Rais Samia Suluhu Hassan, naomba kwa heshima na taadhima nikukumbushe tu kiapo ulichokula siku ile ya Ijumaa tarehe 19/3/2021!

Mag3

Platinum Member
May 31, 2008
13,064
22,757

Mimi Samia Suluhu Hassan naapa kwamba nitakuwa mwaminifu kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuitumikia kwa moyo wangu wote na kwamba nitaihifadhi, nitailinda na kuitetea Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mujibu wa sheria iliyowekwa.

Eeh Mwenyezi Mungu nisaidie.
 
Heheeeee, miradi ya ajabu ifufuliwe? Kuala ni kutudanganya tu maana sisi wabongo ni wapimbafu. Nchi imeanza kuliwa Kama enzi za kikwete. Wako si kukutumikia bali kujaza matumbo yao.
 
They are all crooks! Bagamoyo bandari oyeeee, hapo wameishapokea mabillioni. Masheik na maaskofu wangewapiga marufuku wanasiasa kuingia misikitini au kanisani- hao ni wezi na murderers - wanaiba hela za elimu, afya etc etc
 
Haya nimerudi na nazidi kukukumbusha Mh. Rais Samia Suluhu Hassan kuwa jukumu lako la kwanza kama Jemadari Mkuu wa taifa ni kuihifadhi, kuilinda na kuitetea Katiba ya Jamhuri ya Muungano Tanzania.

Hili jukumu haliepukiki kwa namna yoyote ile, kwa sababu zozote zile na kwa madhumuni yoyote yale na vyombo vyote vya kukusaidia kuihifadhi, kuilinda na kuitetea unavyo na ulipewa na Katiba hiyo hiyo.

Katiba ndio msingi, ilani na dira ya taifa baada ya sisi Wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuamua rasmi na kwa dhati kujenga katika nchi yetu jamii inayozingatia misingi ya uhuru, haki, udugu na amani.

Nadhani Mh. Rais Samia Suluhu Hassan unajua fika kuwa bila matakwa ya Katiba hungeweza kukanyaga milango ya Ikulu na tupo tusioogopa mabadiliko na tulipambana kuhakikisha hilo takwa la Katiba linaheshimiwa.

Mh. Rais, waogope sana waoga wa mabadiliko...hawa kwa uroho wao wa madaraka walikuwa tayari kuisigina Katiba katika harakati zao za kulinda maslahi yao binafsi wakiwa na wasiwasi na uongozi wako.

Lakini leo hii wanafiki hao hao, baada ya wewe kuapishwa, wanajaribu kukushawishi uvunje Katiba eti kwa kisingizio cha uchumi kwanza...yale yale ya mtangulizi wako ambaye naye alitoa kisingizio cha maendeleo kwanza.

Kama alivyowahi kuonya baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, aliyeonja nyama ya mtu haachi. Leo ni kauli tu ya kupiga marufuku uhuru, kesho unakamata, kesho kutwa unatesa na mwisho unapoteza...

Mh. Rais nakuomba usikubali, watu kama hao hawakutakii mema, kaa mbali nao na waogope kama ukoma la sivyo itabidi utumie mbinu zile zile...

Nitaendelea...
 
Mimi naona hamna haja ya kuapishwa kuwa Rais Tanzania. Kwasababu haina mantiki yeyote.
 
Mimi Samia Suluhu Hassan naapa kwamba nitakuwa mwaminifu kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuitumikia kwa moyo wangu wote na kwamba nitaihifadhi, nitailinda na kuitetea Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mujibu wa sheria iliyowekwa.

Eeh Mwenyezi Mungu nisaidie.
Mkuu Mag3 , kwanza naunga mkono hoja, kuwakumbusha viongozi wetu kuhusu viapo vyao, ni jambo jema!.

Ila kiapo ulichokiweka kwa maandishi ni kiapo kimoja, wakati kile alichotamka, japo kinaitwa ni kiapo as if ni kimoja, ila pale ameapa viapo 3!. Ni vizuri ungeviweka kwa maandishi, vyote vitatu, ili tuvitumie kukuonyeshea, yote Mama Samia anayoyasema na kuyatenda ni kwa mujibu wa katiba!.
P.
 
Mh. Rais Samia Suluhu Hassan kuwa jukumu lako la kwanza kama Jemadari Mkuu wa taifa ni kuihifadhi, kuilinda na kuitetea Katiba ya Jamhuri ya Muungano Tanzania.

Hili jukumu haliepukiki kwa namna yoyote ile, kwa sababu zozote zile na kwa madhumuni yoyote yale na vyombo vyote vya kukusaidia kuihifadhi, kuilinda na kuitetea unavyo na ulipewa na Katiba hiyo hiyo.

