Rais Samia Walinde Watanzania Dhidi ya Mauaji ya Pikipiki

Ajali ni ajali tu, mbona magari yanaua sana
Jiulize, hivi inakuwaje magari yanayobeba abiria wengi kwa mpigo, idadi ya vifo vinavyotokana na ajali za magari kuzidiwa na idadi ya vifo vinavyotokana na pikipiki ambayo kwa kawaida huwa inabeba abiria mmoja tu?

Hii ina maana frequencues za ajali za pikipiki zipo juu sana.

Kipindi cha miaka kama minne hivi zilitolewa takwimu za vifo vinavyotokana na ajali za pikipiki, kwa wastani ilikuwa ni watu 10 kwa siku moja. Sijui kwa sasa ni watu wangapi!! Lakini kwa mwaka ule vifo vilivyotokana na pikipiki vilizidi vifo vil8vyotokana na ajali za magari.
 
Bodaboda ni mojawapo ya usafiri wa hovyo sana wa kimaskini.
 
Sheria Kali hakuna..iwekwe Sheria Kali sana na mfumo tu kama ule wa trafiki kusoma plate number yaani bodaboda ukikamatwa na kosa pikipiki inataifishwa ....
 
Wakati mwingine inasikitisha sana, tatizo boda boda wenyewe hawaji hurumii, hwana chakupoteza wala hawana hofu yoyote wanapokuwa barabarani, vitu wanavyofinya inabidi utafakati mara mbili mbili...

Kuna dogo mmoja amefariki majuzi tu hapa kwa ajali na bodaboda yake, yani jioni mtu unaongea nae mzima wa afya kesho mchana unaambiwa kapata ajali kafa.. !

Confidence na ujasiri wao barabarani nafikiri unatokana na kuwa wana Drive Under Influence: matumizi ya madawa , bangi, double kick, na vilevi vingine . .

Kwasababu mtu ambaye akili yake ipo sober by default, ubongo wako unauwezo wakujihami nakukuzuia usifanye maamuzi yatakayopelekea wewe uumoe au kuingia kwenye hatari !
 
Leo hii, japo pikipiki zimekuwa ni chombo kinachotegemewa na wengi kwa usafiri lakini kwa upande mwingine zimekuwa janga kwa Taifa. Hazijawa janga kwa Taifa kwa sababu zenyewe ni janga kwa asili yake bali kwa sababu ya unafiki wa Serikali.

Kuna wakati Polisi walitaka kudhibiti uendeshaji ovyo wa pikipiki lakini wanasiasa na viongozi wa Serikali wanafiki wakazuia zoezi hilo.

Kwa wakati tofauti, nimeshuhudia vifo vya watoto wawili, watu wazima watatu waenda kwa miguu, waebdesha pikipiki wawili na ulemavu wa mama mmoja, vyote vikiwa vimesababishwa na uendeshaji wa ovyo wa pikipiki.

Kifo cha kwanza kilikuwa cha mtoto wa shule wa kike mjini Singida. Nilitoka Dodoma, naelekea Mwanza, watoto walikuwa wametoka shule, nikawa naendesha gari taratibu kwaajili ya usalama wa watoto, lakini mbele yangu ilkuja pikipiki, uendeshaji wake ni kama wa mtu kichaa, kwa kasi ilipishana na gari langu, nilishangaa. Mara nilisikia kishindo kwa nyuma, nikatizama kwenye side mirror, mwendesha pikipiki akawa tayari amemgonga binti mdogo, wa darasa la 4. Niligeuza haraka gari, nikasaidiana na akina mama wawili walikuwa karibu, tukamkimbiza mtoto hospitali ya mkoa wa Singida. Simanzi ikiwa imenijaa, masikitiko yasiyoelezeka. Sikuondoka, nilitaka nijue maendeleo yake. Baadaye mama mzazi wa mtoto alifika. Baadaye nikaongea na daktari tena, naye akanihakikishia kuwa mtoto amepata fahamu anaendelea vizuri. Nikashusha pumzi nikaondoka. Lakini nilipenda sana nijue maendeleo ya yule mtoto, bahati mbaya sikuchukua mawasiliano ya mtu yeyote.

