Rais Samia uondoke ikifika mwaka 2025

Rais Samia uondoke ikifika mwaka 2025

Mikataba tafuta mwanasheria akae na wewe akupe shule kifungu kwa kifungu ili hii chuki yako ipungue.

Nchi imekuwa na marais sita na wawili wametoka visiwani wanne wametoka huku bara. Pengine ni mpango wa Mungu kwa Samia kuwa rais mwaka juzi baada ya kifo cha JPM.

Alitaka kutukumbusha maana pana ya demokrasia na sio huu ubinafsi wetu sisi watu wa huku bara, kujiona muda wote tuna haki kwa sababu ya ukubwa wa eneo letu.

Mungu anazo njia zake za kuongea na binadamu na zina ukuu usioelezeka. Hizi kelele zote ni chuki tu na zinaonyesha namna gani tusivyo na uvumilivu.

Yale yale Maneno ya Mwalimu Nyerere kwamba muungano ndio unaoshikilia uwepo wa TZ. Na tusijidanganye kudhani kuwa roho ya kibaguzi ya kumbagua Rais Samia, itaishia kwake tu, tutamnyooshea vidole rais wa Tanganyika kama leo tunavyomnyooshea SSH.
Mkuu, hapa ungemuweka MUNGU pembeni, ukabaki na binadamu tu. MUNGU ni mkamilifu na sidhani kama anahusika na lolote hapa. Siasa huwa ni mchezo mchafu sana ambao sidhsni kama MUNGU huwa anahudika nao. MUNGU atahusika tu endapo watatubu
 
MATHAYO 5:44:45.

lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi,

ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni; maana yeye huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki.
Mathayo 5:45
 
Kwa mambo yanayoendelea hasa mikataba ya ovyo iliyo ingiwa huu wa kuuza bandari zetu zote Kwa waarabu haikubaliki na hata mbuga zetu kiufupi hili jambo naomba kusema tu limekuondolea sifa kabisa ya kuwa mgombea wa 2025. Watanganyika wana hasira Kali na wewe.

Ukitaka watu warudishe imani kwako ni kuachana na hii mikataba na rudisha nchi kwenye misingi yake ya kulinda Mali zetu.

Mikataba mizuri ni ile yenye faida Kwa Taifa.
Kabisa watanzania tutakuwa wehu kama tutampitisha mama 2025.
 
Kwa mambo yanayoendelea hasa mikataba ya ovyo iliyo ingiwa huu wa kuuza bandari zetu zote Kwa waarabu haikubaliki na hata mbuga zetu kiufupi hili jambo naomba kusema tu limekuondolea sifa kabisa ya kuwa mgombea wa 2025. Watanganyika wana hasira Kali na wewe.

Ukitaka watu warudishe imani kwako ni kuachana na hii mikataba na rudisha nchi kwenye misingi yake ya kulinda Mali zetu.

Mikataba mizuri ni ile yenye faida Kwa Taifa.
Mama huyu ana nia njema, sema waliomzunguka ama wanamdanganya au wanamhujumu.
Ukiona mama huyu ameondoka 2025 watanzania msahau katiba mpya.
 
Kwa mambo yanayoendelea hasa mikataba ya ovyo iliyo ingiwa huu wa kuuza bandari zetu zote Kwa waarabu haikubaliki na hata mbuga zetu kiufupi hili jambo naomba kusema tu limekuondolea sifa kabisa ya kuwa mgombea wa 2025. Watanganyika wana hasira Kali na wewe.

Ukitaka watu warudishe imani kwako ni kuachana na hii mikataba na rudisha nchi kwenye misingi yake ya kulinda Mali zetu.

Mikataba mizuri ni ile yenye faida Kwa Taifa.

Kama ni kuondoka na huu uvamizi kwa nchi yetu Zanzibar uishe kwani hatujakusikia kusema chochote wakati mlipoivamia na kulazimisha nchi iingie kwenye mkataba hewa wa uvamizi mnaouita muungano na mnakuja kutuwa kila ufikapo uchaguzi hali ni hii na hatukusikii

Mikataba mizuri ni ile yenye faida Kwa Taifa.

