Rais Samia, ulitaka kutuhutubia au kuzungumza nasi?

Binafsi nlijiandaa sana kuja kuongea na Mh. Rais nimweleze changamoto na masuluhisho kadhaa kwa baadhi ya changamoto tulizo nazo vijana mitaani.

Achana na mawaziri hawa wahajui changamoto zetu sababu hawajavaa viatu vyetu. Mimi sikuja na chama chochote. Nlikuja na hoja na naona ntaondoka nazo kama nlivyokuja nazo.

Nliamini tunakuja zungumza na Rais wetu. Kumbe tunakuja elezewa mambo kadhaa na watu kadhaa
Hivi wewe unaakili kweli? Kama kila mtu aliyekuwepo pale amgetaka kuongea na Rais wangetumia siku ngapi kukamilisha ndio maana kukawekwa wawakilishi wetu. Kwa akili hizi ndio maana hatujielewi tunataka nini.
 
Mmevishwa mabarakoa mtafikiri mpo wodini. Wenzenu wanasubiri bil za IMF so mligeuzwa maenyesho kuwa vijan mnazingatia barakoa.
 
Hivi wewe unaakili kweli? Kama kila mtu aliyekuwepo pale amgetaka kuongea na Rais wangetumia siku ngapi kukamilisha ndio maana kukawekwa wawakilishi wetu. Kwa akili hizi ndio maana hatujielewi tunataka nini.
We kilaza sijui hata kama unaelewa unachoandika. Hujielewi unataka nini na unadhani wote hawajielewi kama wewe kilaza.
 
Kaka acha tu, Kikwete alivyokuwa anagombea urais kwa mara ya kwanza alikuwa na miaka 54, wakati ule alikuwa anasifiwa kuwa ni bonge la kijana! Hivyo usishangae kumsikia Polepole akijisifia ni kijana mdogo sana.
Kwenye siasa uyo Ni kijana mdogo sana.ila mtaani ameshazeeka
 
Kaka acha tu, Kikwete alivyokuwa anagombea urais kwa mara ya kwanza alikuwa na miaka 54, wakati ule alikuwa anasifiwa kuwa ni bonge la kijana! Hivyo usishangae kumsikia Polepole akijisifia ni kijana mdogo sana.
Ukiwapanga kikwete na polepole halafu ukaita mtoto wa darasa la tatu akuonyeshe mbabu ni nani na kijana ni nani? Bila kupepesa macho yule mtoto, babu atamsonta polepole na kijana atampoint kikwete.
 
Mlipopewa Nafasi Mlishindwa hata Kujenga Hoja...Hamjui mnachotaka hovyo kabisa....Mkaishia Kusema miradi sasa inawahusu nini ile miradi...

Mazingira Ya kazi Mfano hamsemi kama ni biashara hizi Namna gani mnaweza kuziboresha ili mkue..na mnataka serikali iwasaidie Nini??

kilimo Ni kipi mnataka eneo hilo na serikali iwasidie nini?? pembejeo za mkopo?? masoko au mikopo ya Mitambo ili muongeze thamani??

Kwenye eneo la mifugo mnataka nn??
yaani hamjui lolote sasa mnamlamu mama wa watu bure. Mnatakiwa Kujua serikali haikuwekei utajiri mezani uchukue lazima utoe jasho tena jasho la damu...Nyie endeleeni kulemaa...

mnatakiwa kubadilika....
 
Nimeisikilizaa kwa nadhifu saana hotuba ya mheshimiwa Raisi.! Sio kuongea na Vijana kwa ujumla.
Yaani alichoandikiwa na kukiskma kwa kadamnasi ni namba nyiingi kulaghai kuwa serikali inakuja na Miradi na fursa tele!
Utashangaa watu wanapiga makofi na nyimbo kwa wingi! Hakuna hata 1 aliyejliza swali na akajibiwa.
Porojo.na siasa zimebakia.
 
Ule ni usanii kama usanii mwingine. Na kama kweli ile ndio namna ya kiongozi kuongea na watu ili kujua matatizo yao, basi ni njia ya kijima kweli kweli.
Ujima na usanii si aliondoka nao dhalimu wako na sasa tuko vizuri au?
 
Lazima ufahamu kuwa mahali popote viongozi wa CCM wakitia timu mambo yameharibika!
Mambo yaliharibika pale tulipoigawanya Tanzania kuwa ya vyama vya siasa na CCM kujimilikisha nchi hii.Ukisikia Rais anataka kuongea na wazee wa Dar,wanaenda wanaccm,ukisikia ataongea na kinamama wa Tanzania wanaenda UWT,vijana nao wakiitwa utawakuta UVCCM wamejazana nasi tunaridhika,ilhali huo ni ubaguzi wa wazi wazi na wakienda hushangilia na kuchezeshwa singeli badala ya kujenga hoja za kitaifa. Unakuta tunanadiwa Ilani ya Uchaguzi ya chama nasi tumeridhika.Shame on us!
Kila Mara sisi tunaodai agenda za kitaifa kama Katiba,Tume huru ya Uchaguzi, Mahakama huru na Bunge huru tunaambiwa ni wapinzani,mawakala wa mabeberu Ama wapiga dili nasi tunakubali/tunalazimishwa kukubaliana na CCM & Serikali yake.
Nchi hii bila Katiba ya sasa(ya CCM 1977) kubadilika na kujitengenezea Katiba yenye kutupatia dira,Sera na agenda za kitaifa basi tufahamu kuwa kusonga mbele ni ngumu sana.Watu wenye mawazo ya kibinafsi kama CCM hawawezi kututoa kwenye mkwamo huu walioutengeneza kwa miaka nenda rudi tokea Uhuru hadi sasa,tusitegemee maendeleo ya watu.Shame on us.
Eti Katiba siyo kipaumbele Chao?!
 
Back
Top Bottom