Wiki 2 baadaye nilipopita eneo lile, nilisimama kuulizia yule mtoto aliyegongwa na pikipiki alikuwa anaishi wapi. wakanionesha nyumba, lakini hawakuniambia kuwa alifariki. Kumbe haikuwa mbali na pale, nikaoneshwa, hatua kama 30 tu toka barabarani. Mama yake mzazi alikuwa ameketi nje. Nikamsalimia, nikamwuliza yule mama, mtoto anaendeleaje, ndipo akanikumbuka, mara akaanza kulia, akaniambia, "Baba, ulipoondoka, ilipita kama nusu saa tu, mtoto akafariki. Nilikuwa na mtoto huyo tu". Machozi yalinitoka, mpaka leo nikipita pale Singida, eneo lile, kumbukumbu mbaya ile haikosi kunijia.

Mwezi huo huo, siku moja nilimpigia rafiki wa siku nyingi, nilitaka nimpe kazi fulani, akanijibu kuwa yupo msibani Ifakara, kumzika Kaka yake aliyegongwa na pikipiki mjini Dar es Salaam.

Siku nyingine, nimetoka Dodoma, naelekea Kahama, nikawa nimekubaliana na jamaa mmoja, kuwa nipitie Tabora kwa mazungumzo ya kikazi. Nikiwa nimefika Itigi, akanipigia simu kuwa haitawezekana kukutana kwa sababu Dada yake amegongwa na pikipiki, amefariki Dunia.

Nikiwa Dar es Salaam, nilipigiwa simu na Admin Manager, kuwa mfanyakazi wetu mmoja, mama yake mzazi amegongwa na pikipiki hujo Njombe, amevunjika vibaya sehemu mbalimbali. Baadaye nilitumiwa picha za majeruhi, ni ngumu kuamini kuwa ni ajali ya pikipiki, mpaka leo hii, hajaweza kutembea, na hana fahamu kwa sababu ya damage ya kichwa.

Kazini tuliamua kuwapa mikopo wafanyakazi wetu. Baadhi waliamua kununua pikipiki. Naambiwa jioni wakitoka kazini waliamua kuzitumia pikipiki zao kubebea abiria. Mmoja aligonga nguzo ya umeme, alitaka kulipita gari kwa upande wa kushoto, gari aliyotaka kuipita ilikuwa inapishana na gari nyingine kwenye barabara za mtaani, akafariki palepale.

Mwingine alianguka baada ya kugonga pavement ya barabara, akafariki.

Mtu mmoja, kaka yake, mama mmoja niliyekuwa nafahamiana naye sana, akiwa amesimama pembeni ya barabara, aligongwa na pikipiki, naye kwenda kugongesha kichwa kwenye barabara Shinyanga mjini, karibu na daraja la kuelekea Mwanza, alifariki palepale. Nilihudhuria maziko yake.

Mjini Mwanza, nililetewa taarifa kuwa mtoto wa shule amegongwa na pikipiki akiwa anavuka barabara, ikanilazimu kuhudhuria msiba kwa sababu mmoja wa ndugu wa marehemu ni mfanyakazi wetu.

Nimeyataja matukio haya kuonesha ukubwa wa tatizo lililopo. Mimi ni mmoja, nimeshuhudia haya, ni mangapi ambayo yanaendelea kutokea, ambayo sikupata kuyasikia?

Serikali imekuwa kama mzazi ambaye anaogopa kumpokonya mtoto mdogo anayechezea kisu kwa hofu kuwa akimpokonya atalia, huku akimweka mtoto wake kwenye hatari. Mzazi wa namna hiyo ni mjinga, mnafiki, na ni muuaji kwa kushindwa kutimiza wajibu wake kama mzazi.