03 Julai 2017​

Dodoma, Tanzania

Bunge lapitisha Miswada ya sheria za ulinzi wa Maliasili za Taifa​

HOTUBA YA WAZIRI WA SHERIA NA KATIKA MH. PROF. PALAMAGAMBA KABUDI

Hansard :
NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)
1
BUNGE LA TANZANIA
____________
MAJADILIANO YA BUNGE
___________
MKUTANO WA SABA
Kikao cha Hamsini na Nane – Tarehe 3 Julai, 2017
(Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi)
D U A
Naibu Spika (Mhe. Dkt. Tulia Ackson) Alisoma Dua
MWENYEKITI: Tukae, Katibu!
NDG. RAMADHANI ISSA ABDALLAH – KATIBU MEZANI:
HATI ZA KUWASILISHA MEZANI:
Hati zifuatazo ziliwasilishwa mezani na:-
WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA:
Maelezo ya Waziri wa Katiba na Sheria kuhusu
Muswada wa Sheria ya Mamlaka na Nchi kuhusiana na Umiliki
wa Maliasili wa Mwaka 2017 [The Natural Wealth and
Resources (Permanent Sovereignty) Bill, 2017]
Maelezo ya Waziri wa Katiba na Sheria kuhusu
Muswada wa Sheria ya Mapitio na Majadiliano kuhusu
masharti Hasi katika Mikataba ya Maliasili za Nchi wa mwaka
2017 (The Natural Wealth and Resources Contracts (Review
and Re-negotiation of Unconscionable Terms) Bill, 2017] ...

NDG. RAMADHAN ISSA ABDALLAH – KATIBU MEZANI:
MISWADA YA SHERIA YA SERIKALI
Muswada wa Sheria ya Mamlaka ya Nchi kuhusiana na
Umiliki wa Maliasili, 2017 (The Natural Wealth and
Resources (Permanent Sovereignty) Bill, 2017)
na
Muswada wa Sheria ya Mapitio na Majadiliano kuhusu
Masharti Hasi katika Mikataba ya Maliasili za Nchi, 2017
(The Natural Wealth and Resources Contracts (Review and
Re-negotiation of Unconscionable Terms) Bill, 2017)
(Kusomwa Mara ya Pili)
WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: Mheshimiwa Naibu
Spika, kwa mujibu wa Kanuni ya 86 ya Kanuni za Kudumu za
Bunge, Toleo la Mwaka 2016, naomba kutoa hoja kwamba
Muswada wa Sheria ya Mamlaka ya Nchi kuhusiana na Umiliki
wa Maliasili wa 2017 (The Natural Wealth and Resources
(Permanent Sovereignty) Bill, 2017) na Muswada wa Sheria ya
Mapitio na Majadiliano kuhusu Masharti Hasi katika Mikataba
inayohusu Maliasili za Nchi, 2017 (The Natural Wealth and
Resources Contracts (Review and Re-negotiation of
Unconscionable Terms) Bill, 2017) sasa usomwe kwa mara ya
pili na Bunge lako Tukufu lijadili na hatimaye lipitishe Miswada
hii na kuwa sehemu ya sheria za nchi.
Mheshimiwa Naibu Spika, kabla ya kuwasilisha
maudhui ya Miswada hii, naomba nianze kwa kumshukuru
Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema kwa kuturuzuku uhai,
kutujalia afya na kutuwezesha kutekeleza majukumu yetu.
Mheshimiwa Naibu Spika, nachukua fursa hii pia
kumshukuru Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli,
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa imani kubwa
aliyoonesha kwangu kwa kuniteua kuwa Mbunge na Waziri
wa Katiba na Sheria. (Makofi)...

