GE2025 Rais TLS ampigia chapuo Nkuba Ubunge Kahama Mjini

GE2025 Rais TLS ampigia chapuo Nkuba Ubunge Kahama Mjini

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Elias Msuya

Platinum Member
Joined
Dec 23, 2011
Posts
264
Reaction score
1,008
Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Boniface Mwabukusi amewaomaba wananchi wa Kahama Mjini kumchagua Sweetbert Nkuba aliyewania kugombea ubunge endapo atapitishwa na chama chake cha CCM.

Wakili Mwabukusi ameandika katika ukurasa wake wa Facebook baada ya Nkuba kumtembelea ofisini kwake Dar es Salaam.

Itakumbukwa kuwa Nkuba alikuwa mpinzani wa karibu katika kinyang’anyiro cha urais wa TLS mwaka 2024 kilichompa ushindi Mwabukusi.

“Ungeniuliza Maoni yangu ningewaambia wana Kahama hakuna sababu zozote za kutompa nafsi hii ya Utumishi. Ubunge una muhitaji na Taifa lina muhitaji ana uthubutu na Ubunifu ndani yake.

Tumefahamiana kwa zaidi ya Niaka 15 sina mashaka na Msomi Huyu. Ni mtu bora na ni muhimu kuwa na watu hawa Bungeni.

“Tunahitaji Bunge litakalo kuwa na watu makini watakao saidi kukirejesha Bunge katika Uwajibikaji na Ufanisi wa Kikatiba,” ameandika.

522630966_24068230909452376_8433476222537087236_n.jpg
 
Back
Top Bottom