Rais Trump: Rekodi zake si mchezo

Iceman 3D

JF-Expert Member
Sep 3, 2016
20,614
67,078
Rais wa 45 wa Marekani, Donald J Trump ni moja ya binadamu wenye mafanikio sana duniani, japo kisiasa watu wanaweza kumbeza lakini huyu ni mtu ambaye anajua maana ya mafanikio, wakati wa mahojiano yake kipindi ana anza kugombea urais alisema 'I always win, I am a winner" maisha yake japo yamekuwa na kupanda na kushuka yana rekodi mbalimbali.

Zifuatazo ni baadhi tu ya rekodi za Maisha ya bwana Trump;

Trump; mafanikio kama mfanyabishara na raia wa kawaida

1. Trump yuko kwenye kitabu cha rekodi za dunia cha guinness, kwa kuwa mfanya biashara aliye wahi kufanya "biggest financial turnaround in history", kwani Alikuwa bilionea aka filisika na kuwa na madeni yanayofikia dola za marekani Bilioni moja, alijikwamua na kurudi kuwa bilionea tena. Ni rekodi ya dunia hiyo

2. Trump pia yuko kwenye kitabu cha guiness kwa kuweza kufanya dili ya haraka ya zaidi iliyo husisha mamilioni ya dola, ambapo ali present plan zake kwa dakika tatu na wakakubaliana na bwana Ricardo Ballino kufanya dili hiyo ya pesa nyingi.

3. Donald Trump ni binadamu aliyefanikiwa kutoa hotuba na kulipwa pesa nyingi kwa saa, kabla ya kuingia kwenye siasa alikuwa akichaji dola za marekani milioni 1.5 kwa lisaa. Alikuwa akitoa semina za real estate expose.

4. Donald Trump, ni mmoja kati ya wamarekani 256 tu ambao ni mabilionea.

5. Donald Trump, amefanikiwa ku pata heshima na tuzo mbali mbali kama mwana burudani, kama vile Hollywood walk of fame, kwa mchango kwenye burudani, na WWE hall of fame kwa mchango wake kwenye mchezo wa mieleka.

6. Ni mwandishi mbali mbali wa vitabu ambavo viliuza zaidi, kitabu maarufu kikiwa Art of the deal ambacho kiliuza zaid miaka ya 80, pia ni moja ya vitabu vitano vya juu kuuza zadi kwa kufikisha nakala milioni moja zilizo uzwa, kwa kizungu tuna seme best seller.

7. Donald Trump, amewahi kuongoza kipindi cha burudani namba moja kwa Amerika, ambacho ni the apprentice, kwa wale mnao kumbuka miaka ya 2005 tumeangalia sana hiko.

Trump: Rekodi za Siasa

1. Rais Tajiri kuliko wotee waliopata kuwepo marekani ana kadiriwa kuwa na utajiri wa usd bilioni3-5

2. Rais aliye shika madaraka akiwa na umri mkubwaa kuliko wote kwenye historia ya USA, alikuwa na miaka 70.

3. Rais pekee wa Marekani ambaye hakuwahi kuwa mwanasiasa au kiongozi mkubwa wa jeshi, haija wahi tokea hii.

4. Rais pekee ambaye amewahi kuoa zaid ya mara 2. Wenzetu hujali sana familly value talaka zikizid huwa ni ngum kuchaguliwa ila jamaa alipenya.

5. Trump ni mgombea pekee ambaye anadhaniwa alishindwa midahalo yote mitatu na akafanikiwa kushinda urais

6. Trump ni mgombea pekee katika miaka 40 kutoweka wazi malipo yake ya kodi na kushinda uraisi.

7. Trump ni mgombea pekee ambaye, pamoja na kuchukiwa kuliko wagombea wote kwenye historia ya marekani, bado alishinda uraisi(Alikuwa ana kubalika kwa asilimia 32 tu)

8. Trump ni mgombea pekee ambaye alipoteza kura za jumla karibu milioni 3 na bado alifanikiwa ku ukwaa urais wa Marekani.

9. Pamoja na kupingwa na Rais, makamu wake, first lady, speaker , mawaziri, maseneta na viongozi wa chama chake woote, ni watu wa wili tu wa marekani waliowahi kufanikiwa kushinda vikwazo kama hivo na kuwa marais wa Marekani, Andrew Jackson 1828,na Donald Trump 2016.

Umpende au usimpende lazima tukubali kuwa Rais Trump ni moja ya binadamu ambao wamefanikiwa kwenye maisha yao.

Chanzo: ka gugo tuu, vyote hivo utaviona.
 
Duh hiyo No1 kibongo bongo hata muuza genge akifilisika japokuwa mtaji wake ni mdogo usiozidi 100,000/= anaoweza hata kukopeshwa anaweza asirudi mchezoni akaishia kunywa viroba tu kwa mawazo atakayokuwa nayo.kufilisika kabisa sio jambo dogo hata kidogo watu hufikia kujiua.
 
Duh hiyo No1 kibongo bongo hata muuza genge akifilisika japokuwa mtaji wake ni mdogo usiozidi 100,000/= anaoweza hata kukopeshwa anaweza asirudi mchezoni akaishia kunywa viroba tu kwa mawazo atakayokuwa nayo.kufilisika kabisa sio jambo dogo hata kidogo watu hufikia kujiua.
Hahahaha
Wana sema kipindi ambacho Trump alikua ana Daiwa Bilioni moja
Ali pita na binti yake kwejye mitaa wanayo ishi omba omba na homeless, aka mwambia binti yake kuwa, hawa omba omba hapo walipo wana thamani ya bilion moja na zaid kuliko mimi.
Tatizo tu hawajui wata tokaje walipo na kuanza maisha upya.
 
Lakini ameshikwa kichwa na Putin wa Russia, ndio anaiendesha us kwa sasa.
 
Back
Top Bottom