Rais Samia usiongee kwa kalamu, washtakie wananchi

Page 94

JF-Expert Member
Oct 22, 2015
5,205
15,162
Wasalaam!.

Kipindi Mheshimiwa Rais Samia Suluhu anaanza kupanga safu yake ya uongozi, alisisitiza sana watu wafanye kazi kwa bidii na kuheshimia. Zaidi, alihimiza kuwa yeye hatofoka hadharani kwa wale wote ambao wataenenda kinyume na maagizo yake au kinyume na maslahi ya umma. Yeye alichagua njia anayoiita 'kufoka kwa kalamu'. Akimaanisha kumuandikia mhusika aidha barua ya onyo ama ya kumuondoa kazini mara moja.

Ni njia nzuri sana, ila ambayo haina nguvu kwa desturi za nchi yetu. Haswa baada ya aliyekuwa Rais wa awamu ya tano, kujenga tabia ya kueleza madhaifu ya watendaji wote ambao anawaondoa.

Ukweli ni kuwa, pamoja na mengine mengi kilichomfanya Mh Magufuli apendwe sana na sehemu kubwa ya wananchi ni pamoja na kuwa muwazi wa kinachoendelea.

Lakini pia, njia ya kuweka wazi udhaifu ama ufisadi wa Watendaji wanaoondolewa kazini, ni kuwaamsha wengine kwamba macho yako yapo 'active' muda wote.

Njia hii pia itakusaidia kuonesha kwamba wewe si sehemu ya madudu yanayofanyika. Kuwaandikia na kisha mambo kumalizwa kimya kimya, kunafanya wananchi waendelee kuamini kwamba mkono wako pia unahusika.

Hivi majuzi, Mh Rai Samia Suluhu alianza kulalama kwamba kuna baadhi ya watu wanatengeneza maneno ya kuwaaminisha wananchi kwamba ufisadi unafanyika ndani ya awamu hii ya sita anayoiongoza.

Kwa namna moja ama nyingine, awamu hii anayoiongoza inaweza isiwe sehemu ya ufisadi huo. Lakini hao anaowatuhumu wameshamsoma. Yeye ni mtu wa kumaliza mambo kimya kimya. Wanatumia nafasi hiyo kueneza propaganda zao kwa jamii. Na kwa kiasi chake jamii inawaamini.

Wanasema njia ya mpumbavu ni kumpuuzia. Lakini hawa siyo wapumbavu, hawa ni watu werevu wanaojua wanachokitafuta. Wana agenda kubwa nyuma ya propaganda zao.

Njia ya kuwapunguzia nguvu ni kuwasemea kwa wananchi. Waambie ukweli, sema wazi. Jamii itakuelewa barabara. Kuendelea kukaa kwako kimya kunawapa fursa wao kuendelea kurusha makombora huku wakijidai kukaa mbali, kuwa hawahusiki.

Ongea na wananchi, ukitengua sema wazi aliyoyafanya. Hata usipofoka, lakini kwa ndimi yako ya upole na utaratibu sisi wananchi tutakuelewa.

Mungu akusaidie.
 
unapoteza nguvu zako bure !!

Hii nchi inahitaji kiongozi mpya mwenye nguvu na ushawishi ndo mamb yatanyooka


Tukubali ukweli mheshimiwa hana ushawishi tena kwa wadanganyikaa
 
Back
Top Bottom