Leo hii, waendesha pikipiki, hawafuati sheria yoyote ya barabarani.

Hawasimami kwenye taa inapotakiwa kusimama, hawasimami kwenye vivuko vya waenda kwa miguu hata kama watu wanavuka, wana-overtake upande wowote wanaoutaka, hawafuati speed limits, wanabeba mizigo hata isiyoendana na uwezo wa pikipiki (fikiria pikipiki inabeba mbao)! Hii ni nchi ya namna gani?

Ukiuliza ni kwa nini wameachwa hivi, Polisi wanasema kuwa Serikali imewazuia wasibughudhiwe, kwa kuwa waendesha pikipiki ni wengi, wataichukia Serikali, na kisha kuinyima CCM kura. Jambo la ajabu sana. Hivi kuwaachia hawa waende tu ovyo barabarani, hiyo Serikali haioni inawaweka kwenye hatari ya kifo waendesha pikipiki wenyewe, abiria wanaowabeba na waenda kwa miguu?

Serikali, ina maana ipo tayari wananchi waendelee kufa na wengine kuwa vilema, lakini wao wapate tu kura? Huu ni unafiki wa hali ya juu.

Nimeenda baadhi ya nchi, moja ya nchi ambazo nilivutiwa sana na uendeshaji pikipiki ni Burkina Faso. Pikipiki zinafuata sheria zote, kama yalivyo magari. Kwa nini hatupendi kuiga mambo mazuri kama hayo?

Kujifanya watu wema, kwa waendesha pikipiki wavunja sheria, hakuwasaidii wavunja sheria wenyewe, wala raia wengine wote kwa ujumla.

PENDEKEZO
1) Waendesha pikipiki wote (hasa za biashara), wapewe mafunzo kwa awamu kwa gharama ya Serikali. Akishamaliza mafunzo, apewa tag atakayoivaa shingoni. Abiria watahadharishwe kutopanda pikipiki ya waendeshaji wasio na tag.

2) Waendesha pikipiki za biashara wote, wapewe miezi 3, kila mmoja awe amehudhuria mafunzo na kupewa tag. Baada ya kipindi hicho kwisha, kusiruhusuwe mwendesha pikipiki asiye na mafunzo na tag, kuonekana na pikipiki barabarani.

3) Mwenye tag, akivunja sheria, anyang'anywe tag, azuiwe kuendesha, aende mafunzoni tena, kisha apewe tag nyingine.

Jukumu la msingi la Serikali yoyote Duniani ni usalama wa watu wake. Serikali ikishindwa kwenye hili, inakuwa haina uhalali wa kendelea kuwepo.

Nchini mwetu, siasa za unafiki, uwongo na hila, mara nyingi zimelididimiza na zinaendelea kuliangamiza Taifa letu, kila awamu yake, kwa viwango tofauti, kutegemeana na kiongozi mkuu wa nchi ni mtu wa namna gani.

Ni vema kwenye katiba mpya, iwekwe wazi katika kyzuia uongozi wa unafiki unaohatarisha usalama wa wananchi.
Mji wa makambako wametengeneza barabara kwa ajili ya bodaboda na bajaj tu.
Nadhani mamlaka zingine za miji wakajifunze hapo makambako.
 
Juzi nimemwona kijana amekaa upande mmoja huku anaendesha pikipiki...nikajisemea moyon"kifo huwa mnakiita wenyewe"!!
 
Uko sahihi,Pikipiki ni majanga sana kwa nchi hii, mimi mpaka sasa nimeshapata ajali zaidi ya saba na zote wananisababishia boda kwa uzembe wao,nikiona pikipiki sasa hivi inanikaribia naingia na woga na kuamua tu nimpishe njia, ni bora nipaki apite then niendelee.

