Rais wa DRC, Felix Tshisekedi awasamehe waliofungwa kwa kupanga njama za kumuua Laurent Kabila

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Afisi ya rais nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imesema Rais Felix Tshisekedi amewapa msahama wa rais watu ishirini na sita waliokuwa wamefungwa jela kwa njama ya kumuua rais wa zamani wa nchi hiyo Laurent Kabila.

Watu hao walihukumiwa kifo na maafisa wanasema baadhi wamefariki wakiwa gerezani ila hakuna hata mmoja ambaye amenyongwa. Laurent Kabila aliuwawa kwa kupigwa risasi na mlinzi wake katika kasri lake mwezi Januari mwaka 2001.

Mara tu baada ya kumuua, mlinzi huyo naye aliuawa kwa kupigwa risasi. Mtoto wa Laurent, Joseph Kabila mara kadhaa alikataa wito wa kuwasamehe watu hao waliofungwa kwa kumuua baba yake.
 
Yani ni sawa na kuwapongeza kwa kitendo walichokifanya.
Nae Tshisekedi dingi yake alivyofariki Kabila Jr akiwa ni rais aligoma asije kuzikiwa Congo,mwili ukabaki Belgium kwa miaka 2 mpk Tshisekedi alivyokua rais ndipo ukaja kuzikwa hapo Congo.

Sasa labda ndio anamlipizia kisasi kwa style hio hio.
Yani ni sawa na kuwapongeza kwa kitendo walichokifanya.
 
Tshekedi mwenyewe anaongoza hilo taifa kwa kufuata utawala uliopita..maana Bunge la nchi hiyo lina wabunge wengi kutoka chama cha Kabila kuliko chama chake kinachodaiwa kuongoza dola lakini ukweli ni kwamba kabila anaongoza nchi kupitia bunge.
 

Georges Mirindi aandika kitabu :

TRES URGENT À SUIVRE LA SUITE DE GEORGES MIRINDI LA MORT DE LD KABILA, NE NIE PAS C'ÉTAIT BIEN TO


 
Yani ni sawa na kuwapongeza kwa kitendo walichokifanya.
Wengi walionewa, Kabila alipokufa watu walikamatwa hovyo sana, Tshisekedi hajakurupuka lazima ana sababu zake.

Hata hivyo inaaminika sababu za Kabila kuuwawa ni kitendo chake cha kumuua mmoja wa watu wake wa karibu ambaye ndiye aliwa train hao kina “kadogos” ambao walikuwa ndio walinzi wa Rais (jina la huyo jamaa nimelisahau)
 
Kuongoza nchi yenye migogoro isiyokwisha kama DRC kazi kweli kweli.
DRC migogoro itakwisha akipatikana Dictator tena, wakati Mobutu anachukua madaraka nchi ilitaka kugawanyika jimbo la shaba liwe nchi yani kuwe na nchi mbili humo ila Mobutu alipeleka jeshi na waliuwawa wanamgambo wote wakati wake watu waliopanga kupindua nchi au kumuua aliagiza wauwawe nchi ikawa na amani kwa miaka kama 25.
 
Back
Top Bottom