Tatizo lililopo Mwanza nadhani lipo kwenye miji yote, maana hata huku Arusha ni hivyohivyo.
Sasa je tunadhani tatizo ni la Wananchi au Wenye Mamlaka?.
Usipojipa muda wa kutafakari unaweza kudhani ya kuwa Mwendazake aliharibu sana kwa kuruhusu hili...lakini hebu tu jiulize ukiwa na biashara yako utakaa tu mahali kusubiri Wateja au utawafuata walipo?.
Serikali inaajiri Watu inaoamini ni Wataalamu wa kupanga miji, hivi kazi yao sio kuangalia ni namna gani watapanga hiyo Miji ikawatumikia Wananchi wa hali zote?. Hatuna Watu wanaoweza kufikiri nje ya boksi ndio maana siku zote hukimbilia njia za mkato za kutatua matatizo...ikiwemo hiyo ya kufukuza au kuondoa Watu.
Wataalamu wafanye utafiti waone ni nini kinapelekea idadi kubwa ya Watu kwenye eneo fulani tofauti na kwingine, hivyo kama wanaweza kupata namna ya kubadilisha maeneo ya mikusanyiko/mapito ya Watu basi wala hakuna nguvu itahitajika kuwahamisha au kuwaondoa....wataondoka wenyewe maana hayo mambo ni automatic.