Kuna siku siisahau nilikuwa naovertake gari, boda yuko mbele ya ile gari kwa hiyo nilishafanya timing ya kuovertake gari pamoja na boda, nikaona kama ameyumba kutaka kuja upande wangu,nikapiga honi nikiashiria kuwa ninaovertake, akarudi upande wake nikajua kanielewa, nilipokuwa naimaliza ile gari ili nimpite na yeye akakatiza mbele yangu ghafla kuja upande wangu akavuka upande wa pili, yani ilibidi nipark gari nianze kumtafakari,na hapo alikuwa kabeba abiria nyuma...
Jamiiforum kila mtu ana gari [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Leo hii, japo pikipiki zimekuwa ni chombo kinachotegemewa na wengi kwa usafiri lakini kwa upande mwingine zimekuwa janga kwa Taifa. Hazijawa janga kwa Taifa kwa sababu zenyewe ni janga kwa asili yake bali kwa sababu ya unafiki wa Serikali.

Kuna wakati Polisi walitaka kudhibiti uendeshaji ovyo wa pikipiki lakini wanasiasa na viongozi wa Serikali wanafiki wakazuia zoezi hilo.

Kwa wakati tofauti, nimeshuhudia vifo vya watoto wawili, watu wazima watatu waenda kwa miguu, waebdesha pikipiki wawili na ulemavu wa mama mmoja, vyote vikiwa vimesababishwa na uendeshaji wa ovyo wa pikipiki.

Kifo cha kwanza kilikuwa cha mtoto wa shule wa kike mjini Singida. Nilitoka Dodoma, naelekea Mwanza, watoto walikuwa wametoka shule, nikawa naendesha gari taratibu kwaajili ya usalama wa watoto, lakini mbele yangu ilkuja pikipiki, uendeshaji wake ni kama wa mtu kichaa, kwa kasi ilipishana na gari langu, nilishangaa. Mara nilisikia kishindo kwa nyuma, nikatizama kwenye side mirror, mwendesha pikipiki akawa tayari amemgonga binti mdogo, wa darasa la 4. Niligeuza haraka gari, nikasaidiana na akina mama wawili walikuwa karibu, tukamkimbiza mtoto hospitali ya mkoa wa Singida. Simanzi ikiwa imenijaa, masikitiko yasiyoelezeka. Sikuondoka, nilitaka nijue maendeleo yake. Baadaye mama mzazi wa mtoto alifika. Baadaye nikaongea na daktari tena, naye akanihakikishia kuwa mtoto amepata fahamu anaendelea vizuri. Nikashusha pumzi nikaondoka. Lakini nilipenda sana nijue maendeleo ya yule mtoto, bahati mbaya sikuchukua mawasiliano ya mtu yeyote.

Wiki 2 baadaye nilipopita eneo lile, nilisimama kuulizia yule mtoto aliyegongwa na pikipiki alikuwa anaishi wapi. wakanionesha nyumba, lakini hawakuniambia kuwa alifariki. Kumbe haikuwa mbali na pale, nikaoneshwa, hatua kama 30 tu toka barabarani. Mama yake mzazi alikuwa ameketi nje. Nikamsalimia, nikamwuliza yule mama, mtoto anaendeleaje, ndipo akanikumbuka, mara akaanza kulia, akaniambia, "Baba, ulipoondoka, ilipita kama nusu saa tu, mtoto akafariki. Nilikuwa na mtoto huyo tu". Machozi yalinitoka, mpaka leo nikipita pale Singida, eneo lile, kumbukumbu mbaya ile haikosi kunijia.

Mwezi huo huo, siku moja nilimpigia rafiki wa siku nyingi, nilitaka nimpe kazi fulani, akanijibu kuwa yupo msibani Ifakara, kumzika Kaka yake aliyegongwa na pikipiki mjini Dar es Salaam.

