Rais wa Burundi mwenyekiti mpya EAC

mshale21

JF-Expert Member
Apr 8, 2021
2,049
4,904
Arusha. Rais wa Burundi, Evariste Ndayishimiye leo Ijumaa Julai 22, 2022 amechaguliwa kuwa mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

Rais Ndayishimiye amechukua nafasi ya Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta aliyemaliza muda wake.

Mwenyekiti huyo ametangazwa leo na Rais Kenyatta katika kikao cha kawaida cha 22 cha Wakuu wa nchi za Afrika ya Mashariki kilichofanyika leo jijini Arusha.

Kenyatta amesema katika kipindi cha uongozi wake Jumuiya hiyo imefanya maendeleo makubwa na alipewa ushirikiano na Wakuu wa nchi hizo, baraza la Mawaziri la Africa Mashariki na secretarieti ya jumuiya hiyo.

Rais Kenyatta amesema miongoni mwa mafanikio makubwa ya jumuiya hiyo,ni pamoja na kuanzishwa itifaki ya soko la pamoja ambayo imesaidia kuchochea uchumi kwa nchi wanachama.

"Leo ndio mkutano wangu wa mwisho wa EAC na Wakuu wa nchi napenda kueleza tumefanikiwa sana na kuna mambo ya kumalizia ikiwepo uanzishwaji shirikisho la kisasa la Afrika Mashariki na Somalia kujiunga rasmi na Jumuiya hii"amesema

Akizungumza baada ya kupewa jukumu la kuongoza Jumuiya hiyo, Rais Evariste Ndayishimiye amewashukuru Wakuu wa nchi hizo na ameahidi kuendeleza malengo ya Jumuiya hiyo.
 
Somalia tenahmmmm haya,,,,nawanajikutaga kama sio waAfrica kabisa hawa watu bora waende kwa waarabu huko!
 
Duh hadi magufuli asee huyu mwamba ni jiwe kwelikweli mzimu wake bado unawanyima usingizi
Hii jumuiya uchwara hii haina mvuto.

Jumuiya inaundwa na madikteta akina Mseven, Kagame, Magufuli (Rot In Hell), etal.
 
Back
Top Bottom