Rais Samia, watake radhi watu wenye ulemavu wa macho

espy

JF-Expert Member
Oct 26, 2021
284
516
Wengine wamechipuka tu, wakaona dunia ndio hii hapa, wakawa kama kipofu kaona jogoo, kila unachomwambia, kama jogoo? Kama jogoo? Kumbe aliona jogoo macho yakafumba tena, kwa hiyo anachokijua duniani ni jogoo tu.


View: https://youtu.be/xvzea3alrRg?t=1293

Sasa dunia ya leo upeo wa watu kuheshimu watu wenye ulemavu umeongezeka, ndio maana hata neno vipofu halitumiwi kwenye mazungumzo rasmi na ya watu walioelimika. Kiongozi hategemewi kwenye hotuba mbele ya Taifa kutumia mifano ya kuwafanya walemavu wajisikie kama watu washamba, hawajawahi kuiona dunia kwa mapana yake, na wasio na hadhi yeyote, kwa sababu tu ya maumbile yao. Maumbile ambayo wao hawakuyachagua. Rais wetu hakika una exposure kubwa ya kutembea duniani, you know better, and should do better.

Rais Samia tafadhali watake radhi Watanzania wenye ulemavu wa macho.
 
Kwa ukweli kabisa siku hizi za karibuni huyu mama amekuwa anatamka maneno ya ajabu ajabu kama vile sio kiongozi. Sijui ni kujisahau au ni hulka yake iliyokuwa imejificha?

Kwa hali ilivyo na maneno yake ya hovyo sasa hivi ataanza kujibiwa naye kwa mwenendo huo huo na ataaibika sana
 
Madam kheri?
Long time no see..

Turudi kwenye uzi;
Kwanza matumizi ya maneno yeyote yenye kuonyesha unyanyapaa kwa kundi fulani, kutokana na hali ama maumbile yao haupaswi kutumika hata kidogo. Hii haiwahusu watu wa kawaida tu, hata viongozi wa ngazi za juu wanaobeba taswira ya nchi.

Sijaisikiliza clip yote uliyoipakia kwa sababu ni ndefu na yenye kuhitaji kuifatilia kwa muda mrefu.

Lakini, pamoja na kuwa upofu ni hali ya kushindwa kuona kwa ukamili maumbo na mwanga lakini ina maana nyingine katika nyanja mbalimbali.

Kama ambavyo nimetanabaisha kuwa sijaisikiliza na kujua alivyoitumia, lakini kuna namna ikitumika inakuwa haikusudii unyanyapaa kwa watu husika. Mfano akisema 'watu wana upofu wa kisheria', bila shaka amekusudia kufikisha ujumbe kuwa watu wanakosa uelewa na uzingatifu wa mambo kisheria.

Sehemu pekee ambapo mtu anakuwa amekusudia kuwakosea heshima watu hao ni kutumia maneno ya moja kwa moja.
 
Back
Top Bottom