu walikamatwa hovyo sana, Tshisekedi hajakurupuka lazima ana sababu zake
hata hivyo inaaminika sababu za Kabila kuuwawa ni kitendo chake cha kumuua mmoja wa watu wake wa karibu ambaye ndiye aliwa train hao kina “kadogos” ambao walikuwa ndio walinzi wa Rais (jina la huyo jamaa nimelisahau)
Ndigana Masasu
 
Tshekedi mwenyewe anaongoza hilo taifa kwa kufuata utawala uliopita..maana Bunge la nchi hiyo lina wabunge wengi kutoka chama cha Kabila..kuliko chama chake kinachodaiwa kuongoza dola lakini ukweli ni kwamba kabila anaongoza nchi kupitia bunge.
Na ndio maana ameamua kujitoa kwenye utumwa huo!!wa congo man wengi wanamuona kama ndio mkombozi wao, na kabila anachukiwa sana na wa congo, ila ni kikundi tu kidogo ndicho kiko naye nacho ni kutokana na maslahi yao tu!!ila kwa kinachoendelea congo, ufalme wa kabila unakwenda dondoka, na ndio mengi yatamfuata!!hiki kiunzi kama tshekedi atakivuka basi, ataweza kutawala vizuri.
 
Afisi ya rais nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imesema Rais Felix Tshisekedi amewapa msahama wa rais watu ishirini na sita waliokuwa wamefungwa jela kwa njama ya kumuua rais wa zamani wa nchi hiyo Laurent Kabila.

Watu hao walihukumiwa kifo na maafisa wanasema baadhi wamefariki wakiwa gerezani ila hakuna hata mmoja ambaye amenyongwa. Laurent Kabila aliuwawa kwa kupigwa risasi na mlinzi wake katika kasri lake mwezi Januari mwaka 2001.

Mara tu baada ya kumuua, mlinzi huyo naye aliuawa kwa kupigwa risasi. Mtoto wa Laurent, Joseph Kabila mara kadhaa alikataa wito wa kuwasamehe watu hao waliofungwa kwa kumuua baba yake.
Imeisha hiyo.
 
wengi walionewa, Kabila alipokufa watu walikamatwa hovyo sana, Tshisekedi hajakurupuka lazima ana sababu zake
hata hivyo inaaminika sababu za Kabila kuuwawa ni kitendo chake cha kumuua mmoja wa watu wake wa karibu ambaye ndiye aliwa train hao kina “kadogos” ambao walikuwa ndio walinzi wa Rais (jina la huyo jamaa nimelisahau)
Anaitwa kamanda masasu ndanga
 
DRC migogoro itakwisha akipatikana Dictator tena, wakati Mobutu anachukua madaraka nchi ilitaka kugawanyika jimbo la shaba liwe nchi yani kuwe na nchi mbili humo ila Mobutu alipeleka jeshi na waliuwawa wanamgambo wote
wakati wake watu waliopanga kupindua nchi au kumuua aliagiza wauwawe nchi ikawa na amani kwa miaka kama 25
Mobutu alishachemsha kwa waasi wa Katanga hadi akaomba msaada kwa Marekani na Ufaransa ndio wakamuokoa jimbo tajiri la Katanga chini ya aliyekuwa Gavana wakati huo Moise Tshombe lisiende.
 
Mobutu alishachemsha kwa waasi wa Katanga hadi akaomba msaada kwa Marekani na Ufaransa ndio wakamuokoa jimbo tajiri la Katanga chini ya aliyekuwa Gavana wakati huo Moise Tshombe lisiende.

ni kweli mkuu, wakati ule jeshi lilikua disorganized ilibidi afanye vile pia wale waasi walisaidiwa na urusi hivo ilikuwa lazima wapate msaada na wao
 
Ukifuatilia hii sakata utagundua col.eddy kapend ndio kiunganishi cha kuuawa kabila lola
hapana mkuu kilichomgalimu ni harakati zake za kulinusuru taifa manake wanasema ma general walikua wanamsikiliza sana cornel edy kapendi kwa sababu ya ukalibu wake na rais kabila na ndie aliye muua yule kijana aliyemuua rais sema walimuhoji kwanini uliharakia kumuua badala ya tumuhoji hapo akatepeta ila alikua hajui mission yoyote alafu ile kwenda kuongea kwenye TV ilimgalimu zaidi manake yeye hakuwa msemaji wa serikali ila alifanya kwa mapenzi mema ya nchi
 
wengi walionewa, Kabila alipokufa watu walikamatwa hovyo sana, Tshisekedi hajakurupuka lazima ana sababu zake
hata hivyo inaaminika sababu za Kabila kuuwawa ni kitendo chake cha kumuua mmoja wa watu wake wa karibu ambaye ndiye aliwa train hao kina “kadogos” ambao walikuwa ndio walinzi wa Rais (jina la huyo jamaa nimelisahau)
Anselme Masasu
 
Back
Top Bottom