Katiba ndio msingi, ilani na dira ya taifa baada ya sisi Wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuamua rasmi na kwa dhati kujenga katika nchi yetu jamii inayozingatia misingi ya uhuru, haki, udugu na amani
Mkuu Mag3 , naendelea kukuunga mkono, yote usemayo hapa ni kweli, ni hiki ndicho Mama Samia, anachokifanya, ameapa kuihifadhi, kuilinda na kuitetea Katiba ya Jamhuri ya Muungano Tanzania ya mwaka 1977, anailinda, kuitetea na kuihifadhi katiba ya JMT ya mwaka 1977, ila kwenye kuteleza haya, pia anazingatia Sheria, Taratibu, na Kanuni na miongozo ya mtangulizi wake, kama alivunja katiba, na hakufanywa lolote, Mama Samia kaipokea nchi yenye katiba iliyoshavunjwa, anaendelea nayo hivyo hivyo hadi atakapukuwa tayari kuitengeneza ikatengamaa!.

Mama Samia ni dereva wa gari letu, gari lilikuwa kwenye mwendo kasi wa kupaisha uchumi wa nchi, dereva aliyetangulia aliliburuza kwa mwendo mdundo, na kukanyaga na kufukia mashimo ya katiba, na kupitiliza baadhi ya vituo bila kusimama, moja ya vituo alivyo vipitiliza ni kituo cha katiba mpya kwenye ilani iliyopita kwa hoja ya "katiba sio, kipaumbele changu", kituo hicho kimepitilizwa. Gari yetu imeishapitiliza kituo hicho, na kwenye mwelekeo wa ilani hii ya Samia, gari yetu haijapangiwa kupitia kituo hicho!.

Maadam yeye amepokea, gari iliyoshapitiliza kituo hicho, na route ya kupita tena njia hiyo, haijapangwa, dereva wetu kaamua kuendelea na safari ya kujenga uchumi, tukiisha fika salama, ndipo route ijayo, tutaipanga kupitia njia hiyo ya katiba mpya, hivyo abiria wa kituo cha katiba mpya waliopitilizwa kituo cha katiba mpya, kama walipopitilizwa na dereva yule, hawakupiga kelele kuwa walipitilizwa, kumpigia kelele dereva aliyepokea usukani, sio kumtendea haki!.

Mwache dereva Mama Samia aendelee kuendesha gari letu, safari iendelee, safari ijayo, gari letu litapangiwa tena upya route ya kituo cha katiba mpya na huko tutafika!.
P
 
Hakuna mtihani mzito kwa viongozi wetu Kama kulinda katiba, wakishaapa tu wanaanza kukanyaga viapo vyao, au wanachagua vipengele vya kufuata...Mfano hai Ni kitendo Cha rais wetu mpendwa kukataza mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa...
 
naapa kwamba nitakuwa mwaminifu kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuitumikia kwa moyo wangu wote na kwamba nitaihifadhi, nitailinda na kuitetea Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mujibu wa sheria iliyowekwa.

Eeh Mwenyezi Mungu nisaidie.
Mh. Rais Samia Suluhu Hassan, kwa ukumbusho zaidi ni kuwa misingi ya Katiba yetu itabaki imara iwapo tu mambo haya yatazingatiwa...
  1. Uwepo wa demokrasia ambayo serikali yake inasimamiwa na Bunge lenye wajumbe waliopatikana kupitia uchaguzi huru na linalowawakilisha wananchi.
  2. Uwepo wa Mahakama huru zinazotekeleza wajibu wa kutoa haki bila woga wala upendeleo wowote.
Mh. Rais kiapo ulichokula ni pamoja na kuwa mtumishi mwaminifu mkuu wa Watanzania wote bila kuwabagua.

Bila kuathiri sheria za nchi...

Kila mtu anastahili kuwa huru na kukutana na watu wengine kwa hiari yake na kwa amani, kuchanganyika na kushirikiana na watu wengine, kutoa mawazo hadharani, na hasa zaidi kuanzisha au kujiunga na vyama au mashirika yaliyoanzishwa kwa madhumuni ya kuhifadhi au kuendeleza imani au maslahi yake au maslahi mengineyo.

Ni marufuku kwa mtu kuteswa, kuadhibiwa kinyama au kupewa adhabu zinazomtweza au kumdhalilisha

Kila raia anayo haki na uhuru wa kushiriki kwa ukamilifu katika kufikia uamuzi juu ya mambo yanayomhusu yeye, maisha yake au yanayolihusu Taifa

Kila mtu yuko huru kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake, na kutafuta, kupokea na kutoa habari na dhana zozote kupitia chombo chochote bila ya kujali mipaka ya nchi, na pia ana uhuru wa mawasiliano yake kutoingiliwa kati.

