Rais uko wapi kuna wapigaji huku Sekondari ya Darajani, Moshi..

thegeniustzda

JF-Expert Member
Dec 14, 2017
211
358
Shule inaitwa Darajani Secondary School, ipo Moshi vijijini, Marangu..

Jamani huu ni wizi kweli kweli WAZAZI tunalipia laki na hamsini halafu shule nzima wapo 1,000 piga hesabu kwa laki na hamsini mara 1000; sasa ni elimu bure au elimu pesa? Na hii ni shule ya kata na Mheshimiwa Raisi alisema kuwa elimu ni bure!

Mkuu wa hii shule afuatiliwe. Watu wa vijijini tunaliwa sana then wanatulazimisha usipolipa unaitiwa mgambo aje kukukamata.

Jamani hii ni halali? Sambaza imfikie mheshimiwa Rais.. KIRIBIA MWANANGU ATARUDISHWA NYUMBANI TUSAIDIE
 
Hivi wewe umeridhika kua Elimu ni bure, in this world hakuna vya bure ,abure aghali pambana na hali yako
 
Shule inaitwa Darajani Secondary School, ipo Moshi vijijini, Marangu..

Jamani huu ni wizi kweli kweli tunalipia laki na hamsini halafu shule nzima wapo 1,000 piga hesabu kwa laki na hamsini mara 1000; sasa ni elimu bure au elimu pesa? Na hii ni shule ya kata na Mheshimiwa Raisi alisema kuwa elimu ni bure!

Mkuu wa hii shule afuatiliwe. Watu wa vijijini tunaliwa sana then wanatulazimisha usipolipa unaitiwa mgambo aje kukukamata.

Jamani hii ni halali? Sambaza imfikie mheshimiwa Rais..
Soma acha kulalamika usipende vya bure Elimu ndiyo msingi wa Maisha yako
 
Acha ujinga dogo lipa pesa upige shule! Huko uliko hakuna uongozi hadi uanze kumlilia rais? Ninyi ndo mnamlewesha sifa jamaa na kumfanya ajione yeye ndo each & everything hapa bongo, hadi anaingilia majukumu ya mwenyekiti wa kitongoji na kujikuta akipeleka lori mtaroni. Achana na vya bure havina ubora.
 
Kwahiyo hata kama miundombinu mibovu, wazazi mkae tu kwakuwa mmeambiwa elimu bure? Ikipita miaka mitano pasi kurekebishwa huyo mtoto atakuwa wapi na atakuwaje? Mengine ni ya kujiongeza tu. Hata hivyo Mh. Rais hajazuia jamii kushirikishwa ktk upatijanaji wa huduma za kijamii.
 
Kwamba unamtaka rais ahangaike na wapigajibwa shule ya Darajani Moshi, jambo hili linaonesha tatizo kubwa tulilo nalo.
 
Mleta post wewe ni Muongo, Fafanua kinaga ubaga, hiyo hela mnapo obwa mnaambiwa ni ya nini? Unajua isikje kua ni michango wa chakula chako unapo kua shuleni, harafu unakuja kuchafua uongozi wa shule,
Kila Fedha inakua na maelezo, ili tufatilie hii issues eleza ni michango ya nini, then utaona Matokeo ya post yako hii ndani ya wiki hii.
 
wazazi wanatuonea sana walimu magu anatoa hela ya chaki na vifaa vya kiofic tu hatoi hela ya chakula kumlipa mpishi au mlinz sasa sis tutoe mavuz wale au na wasipokula shule tutoe maelezo
 
Acha ujinga dogo lipa pesa upige shule! Huko uliko hakuna uongozi hadi uanze kumlilia rais? Ninyi ndo mnamlewesha sifa jamaa na kumfanya ajione yeye ndo each & everything hapa bongo, hadi anaingilia majukumu ya mwenyekiti wa kitongoji na kujikuta akipeleka lori mtaroni. Achana na vya bure havina ubora.
 
Kwahyo kutoa 150 kwa ajili ya chakula cha mtoto wako mwaka mzima umeona ni pesa nyingi sana!

Kwani hapo jirani hakuna shule jirani ambayo haina chakula ukamhamishia mwanao huko
 
Mfuate Ikulu. Pumbavuuuu!! mpenda bule wewe. Utaolewa na umasikini. Unajua nini maana ya elimu bule wewe...?? "Elimu bila malipo" Simba, C (2017).
 
Back
Top Bottom