Rais Samia Walinde Watanzania Dhidi ya Mauaji ya Pikipiki

Rais Samia Walinde Watanzania Dhidi ya Mauaji ya Pikipiki

CCM na serikali wameshindwa kujenga viwanda na kufufua mashamba iliyoyaua ili vijana wakafanye kazi huko kwahiyo wameleta ajira mbadala ya bodaboda ambazo nyingine wanawapa vijana wakafilie mbali.
CCM wanajifanya kuwajali bodaboda sababu ya siasa tu, Hakuna utu wala Nia njema dhidi Yao ni unafiki tu.
 
Leo hii, japo pikipiki zimekuwa ni chombo kinachotegemewa na wengi kwa usafiri lakini kwa upande mwingine zimekuwa janga kwa Taifa. Hazijawa janga kwa Taifa kwa sababu zenyewe ni janga kwa asili yake bali kwa sababu ya unafiki wa Serikali.

Kuna wakati Polisi walitaka kudhibiti uendeshaji ovyo wa pikipiki lakini wanasiasa na viongozi wa Serikali wanafiki wakazuia zoezi hilo.

Kwa wakati tofauti, nimeshuhudia vifo vya watoto wawili, watu wazima watatu waenda kwa miguu, waebdesha pikipiki wawili na ulemavu wa mama mmoja, vyote vikiwa vimesababishwa na uendeshaji wa ovyo wa pikipiki.

Kifo cha kwanza kilikuwa cha mtoto wa shule wa kike mjini Singida. Nilitoka Dodoma, naelekea Mwanza, watoto walikuwa wametoka shule, nikawa naendesha gari taratibu kwaajili ya usalama wa watoto, lakini mbele yangu ilkuja pikipiki, uendeshaji wake ni kama wa mtu kichaa, kwa kasi ilipishana na gari langu, nilishangaa. Mara nilisikia kishindo kwa nyuma, nikatizama kwenye side mirror, mwendesha pikipiki akawa tayari amemgonga binti mdogo, wa darasa la 4. Niligeuza haraka gari, nikasaidiana na akina mama wawili walikuwa karibu, tukamkimbiza mtoto hospitali ya mkoa wa Singida. Simanzi ikiwa imenijaa, masikitiko yasiyoelezeka. Sikuondoka, nilitaka nijue maendeleo yake. Baadaye mama mzazi wa mtoto alifika. Baadaye nikaongea na daktari tena, naye akanihakikishia kuwa mtoto amepata fahamu anaendelea vizuri. Nikashusha pumzi nikaondoka. Lakini nilipenda sana nijue maendeleo ya yule mtoto, bahati mbaya sikuchukua mawasiliano ya mtu yeyote.

Wiki 2 baadaye nilipopita eneo lile, nilisimama kuulizia yule mtoto aliyegongwa na pikipiki alikuwa anaishi wapi. wakanionesha nyumba, lakini hawakuniambia kuwa alifariki. Kumbe haikuwa mbali na pale, nikaoneshwa, hatua kama 30 tu toka barabarani. Mama yake mzazi alikuwa ameketi nje. Nikamsalimia, nikamwuliza yule mama, mtoto anaendeleaje, ndipo akanikumbuka, mara akaanza kulia, akaniambia, "Baba, ulipoondoka, ilipita kama nusu saa tu, mtoto akafariki. Nilikuwa na mtoto huyo tu". Machozi yalinitoka, mpaka leo nikipita pale Singida, eneo lile, kumbukumbu mbaya ile haikosi kunijia.

Mwezi huo huo, siku moja nilimpigia rafiki wa siku nyingi, nilitaka nimpe kazi fulani, akanijibu kuwa yupo msibani Ifakara, kumzika Kaka yake aliyegongwa na pikipiki mjini Dar es Salaam.

Siku nyingine, nimetoka Dodoma, naelekea Kahama, nikawa nimekubaliana na jamaa mmoja, kuwa nipitie Tabora kwa mazungumzo ya kikazi. Nikiwa nimefika Itigi, akanipigia simu kuwa haitawezekana kukutana kwa sababu Dada yake amegongwa na pikipiki, amefariki Dunia.

