Unajua, sehemu kubwa ya fahari ya jamii yoyote duniani hutokana na vitu walivyovibuni au kuviumba wao wenyewe. Waarabu walitoa mchango mkubwa kwenye mfumo wa namba, wazungu wameunda teknolojia na uvumbuzi usiohesabika, Wachina na Wahindi nao wameacha alama kubwa kupitia kazi na ubunifu wao.
Lakini ukimwangalia Mwafrika mara nyingi hutumia nguvu kubwa kujieleza kupitia mambo ambayo hakuyatengeneza mwenyewe. Atajivunia nguvu alizopewa kwa kuzaliwa, sura au maumbile yake.
Zaidi ya hapo, Mwafrika atajisifia kabila ambalo hakuliumba yeye, atajivunia milima na mandhari ambayo ni sehemu ya mazingira ya asili, au madini yaliyopo ardhini ambayo hakuyatengeneza yeye mwenyewe.
Changamoto kubwa si kuwa hatuna vya kujivunia, bali ni kwamba bado hatujawekeza vya kutosha kwenye ubunifu, utafiti na vitu vitakavyobeba alama yetu duniani kama Waafrika.