Rais Samia, ulitaka kutuhutubia au kuzungumza nasi?

Aisee pole sana. Hiyo ndo inaitwa kutumika kisiasa... Imeishia hiyooo
 
Ukilalamika mitandaoni, toa suluhisho…. ila ukweli leo TUMEPIGWA.
 
Yaani nyie vijana nilifikiri mnaenda kuzungumza na Rais... afadhali hata wazee wa Dar walipata nafasi ya kutoa ya moyoni.... hotuba za viongozi na wabunge ziliwapotezea nafasi adhimu.... poleni sana.
Kwa ccm kiongozi kuhutubia watu huwa wanaita ni kuongea na watu.
 

Ule ni usanii kama usanii mwingine. Na kama kweli ile ndio namna ya kiongozi kuongea na watu ili kujua matatizo yao, basi ni njia ya kijima kweli kweli.
 
Kwa ccm kiongozi kuhutubia watu huwa wanaita ni kuongea na watu.
Mkuu 'tindo',
Huyu mama alidhani huu mtindo wa kukutana na makundi mbalimbali kutampambanua katika uongozi wake.

Kwa bahati mbaya, hakujiandaa vyema kuitumia hii mikutano kwa lolote; si mlejesho wala lengo maalum analolenga kufanikisha kupitia kwenye mikutano hii.

Mimi simlaumu, huenda amejifunza na ataanza kuitumia kwa malengo maalum anayotaka kuyafikia. Vinginevyo matokeo yake yatakuwa ni kama ulalamishi tunaouona hapa.
 
Vijana ndio hao kina polepole ?

Kaka acha tu, Kikwete alivyokuwa anagombea urais kwa mara ya kwanza alikuwa na miaka 54, wakati ule alikuwa anasifiwa kuwa ni bonge la kijana! Hivyo usishangae kumsikia Polepole akijisifia ni kijana mdogo sana.
 

Ninachokiona kwa huyo mama, ni kama ameamua kuiga style ya Magufuli kwenye kile kinachoitwa kukutana na makundi ya wananchi na kujua kero zao. Nadhani wale washauri Magufuli ndio bado wanamshauri na yeye, hivyo wanampa mbinu za kusaka umaarufu, na sio kutatua matatizo ya watu kwa mantiki ya kutatua. Hivi ni kweli rais hajui matatizo ya vijana mpaka akakutane nao hapo aishie kuwahutubia na wala sio hata mjadala?
 
Alijua sana yale mliyotaka kuongea that's why hakuona sababu ya kutembeza mic kwa vijana wote 50.
Wewe binafsi, una jambo gani jipya kwa mfano?
Kwahiyo wewe unamsemea Mama leo sio!?
Yani umeisoma mind yake!?
 
Hama nchi
Huu ni ujinga wa hali ya juu sana ... Na utaendelea kuwagharimu..
Yani vile wewe ni TAGA ....!! unajitoa akili kabisa.

Lakini msije sema hatukuwakumbusha.

Mamlaka ni za Mungu...aliye juu.. The Almighty GOD.
 
KUDEMKA ni hulka yake huyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…