Rais wa Benki ya Dunia kuwasili nchini Jumapili

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,171
23,991
Rais wa Benki ya Dunia, Jim Yong Kim atawasili nchini kwa ziara ambayo madhumuni yake makuu ni kufanya maongezi na Rais Magufuli kuhusu masuala ya kiuchumi na biashara.

Jim Yong Kim pia ataweka jiwe la msingi katika ujenzi wa barabara za juu Ubungo(ubungo interchange) katika makutano ya barabara ya Sam Nujoma na Mandela ambao utagharimu zaidi ya Tsh bilioni 177.

Ujenzi huo unafanywa na Kampuni ya M/S China Civil Engineering Construction Cooperation ya China (CCECC).

Upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa ‘Ubungo Interchange’, ulifanywa na Kampuni ya M/S Hamza Associates ya Misri kwa kushirikiana na Kampuni ya Advanced Engineering Solutions Ltd ya Tanzania kwa gharama za dola za Marekani 440,540 sawa na Sh 951, 218,373.40 na kazi hiyo ilikamilika Desemba mwaka jana.

Mhandisi Mshauri kwa ajili ya usimamizi wa kazi ya ujenzi wa mradi huo ni Kampuni ya M/S DASAN Consultants ya Korea Kusini ikishirikiana na Kampuni ya AFRISA Consulting Ltd ya Tanzania, ambapo gharama za usimamizi ni Tsh 8,286,234,524.

Barabara za juu katika eneo la Ubungo zitajengwa kwa safu tatu, ambapo safu ya chini itatumika kwa magari yanayopita katika barabara ya Morogoro na magari yote yanayopinda kushoto.

Safu ya pili itajengwa katika urefu wa meta 5.75 kutoka usawa wa ardhi na itatumika kwa magari yote yanayopinda kulia ambayo yataongozwa pia na taa za barabarani.

Pia safu ya tatu itajengwa kwa urefu wa meta 12.5 kutoka usawa wa ardhi na itatumika kwa magari yanayopita barabara ya Mandela na Sam Nujoma na barabara zote zitakuwa na njia sita za magari ikiwa ni pamoja na njia mbili za magari ya usafiri wa mabasi yaendayo haraka.

Ieleweke kuwa zaidi ya magari 65,000 yanapita kila siku katika makutano ya barabara za Morogoro, Mandela na Sam Nujoma eneo la Ubungo, hali inayosababisha msongamano katika barabara ya Morogoro ambayo ndio lango kuu la kuingia na kutoka jijini Dar es Salaam.

15910077516_fd1876fa0d_b.jpg
 
Mbona macompany mengi sana?kwao wanajenga hivyo?mlolongo mrefu sana ...
 
Kuna watu hii ni habari mbaya. Ila sisi tunasema. Magufuli selema..hapa kazi tu.

Safi sana. Hii nchi kazi zinachapwa. Mungu murehemu rais wetu.
Kumbuka moto yake ni HapaKaziTu.

Rais pia anatakiwa awe makini sana na hawa World Bank na IMF kwa sababu ni maajenti wa nchi za Magharibi ambazo zinatumia pesa katika unyonyaji wa kisasa.
 
Nafikiri jk angetunisha hazina kwa ujuo huu... Ila maswala ya kuomba kujengewa sijui kanisa....!?
 
Hizi thread za maendeleo huoni watu wakizishambulia,ila unganisha neno LISSU au BASHITE kwenye uzi unavyojaa fasta.Ndo maana magazeti ya UDAKU yanaongoza kwa mauzo,maana ni umbea,udaku,roho mbaya,ushindani wa kipuuzi ndo umewajaa vijana wa kitanzania % kubwa.
 
Hizi thread za maendeleo huoni watu wakizishambulia,ila unganisha neno LISSU au BASHITE kwenye uzi unavyojaa fasta.Ndo maana magazeti ya UDAKU yanaongoza kwa mauzo,maana ni umbea,udaku,roho mbaya,ushindani wa kipuuzi ndo umewajaa vijana wa kitanzania % kubwa.
Kuleta maendeleo ndio jukumu tulilokabidhi kwa serikali hatuwezi kupongeza maana hizi barabara Magufuli hatoi pesa zake za mfukoni. Lakini inapotokea mtu au kiongozi tunaemlipa na kumpa Huduma zote anafanya biashara zake kwenye ofisi ya umma kama bashite lazima tuwe wakali kama pilipili.
 
Alimkimbia katibu mkuu UN kwa kuwa hana fungu,sasa kamtuma mwenzie aje,ajenda ni zile zile ....Zanzibar na demokrasia ndipo upate mkopo
 
Back
Top Bottom