Rais Samia: Walichukulia ukimya na utulivu wangu Kama udhaifu

mshale21

JF-Expert Member
Apr 8, 2021
2,049
4,904
“Katika kipindi cha miezi sita cha urais wangu nilijaribu kuwa mkimya na kusoma wizara zote katika kipindi hicho nao walikuwa wakinisoma pia na kati yao wakachukulia ukimya na utulivu wangu kama udhaifu na wengine waliuchukulia kama njia ya kuonyesha uwezo wao,”

Samia.png
 
Sasa Rais anapoamua kutoa taarifa tu hadharani bila kutuambia ana mpango gani kudhibiti hali hiyo tumueleweje?
 
Hata hapa JF kuna watu wanachukulia upole na ukimya wake kama udhaifu na kusahau kabisa SSH ndio NAMBA MOJA na AMIRI JESHI MKUU

Tukiweza kutoa ushauri wetu bila kumdharau na bila kutumia huo ushauri kujikweza juu ya mamlaka ya Rais tutaweza kumsaidia Rais sana.

Ushauri sahihi uwe kwa nia njema na kwa maslahi mapana ya taifa. Tukitoa ushauri sahihi kwa nia mbaya na ikatokea huo ushauri umefanyiwa kazi tunaweza kuharibu sana mambo

Matusi, dharau, kejeli hazimzuii mama SSH kuwa rais ila zinawezasababisha hata kile tunachoongea au kufanya kisitiliwe maanani

Alitangulia kusema tusipandishe mabega juu
 
“Katika kipindi cha miezi sita cha urais wangu nilijaribu kuwa mkimya na kusoma wizara zote katika kipindi hicho nao walikuwa wakinisoma pia na kati yao wakachukulia ukimya na utulivu wangu kama udhaifu na wengine waliuchukulia kama njia ya kuonyesha uwezo wao,”
Chifu Hangaya kacharuka, naona karidhishwa na uchapakazi wa Mzee wa tozo! Kalemani na Dr. Ndugulile nadhani sasa wamemwelewa chifu!
 
Dikteta lihuaji lenye roho mbaya, huwezi kumfananisha na mama, mama ana hofu ya Mungu ya rohoni kabisa, lile lihuaji limejitia stress limeangamia,
Wewe hiyo hofu ya mungu ya mama uliipima kwa kigezo gani? Wewe uko moyoni mwake hadi ujue hiyo hofu yake iko moyoni?

Kufariki kila mtu atafariki. Hata asingekistress kama unavyosema bado angekufa.

Huyu mama hakuna kitu, ni bure kabisa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom