DOKEZO Rais tunakuomba utupie jicho TARURA

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

koryo1952

JF-Expert Member
Mar 7, 2023
386
765
Tunaishukuru Serikali yetu inatoa fedha nyingi sana kwa TARURA ili iendeleze barabara zetu hasa za Vijijini. Kwa mtindo wa sasa labda siyo wote unapotakiwa kupata kazi lazima utoe rushwa to the tune mpaka 4 millioni.

Ukiisha kupewa kazi kuna mgao wa Ofisi ya RM Mkoa na Ofisi ya TARURA wilaya na hi ni lazima uitoe mpaka asilimia 10 ya malipo ya mkandarasi.

Tatizo hili ni kubwa na wengi wa Wakandarasi hawana la kufanya. Kama nasema uongo fanyeni utafiti kwa Wakandarasi na hapa mtakuja kufahamu ukweli.
 
F4YNuiFXAAAFWfP.jpeg
 
We taja tu ni Tarura Mkoa gani basi. Wakuu watashughulika... Ila ukiandika hivyo too general haitasaidia
 
Rais Dkt Samia anayo habari ya madudu yoote kabisa, kilichopo sasa ni kufukuzwa wahusika na wengine watauawa kwa kupigwa risasi kama majambazi. Subiri moto wake ni mkali mno, waidhani Dkt Samia ni wa kuchezea, si mmeona moto wake leo katimua DC na bado. Homera nje etc subirini. Yaani uzuri lile jeshi la awamu ya 5 la wafuatiliaji lipo kazini 24/7 na lina kila info kwa sasa.

Tena huko halmashauri ndiyo balaa unakuta ma MT NA DT wameharibu mifumo ya ukusanyaji mapato na kutengeneza njia zao ni wengi mno watapukutishwa labda wakimbie nchi hahahaha, watalia na kujuta bora Dkt Magufuli aliyekuwa anakemea huyu Dkt Samia kimya kimya tu kibano na kuondoa kabisa wajinga wote. Ndiyo maana tunasema hata bandari acha ije maana Dkt Samia anayonia njema kabisa.
 
#Mama Kaja
 
Kuna watu wana comment hapa utasema sio wao wanaotoa Rushwa kwa Matrafiki humo barabarani.

Hii nchi yote imejaa Rushwa

Anzia Rita
Nenda Polisi
Nenda Uhamiaji n.k

Sekta yote ya Ujenzi ina rushwa
Hivi ni nani akupitishie malipo ya milioni 500 alafu yeye abaki anasubiria Mshahara wake wenye makato mwisho wa mwezi wa shilingi milioni 2 ?

Nenda kwenye Chaguzi za Chama cha Mapinduzi, bila Rushwa hupati uongozi

Mwaka 2020 nilijidai kwenda kugombea Ubunge.

Hata kura 5 sikupata kwa kutotoa rushwa

Hii Nchi inahitaji reforms
 
Kinachohitajika nikuepuka kuwa kero kwa wananchi. Tatizo hawa wamejiundia kamtandao kao. Ole ukikutwa!
 
Uzalendo unahitajika kuanzia Juu hadi huku Chini.

Kuna maeneo mengine bila kutoa rushwa hupati huduma
 
Mameneja wote wa TARURA Mkoa wa Mara wanatakiwa wafukuzwe kazi na hasa Meneja wa Wilaya ya Tarime. Ukiomba kazi na kukubaliwa upate mradi fulani lazima utoe 4 millioni na ukiishapewa kazi thamani ya kazi uliyopewa mfano Tshs. 200m lazima utoe 10% yaani lazima umpe 20m. Fanyeni utafiti kwa Wakandarasi wa Mkoa wa Mara.
 
Mkuu meneja yupi kaomba rushwa?
 
Kwanini tarura isifumuliwe ibaki tanroads peke yake?
Walioanzisha waliona mbali na mzigo mkubwa waliokuwa nao Tanroads hata wakiifumua kama mifumo ya rushwa bado ipo pale pale haisaidii..bora ungesuggest irudi idara ya ujenzi kama ilivokuwa awali lkn kwangu mm.naona hawakukosea kuanzisha hiyo mamlaka inafanya vizuri japo mapungufu madogo madogo yapo
 
Back
Top Bottom