Nikiwa Dar es Salaam, nilipigiwa simu na Admin Manager, kuwa mfanyakazi wetu mmoja, mama yake mzazi amegongwa na pikipiki hujo Njombe, amevunjika vibaya sehemu mbalimbali. Baadaye nilitumiwa picha za majeruhi, ni ngumu kuamini kuwa ni ajali ya pikipiki, mpaka leo hii, hajaweza kutembea, na hana fahamu kwa sababu ya damage ya kichwa.

Kazini tuliamua kuwapa mikopo wafanyakazi wetu. Baadhi waliamua kununua pikipiki. Naambiwa jioni wakitoka kazini waliamua kuzitumia pikipiki zao kubebea abiria. Mmoja aligonga nguzo ya umeme, alitaka kulipita gari kwa upande wa kushoto, gari aliyotaka kuipita ilikuwa inapishana na gari nyingine kwenye barabara za mtaani, akafariki palepale.

Mwingine alianguka baada ya kugonga pavement ya barabara, akafariki.

Mtu mmoja, kaka yake, mama mmoja niliyekuwa nafahamiana naye sana, akiwa amesimama pembeni ya barabara, aligongwa na pikipiki, naye kwenda kugongesha kichwa kwenye barabara Shinyanga mjini, karibu na daraja la kuelekea Mwanza, alifariki palepale. Nilihudhuria maziko yake.

Mjini Mwanza, nililetewa taarifa kuwa mtoto wa shule amegongwa na pikipiki akiwa anavuka barabara, ikanilazimu kuhudhuria msiba kwa sababu mmoja wa ndugu wa marehemu ni mfanyakazi wetu.

Nimeyataja matukio haya kuonesha ukubwa wa tatizo lililopo. Mimi ni mmoja, nimeshuhudia haya, ni mangapi ambayo yanaendelea kutokea, ambayo sikupata kuyasikia?

Serikali imekuwa kama mzazi ambaye anaogopa kumpokonya mtoto mdogo anayechezea kisu kwa hofu kuwa akimpokonya atalia, huku akimweka mtoto wake kwenye hatari. Mzazi wa namna hiyo ni mjinga, mnafiki, na ni muuaji kwa kushindwa kutimiza wajibu wake kama mzazi.

Leo hii, waendesha pikipiki, hawafuati sheria yoyote ya barabarani.

Hawasimami kwenye taa inapotakiwa kusimama, hawasimami kwenye vivuko vya waenda kwa miguu hata kama watu wanavuka, wana-overtake upande wowote wanaoutaka, hawafuati speed limits, wanabeba mizigo hata isiyoendana na uwezo wa pikipiki (fikiria pikipiki inabeba mbao)! Hii ni nchi ya namna gani?

Ukiuliza ni kwa nini wameachwa hivi, Polisi wanasema kuwa Serikali imewazuia wasibughudhiwe, kwa kuwa waendesha pikipiki ni wengi, wataichukia Serikali, na kisha kuinyima CCM kura. Jambo la ajabu sana. Hivi kuwaachia hawa waende tu ovyo barabarani, hiyo Serikali haioni inawaweka kwenye hatari ya kifo waendesha pikipiki wenyewe, abiria wanaowabeba na waenda kwa miguu?

Serikali, ina maana ipo tayari wananchi waendelee kufa na wengine kuwa vilema, lakini wao wapate tu kura? Huu ni unafiki wa hali ya juu.

Nimeenda baadhi ya nchi, moja ya nchi ambazo nilivutiwa sana na uendeshaji pikipiki ni Burkina Faso. Pikipiki zinafuata sheria zote, kama yalivyo magari. Kwa nini hatupendi kuiga mambo mazuri kama hayo?

Kujifanya watu wema, kwa waendesha pikipiki wavunja sheria, hakuwasaidii wavunja sheria wenyewe, wala raia wengine wote kwa ujumla.

PENDEKEZO
1) Waendesha pikipiki wote (hasa za biashara), wapewe mafunzo kwa awamu kwa gharama ya Serikali. Akishamaliza mafunzo, apewa tag atakayoivaa shingoni. Abiria watahadharishwe kutopanda pikipiki ya waendeshaji wasio na tag.

