#COVID19 Rais Samia pamoja na juhudi zake zote bado anayokazi kubwa ya kufuta mawazo hasi juu ya chanjo ya korona iliypandikizwa na Hayati Magufuli

SOPINTO

Senior Member
Oct 19, 2020
155
385
Ugonjwa wa Korona uliibuka ktk serikali ya awamu ya tano na katika jitihada za kupambana nao , ikajengeka imani kuwa ni ugonjwa uliotengezwa katika maabara kwa dhumuni maalum hususani katika nchi za Afrika. Baada ya muda katika kupambana na ugonjwa huo nchi mbalimbali zikajitangaza kupatikana kwa dawa na chanjo ya ugonjwa huo , lakini aliekuwa mkuu wa nchi kwa wakati huo aliwaaminisha wananchi kuwa hizi chanjo sio salama kabisa kwa maisha ya binadamu na kwasababu ilikuwa kauli ya mkuu wa nchi basi ikaiingia vizuri sana katika akili za watanzania.

Mbaya zaidi taasisi za dini pamoja na taasisi za afya nazo zikakubaliana kwa asilimia 100 kuwa chanjo sio salama kabisa hivyo wananchi watumie dawa za kienyeji na sio chanjo . Hivi sasa mkuu wa nchi yupo katika kampeni juu ya kuwapatia wananchi wake chanjo japo kwa hiyari lakini changamoto kubwa iliyopo ni je; watanzania wapo tayari kwa kiasi kupokea chanjo hiyo? tukumbuke tu kuwa lengo la WHO ni kuwapatia chanjo wananchi wote , je Rais Samia na wananchi watatimiza lengo hilo ili misaada iendelee kumiminika nchini?

Changamoto nyingine ni chanjo gani ndio bora? Je, chanjo kutoka Uchina, Urusi, USA, UK, Canada ambayo itatumiwa na WHO na Je, Watanzania wanaamini chanjo kutoka nchi gani?

Hivi karibuni Waziri mkuu wa Uingereza aliugua ugonjwa wa Korona na mpaka sasa yupo Karantini japokuwa alipata chanjo mara mbili.

USHAURI KWA WIZARA YA AFYA

Wizara ya Afya ifanye kampeni kubwa ( massive kampeni) usiku na mchana ili kuondoa fikra hasi zilizozagaa katika mawazo ya watu.

Kazi iendeleee.
 
Hayo majinga na mazuzu ambayo yanashika fikra za Magufyuli kuwa corana hakuna, sijui na chanjo ni hatari, wao wasichanjwe tu, hakuna wakuwafosi, waachwe hili wamfuate huyo mungu wao huko kuzimu,

Sisi ambao tunajitambua tupo pamoja na dunia inavyotaka na pia tupo pamoja na Rais, tutapigwa chanjo Kama kawaida, hayo mazuzu yaendelee na fikra za mungu wao, wao wanadhani TANZANIA ni kisiwa
 
Hayo majinga na mazuzu ambayo yanashika fikra za Magufyuli kuwa corana hakuna,sijui na chanjo ni hatari, wao wasichanjwe tu,hakuna wakuwafosi, waachwe hili wamfuate huyo mungu wao huko kuzimu...
Ni kweli lakini chanjo ya korona ni ngumu kuikwepa labda usisafiri katika siku zako zote za maisha , mana ukitaka kutoka nje ya nchi lazima uoneshe kazi ya chanjo...
 
Tukiacha na mambo mengine aliyoyafanya Jiwe , ugonjwa wa Corona ni propaganda , Hilo liko wazi hata huhitaji akili ya form four kulielewa, Maghufuli alikosa smartness ya kukabiliana nalo akaja kichwa kichwa mwisho wakamwondoa ....!!!
Aliidharau Corona huyo mungu wenu, mwishoe ikamuondoa, mi binafsi mzazi wangu ilimpata Corona,Ni hatari, uisikie tu kwa mtu,kila siku ile kuekewa mtungi wa oxgen tulikuwa tunalipia elfu themanini, alilazwa kwa wiki tatu, alikuwa anapumua kwa tabu, iyo ward aliyokuwa kalazwa kila siku wanakufa watu kwa changamoto hiyo,

Nyie endeleeni kufuata fikra za dikteta,mtapukutika wote
 
Jaribu na wewe kupandikiza imani tuone. Mimi habari za chanjo ya corona nilishakataa, mliotumwa kutushawishi mnapoteza muda wenu tu.
Mi namshauri mama kuhusu covid awe anapiga vitaarifa kimtindo tu asikomae kivileeee.
 
Aliidharau Corona huyo mungu wenu,,mwishoe ikamuondoa,,.mi binafsi mzazi wangu ilimpata Corona,Ni hatari, uisikie tu kwa mtu,kila siku ile kuekewa mtungi wa oxgen tulikuwa tunalipia elfu themanini, alilazwa kwa wiki tatu, alikuwa anapumua kwa tabu, iyo ward aliyokuwa kalazwa kila siku wanakufa watu kwa changamoto hiyo,

Nyie endeleeni kufuata fikra za dikteta,mtapukutika wote
Hujui lolote...!!! Uwe unachimba vitu kabla ya kuvianika kwenye majukwaa yenye watu ambao inavyoonekana most of them wanakuzidi upeo wa akili
 
Aliidharau Corona huyo mungu wenu,,mwishoe ikamuondoa,,.mi binafsi mzazi wangu ilimpata Corona,Ni hatari, uisikie tu kwa mtu,kila siku ile kuekewa mtungi wa oxgen tulikuwa tunalipia elfu themanini, alilazwa kwa wiki tatu, alikuwa anapumua kwa tabu, iyo ward aliyokuwa kalazwa kila siku wanakufa watu kwa changamoto hiyo,

Nyie endeleeni kufuata fikra za dikteta,mtapukutika wote
Kila siku walikuwa wanakufa? kwanini baba yako hakufa.
 
