Rais Vladimir Putin: Afrika haitokaa iwe huru

Rais Vladimir Putin: Afrika haitokaa iwe huru

WilsonKaisary

JF-Expert Member
Joined
Apr 4, 2017
Posts
392
Reaction score
954
"Afrika haitokaa iwe HURU. Waafrika wanawaamini Wazungu, Wamarekani na Wachina zaidi kuliko wanavyojiamini wao wenyewe....hawajiamini wao wenyewe hata kidogo.

Mzungu au mtu mweupe anafanya makosa Afrika tena makosa ya jinai ila hakuna hatua za kisheria zitakazochukuliwa dhidi yake kwa sababu mamlaka za Afrika zinatutazama sisi weupe kama miungu, jambo ambalo liko mbali sana na ukweli.

Mtu mweusi (Mwafrika) anaweza kuteswa, kunyanyaswa na hata kuuawa kinyama Ulaya lakini hakuna mamlaka yoyote ya Afrika inayoweza kuuliza wala kuhoji.

Waafrika wamejikubali na kuamini kuwa wao ni watu DHAIFU wasio na tumaini haswa linapokuja suala la kupambana na Wazungu, Wamarekani na Wachina. Mzungu, Mmarekani au Mchina anaweza kumdhalilisha, kumtukana, kumpiga na hata kumuua Mwafrika katika ardhi ya Afrika tena kwenye nchi yake au nje ya Afrika na Viongozi wa Afrika wataliona hilo na kila mmoja atajiweka kana kwamba hakuona wala kusikia.

Adui wa Mwafrika ni Mwafrika. Mwafrika mpe silaha, pesa au ahadi ya madaraka madogo tu kwa sharti moja tu la kumuua Mwafrika mwenzake, atamuua kinyama kuliko ulivyotarajia. Adui wa Mwafrika sio mzungu, sio Mmarekani wala sio mchina. Adui wa Mwafrika ni AKILI na fikra zake na ndio maana leo Wazungu, Wamarekani, Waarabu na Wachina wameitawala tena Afrika kwa kutumia dini, Elimu, uchumi, teknolojia, siasa na utamaduni.

Waafrika ni watu wanaochukiana na wasioaminiana na ndio maana Afrika haiwezi kuungana na haitokaa iungane kuwa na dola imara. Chuki ya wenyewe kwa wenyewe na utengano ndio inayowapa wakoloni wao nguvu ya kuendelea kunyonya rasilimali za Afrika."

Je unakubaliana na Rais Vladmir Putin?
 
Hizi chuki za wenyewe kwa wenyewe pia zinatoka na njaaa iliyopo Africa na kukosa hali ya kusubutu ya kujitegema kwa hali na Mali bila kuwaza msaada na pia tamaa za madaraka na ubinafsi wakutajirika kwa kundi la watu wa chache kujipalia Mali na kujilinda wakitumia kivuli kidogo Cha kuwaadawa watu wanawawekea mambo sawa huko mbeleni na wenyewe watakula mema ya nchi lakini hakuna ukweli Kila kiongozi anapambana kutengeneza msingi kula kwake na watu wake wa karibu.

Mataifa mengi ya Africa VIONGOZI WANATOKA madarakani wamejilimbikizia Mali wengine wanakufa zinapotelea kwenye mabank ya wenzetu Kuna haja ya kuanza mpango mazubuti wakupunguza kukopa kutoka kwa mataifa ya ulaya na kuanza kuja vitu vyetu vya ndani tutakuwa sawa tu mbeleni ataka Kama sio Karne hi basi hioo ijayo.

Africa tunaweza Kila mmoja akiamua kumjali mwafrica mwenzie Kama ndugu na tukiweka tofauti za kidini, Kisiasa na kikabila pembeni
 
Kwenye hili janga la corona kuna kidume mmoja tu kaamua kuwaonyesha wenzie kwamba uanaume ni pamoja na kuwa na maamuzi yako,bahati mbaya wenzake wanaendekeza umama.
 
Ni kweli safari bado ndefu sijui tunafanyaje labda kizazi cha nne kinaweza kuelewa
redemption song- bob Marley
 
Mkuu mimi nimemsikia lissu kwa mdomo wake akiwapigania mashoga jifunze kutafuta ukweli
Kweli putin hajakosea.yaani upo tayari kuedit uwongo ili mladi mwafrika mwenzako afeli.
Kuwa na siasa za kubishana kwa hoja sio kupigana risasi au kuvunjana miguu.
Siasa zipo tu umezikuta utakufa utaziacha grow up.
 
Haya maneno wazungu wengi waliowahi kuja Africa wanayajua. Mwalimu wangu prof Wolfgang H. Hauffe ni RAIA wa Sweden mwenye asili ya Germany alitwambia darasani 2010 (akiwa na miaka 76) kwamba hapa darasani mnaheshimiana , lakin mmoja wenu akipata mamlaka juu wengine he will start treating them like shit. Akaongeza Africa mnastahili kwanza kupendana na kuthaminiana kabla ya kutegemea nchi za ulaya kuwathamani. Prof Silvio do Bono (RAIA wa Malta) huyu ni mdogo nadhani early 50s, naye alisema msidhani wazungu wote ni wasomi au matajiri, kuna omba omba kuna vilaza hata kuliko huku Africa. Tatizo mnakubali upuuzi wote mnaoshauriwa na wazungu ambao hawajui chochote wala hali ya Africa kuhusu swala la maendeleo .Akasema mwafrica akiandaa job offer wakaiitwa watu interview akaja mzungu form six na mwafrica mwenye PhD , HR mwafrica atachukua mzungu form six na atakubali upuuzo wa mzungu na kudharau mawazo yenye akili ya mwafrica mwenzake. Bado tuna mental slavery , our minds are not yet free. Bado tunajiweka watu wa daraja la tatu. Na mbaya zaidi hii mentality iko ndani ya +90% ya waafrica ,wasomi na ambao si wasomi. So bado safari ipo
 
Hawezi kusema hivyo... Weka chanzo cha hiyo habari.
 
hakika japokua hayo maneno hapo juu hayawezi kusemwa namtu wakariba ya putin
 
Back
Top Bottom