Mtoto halali na hela
JF-Expert Member
- Aug 10, 2012
- 55,633
- 55,249
Habari njema
Hii safiRais wa Benki ya Dunia, Jim Yong Kim atawasili nchini kwa ziara ambayo madhumuni yake makuu ni kufanya maongezi na Rais Magufuli kuhusu masuala ya kiuchumi na biashara.
Jim Yong Kim pia ataweka jiwe la msingi katika ujenzi wa barabara za juu Ubungo(ubungo interchange) katika makutano ya barabara ya Sam Nujoma na Mandela ambao utagharimu zaidi ya Tsh bilioni 177.
Ujenzi huo unafanywa na Kampuni ya M/S China Civil Engineering Construction Cooperation ya China (CCECC).
Upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa ‘Ubungo Interchange’, ulifanywa na Kampuni ya M/S Hamza Associates ya Misri kwa kushirikiana na Kampuni ya Advanced Engineering Solutions Ltd ya Tanzania kwa gharama za dola za Marekani 440,540 sawa na Sh 951, 218,373.40 na kazi hiyo ilikamilika Desemba mwaka jana.
Mhandisi Mshauri kwa ajili ya usimamizi wa kazi ya ujenzi wa mradi huo ni Kampuni ya M/S DASAN Consultants ya Korea Kusini ikishirikiana na Kampuni ya AFRISA Consulting Ltd ya Tanzania, ambapo gharama za usimamizi ni Tsh 8,286,234,524.
Barabara za juu katika eneo la Ubungo zitajengwa kwa safu tatu, ambapo safu ya chini itatumika kwa magari yanayopita katika barabara ya Morogoro na magari yote yanayopinda kushoto.
Safu ya pili itajengwa katika urefu wa meta 5.75 kutoka usawa wa ardhi na itatumika kwa magari yote yanayopinda kulia ambayo yataongozwa pia na taa za barabarani.
Pia safu ya tatu itajengwa kwa urefu wa meta 12.5 kutoka usawa wa ardhi na itatumika kwa magari yanayopita barabara ya Mandela na Sam Nujoma na barabara zote zitakuwa na njia sita za magari ikiwa ni pamoja na njia mbili za magari ya usafiri wa mabasi yaendayo haraka.
Ieleweke kuwa zaidi ya magari 65,000 yanapita kila siku katika makutano ya barabara za Morogoro, Mandela na Sam Nujoma eneo la Ubungo, hali inayosababisha msongamano katika barabara ya Morogoro ambayo ndio lango kuu la kuingia na kutoka jijini Dar es Salaam.
![]()
Hapa waliongea lugha gani mkuu??Ataongea naye kwa lugha gani?
KasomeMbona macompany mengi sana?kwao wanajenga hivyo?mlolongo mrefu sana ...
Ww ni mtanzania halisi,Mbona macompany mengi sana?kwao wanajenga hivyo?mlolongo mrefu sana ...
We inakuuma nn sasa!???Huyo rais wa benki ya dunia anaweza kupewa kuongea na waziri wa fedha au hata gavana wa benk maana mzee anaweza akawa yuko bize
Czan ila wakianza excution ya mrad lazma watalianngalia hilo kutoka kwenye point of design....ndo maana ya company kuwa nying kias hicho kwenye post contract il kuweza ku deal na changamoto ztakazo jitokeza...so wala ucwe na wac wacNaomba kuuliza. Hivi wamefactor in njia za mwendokasi za barabara ya sam nujoma from Mwenge to Buguruni endapo zitakuja kujengwa?
Execution ndio hiyo inaanza mwisho wa mwezi huu. Design zishakamilika wanataka waanze ujenzi. Au unamaanisha kwamba watakuja kurekebisha baadae kitu kimeshajengwa na kutumikaCzan ila wakianza excution ya mrad lazma watalianngalia hilo kutoka kwenye point of design....ndo maana ya company kuwa nying kias hicho kwenye post contract il kuweza ku deal na changamoto ztakazo jitokeza...so wala ucwe na wac wac
Hapana....mrad una phase 2... Pre contract na post contract stage...so mabadiliko yoyote yanapotokea site that means design team kama technical team na contractor kama mjenz hufanya site meeting na kuhakikisha kuwa design inakua friendly user...refer dart project...Execution ndio hiyo inaanza mwisho wa mwezi huu. Design zishakamilika wanataka waanze ujenzi. Au unamaanisha kwamba watakuja kurekebisha baadae kitu kimeshajengwa na kutumika
Kwa hiyo hawakulifikiria hilo kwenye original designs?Hapana....mrad una phase 2... Pre contract na post contract stage...so mabadiliko yoyote yanapotokea site that means design team kama technical team na contractor kama mjenz hufanya site meeting na kuhakikisha kuwa design inakua friendly user...refer dart project...
Kwa maisha ya kiafrica design inaweza fanya mrad uende mpaka zaid ya 50% more.....
Atampa kibarua cha ukalimani "mchungaji" Peter Msigwa. Usiwe na hofu.Ataongea naye kwa lugha gani?