Aliidharau Corona huyo mungu wenu,,mwishoe ikamuondoa,,.mi binafsi mzazi wangu ilimpata Corona,Ni hatari, uisikie tu kwa mtu,kila siku ile kuekewa mtungi wa oxgen tulikuwa tunalipia elfu themanini, alilazwa kwa wiki tatu, alikuwa anapumua kwa tabu, iyo ward aliyokuwa kalazwa kila siku wanakufa watu kwa changamoto hiyo,

Nyie endeleeni kufuata fikra za dikteta,mtapukutika wote
Kwani wanaodungwa hiyo michanjo hamfi?

Simple nyie jifungueni wengine tuacheni. Kila mtu afanye lake, mmejaa viherehere kuliko hata shetani
 
Ni kweli lakini chanjo ya korona ni ngumu kuikwepa labda usisafiri katika siku zako zote za maisha , mana ukitaka kutoka nje ya nchi lazima uoneshe kazi ya chanjo...

Kama unajiandaa kwa paper, nenda kaendelee kuchimbua.

Magufuli hakubahatisha kuhusiana na hii ishu ya Corona

Aliweka wazi juu ya mashaka yake kuhusu huu ugonjwa kwamba kwann chanjo yake igunduliwe haraka haraka ilhali kuna magonjwa mengne ya viruses kama HIV/AIDS, Malaria nk yanayoisumbua dunia na tafiti zake juu ya chanjo hayajapatikana mpaka sasa

Na ukweli juu ya mashaka haya unadhihirika hivi sasa, ambapo Waziri Mkuu Uingereza kapigwa chanjo na bado siku chache zilizopita kakutwa na maambukizi ya Corona

Magufuli was right
 
Kwani wanaodungwa hiyo michanjo hamfi?!
Simple nyie jifungueni wengine tuacheni. Kila mtu afanye lake, mmejaa viherehere kuliko hata shetani
Watu wajinga wanafarijiana. They are full of hates kuliko hata maarifa muhimu.
Leohii ikitokea Samia akabadili mtazamo kwa kuangalia namna watu wanavyodhurika na bila usalama wowote dhidi ya virus, utawaona tena wanapongeza. Ujinga ni adui mkubwa kuliko maradhi wala umaskini.

Sikuwahi kukubaliana na Magufuli kwenye kila Jambo ILA kwenye chanjo.....
Nasema hivi SITACHANJWA
 
Rais alishasema mbona chanjo ni hiari.

Hisia hasi zimetoka wapi tena..kumbe mnakiri jpm alikuwa strong kiushawishi kwa kiwango cha ajabu hata mpaka inawashangaza.

sasa kama jpm alikuwa na uwezo wa kushawishi raia wake kwa kiwango hicho je angeshindwaje kuwashawishi raia haohao kumpa kura za kishindo?

Umekiri pia kiongozi mkubwa wa uingereza ameripotiwa kuugua korona licha ya kudungwa chanjo ya korona awali

Huon basi jpm alikuwa sahihi ku-raise doubt na chanjo za korona
 
Kachanje tu ndugu. Hiyari yako. Kila mtu ana akili ya kujua cha kuchagua. Usijione una akili sana kuliko wanaozikataa. Wana akili timamu na akili zao zimewaelekeza hivyo. Waache!

Wewe ukishachanja si unakuwa na kinga? Waache wasiochanja wapukutike ili wajifunze. Kumbuka gonjwa hatari halihitaji kampeni. Kwa kipindi chote hiki bila shaka Watanzania wameshajua hili gonjwa ni hatari kiasi gani!
 
Kachanje tu ndugu. Hiyari yako. Kila mtu ana akili ya kujua cha kuchagua. Usijione una akili sana kuliko wanaozikataa. Wana akili timamu na akili zao zimewaelekeza hivyo. Waache...
Nyie endeleeni kumuenzi Magufuli msichanjwe, ,muanze kufa Kama kuku wa mdondo
 
Tukiacha na mambo mengine aliyoyafanya Jiwe , ugonjwa wa Corona ni propaganda , Hilo liko wazi hata huhitaji akili ya form four kulielewa, Maghufuli alikosa smartness ya kukabiliana nalo akaja kichwa kichwa mwisho wakamwondoa ....!!!
 
Rais alishasema mbona chanjo ni hiari.

Hisia hasi zimetoka wapi tena..kumbe mnakiri jpm alikuwa strong kiushawishi kwa kiwango cha ajabu hata mpaka inawashangaza...
Nathubutu kusema lileta mada ni rimbumbumbu kwerikweri (am sorry mleta mada), yaani anaanzisha mada alafu hapohapo anatoa mfano wenye kukinzana na mada yake
 
Back
Top Bottom