Rais Samia Suluhu Hassan amemteua, Shaaban Kisu kuwa Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais-Ikulu

Rais Samia Suluhu Hassan amemteua, Shaaban Kisu kuwa Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais-Ikulu

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
3,177
Reaction score
7,472
Screenshot 2025-05-07 140603.jpg

Rais Samia Suluhu Hassan amemteua, Shaaban Kisu kuwa Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais-Ikulu.

Taarifa imetolewa leo Mei 7,2025 na Katibu Mkuu Kiongozi,Moses Kusiluka katika hafla ya waandishi wa habari wateule kwenye Tuzo za Samia Kalamu Awards,zilizokabidhiwa Mei 5,2025.

Chanzo: Nipashe
 
Hongera yake,msimsahau mwanasheria mzoefu huyu si mwingine Pascal Mayalla!
 
Si tunaambiana kila siku nchi ina uhaba wa ajira?hata huyo mkuu wa nchi anajua na kuna wakati akizungumza huwa analikiri hilo?

Shaban Kisu tangu nazaliwa napata akili 80s huko sasa nakaribia mvi bado tu anahitajika kwenye ajira?kwanini wasipewe nafasi damu changa wakaonyesha nao wana nini?
 
Sasa unampa damu changa asie na taarifa nyeti za nchi then iweje?
Kuna sehem zinahitaji uzoefu fulani.
 
Sasa unampa damu changa asie na taarifa nyeti za nchi then iweje?
Kuna sehem zinahitaji uzoefu fulani.
Hakuna kitu kama hicho,mkurugenzi mawasiliano ya raisi hajawa wa muhimu kiasi kwamba inabidi ajue mambo fulani fulani ya taifa America tu hapo wakati wa babu Biden walimpa mwanamke tena aged 41.

Siku akiteuliwa CDF au IGP mdogo kiumri ndiyo tutaingia shaka siyo hao sijui watu wa habari wapishi na wafagizi.
 
Hichi cheo kipo kikatiba? au ni kama cha naibu waziri mkuu, kwenye katiba hakipo
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, amemteua Bw. Shaaban Kissu kuwa Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu.

Taarifa ya uteuzi huo imetolewa leo, Jumatano, Mei 7, 2025, na Katibu wa Rais, Bw. Waziri Salum, wakati wa hafla ya chakula cha mchana iliyowakutanisha Rais Samia na wanahabari walioshiriki katika tuzo za Samia Kalamu Awards.
Bw. Kissu, ambaye awali alikuwa Mkurugenzi wa Africa Media Group, alipokea taarifa ya uteuzi huo akiwa mshereheshaji wa hafla hiyo. Katibu wa Rais alisema uteuzi huo umetangazwa rasmi leo na hata Kissu mwenyewe hakuwa na taarifa kabla ya kutangazwa kwake.

“Hii taarifa nafikiri ni ‘surprise’ hata kwa Kissu mwenyewe, kwa sababu hakuwa na taarifa. Hata mmeona nimechelewa kufika hapa – tulikuwa tunashughulikia masuala hayo,” alisema Waziri Salum, akimwakilisha Rais Samia katika hafla hiyo.

Uteuzi huu unatajwa kuwa sehemu ya juhudi za kuimarisha mfumo wa mawasiliano Ikulu, sambamba na kuleta uzoefu mpya katika kusimamia mahusiano kati ya taasisi ya Urais na vyombo vya habari.
 
Mshehereshaji wa shughuli za kitaifa, juzi tu alikuwa kwenye mei mosi, jana kwenye tuzo za kalamu, sasa itabidi aibuke mc mwingine wa kitaifa
 
Back
Top Bottom