Siku nyingine, nimetoka Dodoma, naelekea Kahama, nikawa nimekubaliana na jamaa mmoja, kuwa nipitie Tabora kwa mazungumzo ya kikazi. Nikiwa nimefika Itigi, akanipigia simu kuwa haitawezekana kukutana kwa sababu Dada yake amegongwa na pikipiki, amefariki Dunia.

Nikiwa Dar es Salaam, nilipigiwa simu na Admin Manager, kuwa mfanyakazi wetu mmoja, mama yake mzazi amegongwa na pikipiki hujo Njombe, amevunjika vibaya sehemu mbalimbali. Baadaye nilitumiwa picha za majeruhi, ni ngumu kuamini kuwa ni ajali ya pikipiki, mpaka leo hii, hajaweza kutembea, na hana fahamu kwa sababu ya damage ya kichwa.

Kazini tuliamua kuwapa mikopo wafanyakazi wetu. Baadhi waliamua kununua pikipiki. Naambiwa jioni wakitoka kazini waliamua kuzitumia pikipiki zao kubebea abiria. Mmoja aligonga nguzo ya umeme, alitaka kulipita gari kwa upande wa kushoto, gari aliyotaka kuipita ilikuwa inapishana na gari nyingine kwenye barabara za mtaani, akafariki palepale.

Mwingine alianguka baada ya kugonga pavement ya barabara, akafariki.

Mtu mmoja, kaka yake, mama mmoja niliyekuwa nafahamiana naye sana, akiwa amesimama pembeni ya barabara, aligongwa na pikipiki, naye kwenda kugongesha kichwa kwenye barabara Shinyanga mjini, karibu na daraja la kuelekea Mwanza, alifariki palepale. Nilihudhuria maziko yake.

Mjini Mwanza, nililetewa taarifa kuwa mtoto wa shule amegongwa na pikipiki akiwa anavuka barabara, ikanilazimu kuhudhuria msiba kwa sababu mmoja wa ndugu wa marehemu ni mfanyakazi wetu.

Nimeyataja matukio haya kuonesha ukubwa wa tatizo lililopo. Mimi ni mmoja, nimeshuhudia haya, ni mangapi ambayo yanaendelea kutokea, ambayo sikupata kuyasikia?

Serikali imekuwa kama mzazi ambaye anaogopa kumpokonya mtoto mdogo anayechezea kisu kwa hofu kuwa akimpokonya atalia, huku akimweka mtoto wake kwenye hatari. Mzazi wa namna hiyo ni mjinga, mnafiki, na ni muuaji kwa kushindwa kutimiza wajibu wake kama mzazi.

Leo hii, waendesha pikipiki, hawafuati sheria yoyote ya barabarani.

Hawasimami kwenye taa inapotakiwa kusimama, hawasimami kwenye vivuko vya waenda kwa miguu hata kama watu wanavuka, wana-overtake upande wowote wanaoutaka, hawafuati speed limits, wanabeba mizigo hata isiyoendana na uwezo wa pikipiki (fikiria pikipiki inabeba mbao)! Hii ni nchi ya namna gani?

Ukiuliza ni kwa nini wameachwa hivi, Polisi wanasema kuwa Serikali imewazuia wasibughudhiwe, kwa kuwa waendesha pikipiki ni wengi, wataichukia Serikali, na kisha kuinyima CCM kura. Jambo la ajabu sana. Hivi kuwaachia hawa waende tu ovyo barabarani, hiyo Serikali haioni inawaweka kwenye hatari ya kifo waendesha pikipiki wenyewe, abiria wanaowabeba na waenda kwa miguu?

Serikali, ina maana ipo tayari wananchi waendelee kufa na wengine kuwa vilema, lakini wao wapate tu kura? Huu ni unafiki wa hali ya juu.

Nimeenda baadhi ya nchi, moja ya nchi ambazo nilivutiwa sana na uendeshaji pikipiki ni Burkina Faso. Pikipiki zinafuata sheria zote, kama yalivyo magari. Kwa nini hatupendi kuiga mambo mazuri kama hayo?