2) Waendesha pikipiki za biashara wote, wapewe miezi 3, kila mmoja awe amehudhuria mafunzo na kupewa tag. Baada ya kipindi hicho kwisha, kusiruhusuwe mwendesha pikipiki asiye na mafunzo na tag, kuonekana na pikipiki barabarani.

3) Mwenye tag, akivunja sheria, anyang'anywe tag, azuiwe kuendesha, aende mafunzoni tena, kisha apewe tag nyingine.

Jukumu la msingi la Serikali yoyote Duniani ni usalama wa watu wake. Serikali ikishindwa kwenye hili, inakuwa haina uhalali wa kendelea kuwepo.

Nchini mwetu, siasa za unafiki, uwongo na hila, mara nyingi zimelididimiza na zinaendelea kuliangamiza Taifa letu, kila awamu yake, kwa viwango tofauti, kutegemeana na kiongozi mkuu wa nchi ni mtu wa namna gani.

Ni vema kwenye katiba mpya, iwekwe wazi katika kyzuia uongozi wa unafiki unaohatarisha usalama wa wananchi
Great thinker
 
Ndugu HAMATAN,pamoja na kuandika Ujumbe mzuri lakini SIDHANI kama ilikuwa ni lazima uandike hali ya kiafya ya huyo Mama wa Singida kwamba AMEATHIRIKA!!!sijui ni Ujumbe gani uliokuwa unataka kuuleza hapa zaidi ya UNYANYAPAA!!!kwa hiyo unataka wakazi wote wa Singida na majirani wa huyo Mama sasa wajue kwamba ni MUATHIRIKA??wewe uliambiwa kwamba ni MUATHIRIKA,je ulimpima kupata uthibitisho huo??kutaja status ya Afya ya mtu ni zaidi ya UPUMBAVU
Samahani. Sikukusudia hilo. Nimeondoa bandiko. Nawe naomba uliondoe bandiko hili. Sorry for that.
 
CCM wanajifanya kuwajali bodaboda sababu ya siasa tu, Hakuna utu wala Nia njema dhidi Yao ni unafiki tu.
Nakubaliana nawe. Hata bodaboda wenyewe, wapo wanaokuwa vilema, na wapo wanaofariki. Na wengine hulazimika kuendesha ovyo kwa sababu inaonekana ndiyo mazingira waliyowekewa na Serikali. Huwezi kusema unampenda mtu, wakati imemwekea mazingira ya kuhatarisha maisha yake na ya watumiaji wengine wa barabara.
 
Abiria pia tunachangia ,unapandaje kwenye pikipiki bodaboda mwenye mvuta bangi ,au kanyoa kiduku,ukiangalia tu uso unajua huyu chapombe au bangi tupu na bado unapanda
Hapo unaongelea aliyepanda bodaboda, lakini fikiria mwenda kwa miguu, wala hajapanda bodaboda, lakini anaenda kugongwa na pikipiki, labda inaendeshwa na huyo mvuta bangi.
 
Nilikuwa na mpango wa kununua pikipiki niingie barabaran ila hizi takwimu za vifo zimenitisha, bodaboda yenyewe nimefundishwa mtaani tu
 
Hapo unaongelea aliyepanda bodaboda, lakini fikiria mwenda kwa miguu, wala hajapanda bodaboda, lakini anaenda kugongwa na pikipiki, labda inaendeshwa na huyo mvuta bangi.
Bodaboda hawafuati sheria za usalama barabarani.Wengi tukiandika ajali,za bodaboda ni nyingi,kuliko tunazozijua.NI HATARI TUPU,UWENDESHAJI WAO,NI WA KUTAHARISHA MAISHA YAO,NA YA WENGINE.
 
Mahojiano Kati ya DC mpumbavu na OCD.

DC mpumbavu-OCD kwanini mnakamata kila boda boda asiye na kofia mbili,kwani kila mwenye piki piki anabeba abiria!!! kama ana dharura tu!!!

OC asiyejiamini-aaaah mh tuna blah blah bla.

DC mpumbavu-kuanzia leo sitaki kuona mnakamata piki piki kisa helmet sawa OCD???

