Rais wa Benki ya Dunia kuwasili nchini Jumapili

Rais wa Benki ya Dunia kuwasili nchini Jumapili

Kwa hiyo hawakulifikiria hilo kwenye original designs?
It's like unaharibu kitu on purpose just because you'll fix it baadae
Yea inawezekana kabsa....siku zote tanzania ufisad wote unasababishwa na technical team (consultants) ... Wanaamn wakiandika variation yoyote Ile itafanyiwa kaz..

Aisee nakubal kabsa wasom weng ndo wanaotuangusha kwel kwel...mfano jk international airport phase III.. Kujenga kwa jengo lenye 60000 Sq.m n kama billion. Mia moja na ushee.. Sasa mh.magu alipocheck zile drawing na kulingana na standard ama rate za AQRB tukajikuta tumepigwa kama billion Mia 4 na kitu..yaan mpaka contractor kapigwa...uccheze na watanzania...they are very dangerous..

Kwa hyo nnaamn wakat design zinafanywa kwenye huu mrad wa ubungo waliogopa kupitia kwenye design ila wanasubir kwenye post contract...let's wait Hawa jamaa watakuja na swagga gani
 
Rais wa Benki ya Dunia, Jim Yong Kim atawasili nchini kwa ziara ambayo madhumuni yake makuu ni kufanya maongezi na Rais Magufuli kuhusu masuala ya kiuchumi na biashara.

Jim Yong Kim pia ataweka jiwe la msingi katika ujenzi wa barabara za juu Ubungo(ubungo interchange) katika makutano ya barabara ya Sam Nujoma na Mandela ambao utagharimu zaidi ya Tsh bilioni 177.

Ujenzi huo unafanywa na Kampuni ya M/S China Civil Engineering Construction Cooperation ya China (CCECC).

Upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa ‘Ubungo Interchange’, ulifanywa na Kampuni ya M/S Hamza Associates ya Misri kwa kushirikiana na Kampuni ya Advanced Engineering Solutions Ltd ya Tanzania kwa gharama za dola za Marekani 440,540 sawa na Sh 951, 218,373.40 na kazi hiyo ilikamilika Desemba mwaka jana.

Mhandisi Mshauri kwa ajili ya usimamizi wa kazi ya ujenzi wa mradi huo ni Kampuni ya M/S DASAN Consultants ya Korea Kusini ikishirikiana na Kampuni ya AFRISA Consulting Ltd ya Tanzania, ambapo gharama za usimamizi ni Tsh 8,286,234,524.

Barabara za juu katika eneo la Ubungo zitajengwa kwa safu tatu, ambapo safu ya chini itatumika kwa magari yanayopita katika barabara ya Morogoro na magari yote yanayopinda kushoto.

Safu ya pili itajengwa katika urefu wa meta 5.75 kutoka usawa wa ardhi na itatumika kwa magari yote yanayopinda kulia ambayo yataongozwa pia na taa za barabarani.

Pia safu ya tatu itajengwa kwa urefu wa meta 12.5 kutoka usawa wa ardhi na itatumika kwa magari yanayopita barabara ya Mandela na Sam Nujoma na barabara zote zitakuwa na njia sita za magari ikiwa ni pamoja na njia mbili za magari ya usafiri wa mabasi yaendayo haraka.

Ieleweke kuwa zaidi ya magari 65,000 yanapita kila siku katika makutano ya barabara za Morogoro, Mandela na Sam Nujoma eneo la Ubungo, hali inayosababisha msongamano katika barabara ya Morogoro ambayo ndio lango kuu la kuingia na kutoka jijini Dar es Salaam.

15910077516_fd1876fa0d_b.jpg
Tunahitaji vyeti tu
 
Kuna watu hii ni habari mbaya. Ila sisi tunasema. Magufuli selema..hapa kazi tu.

Safi sana. Hii nchi kazi zinachapwa. Mungu murehemu rais wetu.
Amefariki lini huyu unayemwombea kwa Mungu kwamba amurehemu? Mods hebu mpigeni ban (hata ya saa tatu tu inatosha) huyu mtu akajifunze matumizi ya Kiswahili sanifu huko mitaani! Mkuu tengua hii kauli haraka kabla hujaitwa kwa kamanda Sirro!!
 
Rais wa benk ya dunia anatarajiwa kuitembelea Tanzani katika ziara ambayo ataweka jiwe la msingi la ujenzi wa flyover za ubungo.Tukumbuke kwenye kampeni za urais 2015 moija ya ahadi ya Rais Magufuli na Ilani ya CCM ni kujenga flyover jijini Dar ili kukabi.iana na tatizo la msongamano.N.B tumuhukumu Magufuli kwa ilani ya ccm na ahadi zake.
 
Okei, sasa nimeelewa zile shughuli pale pamoja na bomoa bomoa ni za nini? Nilikuwa sijui.
 
http://mtembezi.co.tz/2017/03/19/ra...ara-ya-juu-katika-makutano-ya-ubungo/#respond
ubungo-flyover.jpg


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kushirikiana na Rais wa Benki ya Dunia, Dkt. Jim Yong Kim wanatarajiwa kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara za juu (Ubungo interchange) eneo la Ubungo jijini Dar es Salaam Machi 20 mwaka huu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Habari na Mawasiliano, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano inasema kuwa mradi wa ujenzi wa barabara za juu katika makutano ya Ubungo yatagharimu takribani shilingi bilioni 188.71 ambapo una lengo kupunguza msongamano wa magari katika barabara za Morogoro, Nelson Mandela na Sam Nujoma.

“Mradi huo ni sehemu ya uboreshaji usafiri Jijini Dar es Salaam yaani (Dar es salaam Urban Transport Improvement Project), utakaogharimiwa kwa mkopo kutoka Benki ya Dunia na mchango wa Serikali ya Tanzania”

Aidha, taarifa hiyo ilisema kuwa, mradi huo utahusisha pia awamu ya tatu na ya nne ya ujenzi wa miundombinu ya mabasi yaendayo haraka (Bus Rapid Transit- BRT), katika barabara ya Nyerere kutoka katikati ya jiji la Dar es Salaam hadi Gongo la mboto na barabara ya Bagamoyo kutoka katikati ya jiji hadi Tegeta.
 
Nchi unajengwa kwa kweli. Licha ya mapungufu ya hapa na pale




ILA BASHITE FANYA UENDE SASA MAANA TUMECHOKA DRAMA SIYE
 
Hatuyataki hayo mabarabara yake wala viwanda,

"Atutolee bashite kwanza
 
Ngoja nirudi Kule kwingine, sababu huku hakuna jipya, maana kama ni kodi kwa ajili ya maendeleo ninalipa vizuri sana na sijawahi kukwepa...
 
Back
Top Bottom