Kujifanya watu wema, kwa waendesha pikipiki wavunja sheria, hakuwasaidii wavunja sheria wenyewe, wala raia wengine wote kwa ujumla.

PENDEKEZO
1) Waendesha pikipiki wote (hasa za biashara), wapewe mafunzo kwa awamu kwa gharama ya Serikali. Akishamaliza mafunzo, apewa tag atakayoivaa shingoni. Abiria watahadharishwe kutopanda pikipiki ya waendeshaji wasio na tag.

2) Waendesha pikipiki za biashara wote, wapewe miezi 3, kila mmoja awe amehudhuria mafunzo na kupewa tag. Baada ya kipindi hicho kwisha, kusiruhusuwe mwendesha pikipiki asiye na mafunzo na tag, kuonekana na pikipiki barabarani.

3) Mwenye tag, akivunja sheria, anyang'anywe tag, azuiwe kuendesha, aende mafunzoni tena, kisha apewe tag nyingine.

Jukumu la msingi la Serikali yoyote Duniani ni usalama wa watu wake. Serikali ikishindwa kwenye hili, inakuwa haina uhalali wa kendelea kuwepo.

Nchini mwetu, siasa za unafiki, uwongo na hila, mara nyingi zimelididimiza na zinaendelea kuliangamiza Taifa letu, kila awamu yake, kwa viwango tofauti, kutegemeana na kiongozi mkuu wa nchi ni mtu wa namna gani.

Ni vema kwenye katiba mpya, iwekwe wazi katika kyzuia uongozi wa unafiki unaohatarisha usalama wa wananchi.
Hapo ulipouliza ' hii ni nchi ya aina gani?', ndio kila kitu!
Nahisi hii nchi inajiendesha yenyewe! Kila anayetajwa kuwa na dhamana fulani, kazi yake ni kupokea malipo halali na haramu, ila hatekelezi wajibu wowote wa hiyo dhamana. Na naanzia kwa rais!
 
Nyie mbona mnatusimanga sana sie bodaboda....yaani hivi vidogo mnashindwa kuvumilia lakini ufisadi mnavulimia. Wacha tunapambana life mzeya
Jaribu kidogo kuwa mtu mzima kijana ukipoteza mama yako au mwanao utasema hivyo?
 
Week kama tatu zilizopita kuna mfanyakazi wa bank moja aligongwa na pikipiki iliyokua imebeba mageti Kigamboni wakati anafanya mazoezi ya kukimbia akafariki hapo hapo.

Mwezi uliopita tuligonga pikipiki na gari ya ofisi ila uzembe ulikua wa pikipiki.

Nilimuuliza mtu kwamba, Je ni kweli mafuta ya pikipiki huwa yanawalewesha madereva wake? Maana madereva wa pikipiki za biashara wako kama kuna nati zimechomoka namna wanavyohatarisha maisha yao barabarani
 
Upungufu wa akili na unafiki wa DC kama huyo, ndio unaochangia maafa haya tunayoyashuhudia, yanasababisgwa na uendeshaji mbaya wa pikipiki.
Na uwezekano mkubwa huyo Dc ni shoga
 
Jf inanikasirisha sana .nilishawahi kuandika hanari yenye kichwa cha habari " pikipiki ni janga la taifa" nilishangaa umefutwa.

ila acha tukalalamikie twitter huku sasa wanatumia wenyewe JF modereter
 
Huku kwetu ndani ya wiki mbili wamefariki dereva wawili.. mmoja alikuwa ni mwanangu sanaa bado ni ngumu kuamini kama jamaa ndo hatorudi tena [emoji17]

Kweli Dunia tunapita..
Acha wafe hawa wahuni wanaendesha bodaboda kama vichaa japo wapo wanaojielewa pia
 
RIP kijana mdogo Anko Ally, boda mwaminifu sana wa IKULU
 
Back
Top Bottom