GE2025 Rais Samia: Oktoba 29 Tokeni kapigeni kura hakuna jambo baya litatokea

GE2025 Rais Samia: Oktoba 29 Tokeni kapigeni kura hakuna jambo baya litatokea

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
1,446
Reaction score
2,093
Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Samia Suluhu Hassan akizungumza na wananchi kwenye Mkutano wa Kampeni leo Septemba 18, 2025 katika Jimbo la Nungwi, visiwani Zanzibar amesema kuwa nchi yetu Tanzania ipo vizuri kwenye masuala ya Ulinzi na Usalama na kuwataka wananchi kuondoa hofu na kujitokeza Oktoba 29, 2025 kwenda kupiga kura kwani vyombo vya usalama na ulinzi vimejipanga vizuri

"Nchi yetu ipo vizuri kwenye masuala ya ulinzi na usalama, na jana kule kusini niliwatoa hofu wananchi nikawaambia vyombo vyetu vimejipanga vizuri msiwe na wasiwasi 29 Oktoba ikifika tokeni kapigeni kura hakuna jambo baya litatokea" amesema Mgombea Urais CCM, Samia Suluhu Hassan

 
Back
Top Bottom