Kila raia anayo haki ya kupewa taarifa wakati wote kuhusu matukio mbalimbali nchini na duniani kote ambayo ni muhimu kwa maisha na shughuli za wananchi, na pia juu ya masuala muhimu kwa jamii.
 
Mapungufu ya Mama Samia, hayawezi kulinganishwa na unyama wa Maguful. Bado Nina Imani kubwa na Mama tumor nafasi.
 
Hii nchi inaviongozi wa upinzani hawajui kuishi kwa nyakati zilizomo. Mfano hili sekeseke la upinzani na mama asilimia kubwa ya wananchi bado wana imani na mama sio kwamba hawahitaji katiba mpya! Ila wanaona ajenda ya katiba mpya wanasiasa wa wanaipigia chapuo kwa maslahi ya Chadema (Vyama vya upinzani) zaidi kuliko ajenda nyingine.

By then tulikua pamoja sababu adui yetu alikua Jiwe Ila sasa msilazimishe ajenda zenu zicompromise harakati zetu za maisha zilizokua shuttered kipindi cha Jiwe. Push your agendas slowly hata sisi tuna agendas zetu za maendeleo tunampush mama atekeleze tufike. Hizi katiba mpya za kukurupuka tutakosa wote.
 
Hii nchi inaviongozi wa upinzani hawajui kuishi kwa nyakati zilizomo. Mfano hili sekeseke la upinzani na mama asilimia kubwa ya wananchi bado wana imani na mama sio kwamba hawahitaji katiba mpya!
Unajuaje kuwa aliyeanzisha hii thread ni kiongozi wa upinzani? Mimi sikujiunga CCM toka kipindi cha mfumo wa chama kimoja na hadi sasa sijajiunga na chama chochote cha kisiasa hapa nchini.

Mimi ni mwananchi tu anayeamini kwamba adui nambari moja wa taifa hili ni CCM kwani ndicho chama pekee kimekuwa madarakani toka kianzishwe.
Ila wanaona ajenda ya katiba mpya wanasiasa wa wanaipigia chapuo kwa maslahi ya Chadema (Vyama vya upinzani) zaidi kuliko ajenda nyingine.
Umekurupuka ndugu yangu...kwenye hii thread inayoongelewa ni yeye kushindwa kuheshimu kiapo chake cha kuihifadhi, kuilinda na kuitetea Katiba kama ilivyo kwa sasa.

Kwa kuzuia shughuli za kisiasa Mh. Rais kavunja Katiba na hiyo ndiyo ajenda kuu ya thread hii...anakumbushwa kiapo chake. Pamoja na hilo Katiba ni ya Tanzania si ya Chadema wala CCM na haitegemei hisani ya Rais.
By then tulikua pamoja sababu adui yetu alikua Jiwe Ila sasa msilazimishe ajenda zenu zicompromise harakati zetu za maisha zilizokua shuttered kipindi cha Jiwe. Push your agendas slowly hata sisi tuna agendas zetu za maendeleo tunampush mama atekeleze tufike. Hizi katiba mpya za kukurupuka tutakosa wote.
Mimi siogopi mabadiliko na ndio maana baada ya kifo cha dhalimu mwendazake niliunga mkono kuheshimiwa kwa Katiba Mh. Samia aweze kutwaa madaraka!

Ghafla baada ya kuapishwa ni kama vile naye ameamua kuisigina Katiba hiyo hiyo iliyomwezesha kutwaa hayo madaraka kwa kupingana nayo. Huo ndio ugomvi wetu na mama, period!
 
Hivi viapo vina nguvu sana katika ulimwengu wa kiroho..ni maagano!! Yana madhara makubwa sana kwa mwanadamu kama akiyakiuka.
 
Mkuu Mag3 , naendelea kukuunga mkono, yote usemayo hapa ni kweli, ni hiki ndicho Mama Samia, anachokifanya, ameapa kuihifadhi, kuilinda na kuitetea Katiba ya Jamhuri ya Muungano Tanzania ya mwaka 1977, anailinda, kuitetea na kuihifadhi katiba ya JMT ya mwaka 1977, ila kwenye kuteleza haya, pia anazingatia Sheria, Taratibu, na Kanuni na miongozo ya mtangulizi wake, kama alivunja katiba, na hakufanywa lolote, Mama Samia kaipokea nchi yenye katiba iliyoshavunjwa, anaendelea nayo hivyo hivyo hadi atakapukuwa tayari kuitengeneza ikatengamaa!.

