Rais tuhutubie

Rais tuhutubie

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2012
Posts
10,353
Reaction score
26,194
1.Rais tuhutubie,ukweli utuambie,waongozwa sie,tunakuomba Mheshimiwa. 2. Ya Sensa yamepita,ya Ponda yanaita,UAMSHO wajikita,tunaomba hotuba. 3. Tunataka kusikia,wapi mmefikia,matatizo kututatulia,tuhutubie Mkuu. 4. EPA ndio basi? RICHMOND ndio kasi? Mafisadi ni waasi? Tupe majibu Rais. 5. Tunahitaji kujua,gamba kujivua,wapi imeishia,CHADEMA wanatishia,ni vyema tukaambiwa. 6. Vipi mwaka ujao,tukae wa kula mkao,au bado peke yao. Tuweke wazi Mkuu. 7. Do you have solution,kwa migomo vyuoni,na mishahara Serikalini? Tuweke wazi Rais. Happy new year to you all!
 
Kweli raisi inabidi utuhutubie leo mwisho wa mwaka!
 
Nadhani wana Type hotuba subirini wakimaliza wafanye editing alafu apewe mkuu wa kaya kuwasomea wananchi. Kuweni na subra ngoja ni wa text waongeze speed ya ku type
 
...ndugu Mselewa,

1. Avatar yako (ni kweli hawaivi na ndugu yake na huyo Nkunda???)
2. Aina ya maswali uliyouliza (ni ya kweli ila machungu)

...utaambiwa umetumwa na hao CDM au unaleta uchochezi, ngoja wakereketwa wapite huku....
 
NAUNGA MKONO.
1. Inatakiwa kujua kama nchi priorities za 2013 zitakua ni zipi ukiachana na suala la KATIBA

2. Yeye kama raisi wetu angependa a achieve nini kwa mwaka 2013

3. Tujue nini tumeweza, na nini tumeshindwa kutimiza mwaka 2012 na jinsi gani amedhamilia kumalizia kwa mwaka 2013

4. namtakia raisi HAPPY NEW YEAR.
 
...ndugu Mselewa,

1. Avatar yako (ni kweli hawaivi na ndugu yake na huyo Nkunda???)
2. Aina ya maswali uliyouliza (ni ya kweli ila machungu)

...utaambiwa umetumwa na hao CDM au unaleta uchochezi, ngoja wakereketwa wapite huku....

Si umeona Mkuu Rais kahutubia?
 
Back
Top Bottom