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya maelezo hayo
ya utangulizi, naomba sasa kutoa maelezo kuhusu Muswada
wa Sheria ya Mamlaka ya Nchi kuhusiana na Umiliki wa
Maliasili wa Mwaka 2017 (The Natural Wealth and Resources
(Permanent Sovereignty) Bill, 2017) na Muswada wa Sheria ya
Mapitio na Majadiliano kuhusu Masharti Hasi katika Mikataba
inayohusu Maliasili za Nchi, 2017 (The Natural Wealth and
Resources Contracts (Review and Re-negotiation of
Unconscionable Terms) Bill, 2017).
Mheshimiwa Naibu Spika, misingi ya Katiba ya Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania; Muswada wa Sheria ya Mamlaka
ya Nchi kuhusiana na Umiliki wa Maliasili wa 2017
unapendekeza kuweka masharti yanayohusianisha misingi
iliyomo katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
1977, mikataba na misingi ya sheria mbalimbali za Kimataifa
ambazo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inazitambua
na ama imesaini au kuridhia.
Mheshimiwa Naibu Spika, sheria inayopendekezwa
kupitia Muswada huu ina msingi wake katika Ibara ya 8(1) ya
Katiba ambayo inaweka masharti kuwa Tanzania ni nchi
inayozingatia msingi wa demokrasia na haki ya kijamii na
kwa msingi huo, wananchi wake ndio msingi wa mamlaka
yote ya nchi na Serikali inawajibika kwa wananchi wake.
Ibara hiyo inaeleza kama ifuatavyo:-
“Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni nchi
inayofuata misingi ya demokrasia na haki ya kijamii na kwa
hiyo: –
(a) wananchi ndio msingi wa mamlaka yote na
Serikali itapata madaraka na mamlaka yake yote kutoka kwa
wananchi kwa mujibu wa Katiba hii;
(b) lengo kuu la Serikali litakuwa ni ustawi wa
wananchi;
(c) Serikali itawajibika kwa wananchi;
(d) Wananchi watashiriki katika shughuli za Serikali
yao kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii.” Mwisho wa
kunukuu.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa ujumla, Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania ikiwa ni nchi yenye uhuru kamili ina
haki na mamlaka ya kusimamia maliasili na utajiri wake. Kwa
msingi huo, Serikali inayo wajibu wa kulinda maslahi ya
wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika
mikataba inayoingia kuhusiana na maliasili na utajiri huo
kama inavyoelekezwa katika Ibara ya 27 ya Katiba ya Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania. Ibara hiyo inaeleza kama
ifuatavyo:-
“(1) Kila mtu ana wajibu wa kulinda mali asilia ya
Jamhuri ya Muungano, mali ya Mamlaka ya Nchi na mali
yote inayomilikiwa kwa pamoja na wananchi, na pia
kuiheshimu mali ya mtu mwingine.
(2) Watu wote watatakiwa na sheria kutunza vizuri mali
ya Mamlaka ya Nchi na ya pamoja, kupiga vita aina zote za
uharibifu na ubadhirifu, na kuendesha uchumi wa Taifa kwa
makini kama watu ambao ndio waamuzi wa hali ya baadaye
ya Taifa lao.”
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuzingatia misingi hiyo
iliyowekwa na Katiba, Ibara ya 9(1)(c) ya Katiba inaelekeza
kuwa shughuli za Serikali zitekelezwe kwa njia ambazo
zitahakikisha kwamba utajiri wa Taifa unaendelezwa,
unahifadhiwa na unatumiwa kwa manufaa ya wananchi
wote kwa ujumla na pia kuzuia mtu kumnyonya mtu
mwingine.
Mheshimiwa Naibu Spika, misingi ya maazimio ya
Umoja wa Mataifa; Muswada huu unazingatia uwepo wa
Sheria ya Kimataifa inayotambua haki ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kuhusiana na umiliki wa maliasili.
Aidha, Muswada umezingatia kwamba Tanzania imesaini na
kuridhia mikataba mbalimbali ya Kimataifa ikiwemo Azimio
la Umoja wa Mataifa Namba 523(vi) la tarehe 12 Januari, ..
 
Kwa mambo yanayoendelea hasa mikataba ya ovyo iliyo ingiwa huu wa kuuza bandari zetu zote Kwa waarabu haikubaliki na hata mbuga zetu kiufupi hili jambo naomba kusema tu limekuondolea sifa kabisa ya kuwa mgombea wa 2025. Watanganyika wana hasira Kali na wewe.

Ukitaka watu warudishe imani kwako ni kuachana na hii mikataba na rudisha nchi kwenye misingi yake ya kulinda Mali zetu.

Mikataba mizuri ni ile yenye faida Kwa Taifa.
Sidhani kama atakuelewa, maana hapo ni sawa nakuuacha mzinga wa nyuki wenye asali wakati nyuki wanapiga kelele tu hata hawaumi.
Nasikia kuna tumiswaada lukuki tunapelekwa kwa wapiga meza watubariki, kakiwemo wajuba kutoka nje (wageni) kumiliki ardhi kiroho safi yaani fuedha yako tu.
 
Kwa mambo yanayoendelea hasa mikataba ya ovyo iliyo ingiwa huu wa kuuza bandari zetu zote Kwa waarabu haikubaliki na hata mbuga zetu kiufupi hili jambo naomba kusema tu limekuondolea sifa kabisa ya kuwa mgombea wa 2025. Watanganyika wana hasira Kali na wewe.

Ukitaka watu warudishe imani kwako ni kuachana na hii mikataba na rudisha nchi kwenye misingi yake ya kulinda Mali zetu.

Mikataba mizuri ni ile yenye faida Kwa Taifa.
Hadi 2025 si atakuwa amewapa Waarabu kila kitu?
Asimalize mwaka huu aondoke tu
 
Back
Top Bottom