Mama Samia ni dereva wa gari letu, gari lilikuwa kwenye mwendo kasi wa kupaisha uchumi wa nchi, dereva aliyetangulia aliliburuza kwa mwendo mdundo, na kukanyaga na kufukia mashimo ya katiba, na kupitiliza baadhi ya vituo bila kusimama, moja ya vituo alivyo vipitiliza ni kituo cha katiba mpya kwenye ilani iliyopita kwa hoja ya "katiba sio, kipaumbele changu", kituo hicho kimepitilizwa. Gari yetu imeishapitiliza kituo hicho, na kwenye mwelekeo wa ilani hii ya Samia, gari yetu haijapangiwa kupitia kituo hicho!.

Maadam yeye amepokea, gari iliyoshapitiliza kituo hicho, na route ya kupita tena njia hiyo, haijapangwa, dereva wetu kaamua kuendelea na safari ya kujenga uchumi, tukiisha fika salama, ndipo route ijayo, tutaipanga kupitia njia hiyo ya katiba mpya, hivyo abiria wa kituo cha katiba mpya waliopitilizwa kituo cha katiba mpya, kama walipopitilizwa na dereva yule, hawakupiga kelele kuwa walipitilizwa, kumpigia kelele dereva aliyepokea usukani, sio kumtendea haki!.

Mwache dereva Mama Samia aendelee kuendesha gari letu, safari iendelee, safari ijayo, gari letu litapangiwa tena upya route ya kituo cha katiba mpya na huko tutafika!.
P
P Kati ya watu ambao nikiona andiko lenye jina lako lazima nilisome ni wewe P ila hapa kidogo, mfano wako bado siungi mkono hoja yako ya dereva wa gari la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ina maana mama hata akikuta barbara imefungwa au kunashimo aendelee tu asirudi nyuma?
 
Mkuu Mag3 , naendelea kukuunga mkono, yote usemayo hapa ni kweli, ni hiki ndicho Mama Samia, anachokifanya, ameapa kuihifadhi, kuilinda na kuitetea Katiba ya Jamhuri ya Muungano Tanzania ya mwaka 1977, anailinda, kuitetea na kuihifadhi katiba ya JMT ya mwaka 1977, ila kwenye kuteleza haya, pia anazingatia Sheria, Taratibu, na Kanuni na miongozo ya mtangulizi wake, kama alivunja katiba, na hakufanywa lolote, Mama Samia kaipokea nchi yenye katiba iliyoshavunjwa, anaendelea nayo hivyo hivyo hadi atakapukuwa tayari kuitengeneza ikatengamaa!.

Mama Samia ni dereva wa gari letu, gari lilikuwa kwenye mwendo kasi wa kupaisha uchumi wa nchi, dereva aliyetangulia aliliburuza kwa mwendo mdundo, na kukanyaga na kufukia mashimo ya katiba, na kupitiliza baadhi ya vituo bila kusimama, moja ya vituo alivyo vipitiliza ni kituo cha katiba mpya kwenye ilani iliyopita kwa hoja ya "katiba sio, kipaumbele changu", kituo hicho kimepitilizwa. Gari yetu imeishapitiliza kituo hicho, na kwenye mwelekeo wa ilani hii ya Samia, gari yetu haijapangiwa kupitia kituo hicho!.

Maadam yeye amepokea, gari iliyoshapitiliza kituo hicho, na route ya kupita tena njia hiyo, haijapangwa, dereva wetu kaamua kuendelea na safari ya kujenga uchumi, tukiisha fika salama, ndipo route ijayo, tutaipanga kupitia njia hiyo ya katiba mpya, hivyo abiria wa kituo cha katiba mpya waliopitilizwa kituo cha katiba mpya, kama walipopitilizwa na dereva yule, hawakupiga kelele kuwa walipitilizwa, kumpigia kelele dereva aliyepokea usukani, sio kumtendea haki!.

Mwache dereva Mama Samia aendelee kuendesha gari letu, safari iendelee, safari ijayo, gari letu litapangiwa tena upya route ya kituo cha katiba mpya na huko tutafika!.
P
Je kuna popote katika mada yangu nimeongelea Katiba mpya? Mimi nimemtaka tu mama aheshimu kiapo chake cha kuihifadhi, kuilinda na kuitetea Katiba, period.

Ziko thread nyingi zinazoongelea madai ya Katiba mpya na mimi naziunga mkono lakini katika hii thread namkumbusha tu Mh. Rais umuhimu wa kuheshimu kiapo chake.
 
Kwani kuna nini hapo bandari ya Bagamoyo mbona watu wanaisakama sana? Nadhani kama kuna jambo linatakiwa kuwekwa sawa liwekwe bandari ijengwe.

Nampenda sn mama Samia, Mungu mbariki Samia
 
Back
Top Bottom