Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 4,783
- 14,975
Rais Samia akiwaapisha viongozi wateule Ikulu Mei 24, 2024
Maagizo kwa Lazaro Jacob Twange Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO)
"Nimekupeleka kwenye Shirika ambalo ni security ya nchi yetu na hii ni baada ya mchujo mkubwa kuangalia loyality, uwajibikaji, uzoefu na mambo yote umeibuka kwamba unaweza kushika Shirika hili"
"Shirika hili kama nilivyokwambia ni security ya nchi kwasababu Umeme ndani ya nchi yetu ndio kila kitu, chukulia mfano umeme uzimwe sio maeneo ya uchumi, maeneo ya wananchi tu, wakose umeme siku mbili, siku tatu kelele ya kisiasa itakayopigwa hapo lakini sasa chukulia upande wa pili wa maeneo ya uchumi, umeme ukikosekana ina maana uchumi wa nchi unakwenda kuzorota"
"Tumefanya jitihada kubwa kama Serikali ya kuweka uzalishaji wa umeme kwenye vyanzo kadhaa, tunachazo kikubwa Julius Nyerere Hydropower Project (JNHPP) na ile ndio roho yetu kama nchi pamoja na kwamba asilimia 60 hadi sasa...tuseme imeshuka sasa baada ya JNHPP kuzalisha lakini huko nyuma ilikuwa asilimia 60 sasa tuseme labda asilimia 40 ya umeme wote wa nchi hii umatokana na gesi kwahiyo asilimia 60 utatokana sasa na vyanzo vingine baada ya JNHPP kuanza kazi"
"Tuna umeme wakutosha, Chalinze pale tunaingiza umeme wakutosha tatizo tulilonalo ni uambukizaji kwenda kupeleka Kaskazini na nyanda za juu kusini magharibi mwa nchi, miradi hiyo ipo lakini kulikuwa na kusuasua kukubwa kwa kuanza kwa miradi hiyo kaangalie na uhakikishe uambukizaji unafanyika"
"Tunaongezeko la uwekezaji ndani ya nchini, wote hawa Viwanda vinataka umeme na si kupata umeme lakini wa kuaminika, wahakikishe umeme saa zote upo wanazalisha wanavyotaka, kiwango wanachokitaka ili waweze kufanya uzalishaji na kukuza uchumi wetu, kwahiyo una kazi kubwa ndugu yangu"
"Ndani ya nchi yetu Mungu ametubariki Uranium kwa muda mrefu sana tuliaminishwa kwamba kutengeneza umeme wa Uranium ni hatari lakini nchi zinazoendelea wanatumia na ndio chazno kikubwa cha umeme wao, sisi tuna low material hapa ndani wanatuambia hatari ili wachote wapeleke kwao wakatengeneze umeme kwao, sasa pamoja na wizara ni vyema kusimamia mradi wetu ule wa Uranium kule Tunduru kwamba sasa wale wawekezaji waanze kazi na tufaidike na rasilimali ile nchini na kama wanataka kuchukua nje wachukue lakini kwanza tufaidike ndani ya nchi nategemea kuna matani mengi tu (makadirio ya sasa hivi kama tani 58,500 za uranium zimelala pale) huu mradi uende na tuanze"
"Umeme wa Nyukilia kama wao wanautumia, tunaweza kuutumia na tukawa na umeme wakutosha nchini lakini na kuuza nchi jirani kama tunavyotaka kuuza sasa kwa Zambia lakini nasi tunanunua kutoka Ethiopia. Sasa tukijitosheleza hatutakwenda kununua"
Rais Samia Suluhu Hassan, akiapisha viongozi wateule wa Tume ya Maadili, amewataka kusimamia maadili kwa watumishi wa umma kwa nguvu na uadilifu.
"Sisi viongozi ni watu na wanadamu, kuna miiko tumewekewa. Ukitufanyia tathmini leo unaweza ukatukuta asilimia 30 tu kweli tunafuata hiyo miiko ya uongozi. Sasa mna kazi ya kutulea huko. Ujazaji fomu na kuwaleteeni hiyo tunafanya sana, lakini matendo mengine yetu binafsi huko ni mambo mengine. Kwa hiyo naomba mkasimamie maadili kwenye Utumishi wa Umma, tumeharibika."
"Leo hii mtumishi wa umma anakosa uzalendo. Mtumishi wa umma anathubutu kuchukua siri kwenye mafaili, akapiga picha kwenye simu yake na akasambaza akijua kwamba anamkomoa Rais, lakini kumbe ni yeye amekosa maadili, ni yeye hawajibiki kwa taifa lake."
Ameongeza kuwa, "Jitu lishapotoka huko nje, unaliteua, unaliweka, linakwenda na imani yake ile ile badala ya kutumikia nchi."