BODABODA-wanashangilia katika mkutano ule,woyoooooooooo
 
Hapo unaongelea aliyepanda bodaboda, lakini fikiria mwenda kwa miguu, wala hajapanda bodaboda, lakini anaenda kugongwa na pikipiki, labda inaendeshwa na huyo mvuta bangi.
mkuu kweli ni changamoto maana tuna bodaboda wa hovyo sana
 
Mahojiano Kati ya DC mpumbavu na OCD.

DC mpumbavu-OCD kwanini mnakamata kila boda boda asiye na kofia mbili,kwani kila mwenye piki piki anabeba abiria!!! kama ana dharura tu!!!

OC asiyejiamini-aaaah mh tuna blah blah bla.

DC mpumbavu-kuanzia leo sitaki kuona mnakamata piki piki kisa helmet sawa OCD???

BODABODA-wanashangilia katika mkutano ule,woyoooooooooo
Upungufu wa akili na unafiki wa DC kama huyo, ndio unaochangia maafa haya tunayoyashuhudia, yanasababisgwa na uendeshaji mbaya wa pikipiki.
 
CCM na serikali wameshindwa kujenga viwanda na kufufua mashamba iliyoyaua ili vijana wakafanye kazi huko kwahiyo wameleta ajira mbadala ya bodaboda ambazo nyingine wanawapa vijana wakafilie mbali.
Nasikia hapa dar kila wiki kuna bodaboda mia tatu 300 mpya za mkopo zinaingia barabarani, sijui kama wote hao wana leseni za udereva.
 
Tatizo sio waendesha boda tu hata wenye magari nao wanafanya makosa Tena makubwa tu.Ila wao siku zote ni wasomi Tena mno hasa linapotokea swala la ajali pili ni ni trafiki hasa wale wanaoongoza badala ya taa niliwahi kusimama upande wa taa ambao hautoki magari mengi bahati mbaya siku hiyo nilikuwa mwenyewe kwenye uelekeo wangu huwezi amini ilinichukua robo saa kusubiri trafiki aniruhusu kupita hiyo ni sawa kweli.(HATA MADEREVA WA MAGARI WA MCHONGO WAPO)
 
CCM na serikali wameshindwa kujenga viwanda na kufufua mashamba iliyoyaua ili vijana wakafanye kazi huko kwahiyo wameleta ajira mbadala ya bodaboda ambazo nyingine wanawapa vijana wakafilie mbali.
Hata magari yanaua mjomba sio pikipiki peke yake
 
Abiria pia tunachangia ,unapandaje kwenye pikipiki bodaboda mwenye mvuta bangi ,au kanyoa kiduku,ukiangalia tu uso unajua huyu chapombe au bangi tupu na bado unapanda
Kuna abiria ni wajinga sana,unamkuta kapanda bodaboda inayoendeshwa na dereva ambaye kwa muonekano wake tu,ni mvuta bangi,yaani kavaa hovyo,kanyoa hovyo na kwa saikolojia ya kawaida tu,unaona huyu dereva ni mapepemapepe,lakini mtu anapanda pikipiki.
Abiria nao wapewe elimu ya utambuzi,kwanza wajitambue wao wenyewe,pili watambue bodaboda wa hovyo ambao wanakimbizakimbiza pikipiki hovyo,na hawajihurumii.
Dereva boda unakuta anakimbiza pikipiki hadi unajiuliza,akiumia atamudu kweli gharama za matibabu au ndiyo ile kuwapatia ndugu pamoja na jamaa mzigo?
Mtu anakimbizakimbiza hovyo,ana ovrtake upande usioruhusiwa,huku kaweka earphones masikioni au kafungulia miziki ya singeli,hadi unamshangaa na aliyepanda kwenye pikipiki,kua hajitathmini au ni chizi mwenzake?Ujinga mtupu.
Mtu anaendesha hovyo,matokeo yake anapasuka kichwa au anaenda kupasuliwa kichwa hospitalini tena kwa msaada wa ndugu na jamaa.
 
Abiria nao vipi? Huwa nashangaa kuona abiria kapakizwa na kuendeshwa kama mzigo na yuko comfortable hadi anachat kwa simu? Huwa sipati jibu mwehu kati yao ni dereva au abiria?! Tena kama ndio umewwakosakosa kuwagonga abiria ndio wa kwanza kukumwagia matusi!
 
Back
Top Bottom