Rais Samia na viatu vya Hayati Dkt. Magufuli

NKWENYE

Member
Feb 19, 2017
55
177
Habari ndugu zangu, poleni na makali ya tozo.

Niende kwenye mada moja kwa moja, baada ya kuondoka mpendwa wetu JPM kwa hakika moja ya swali zito lililokuwa liko kwa waombolezaji wote ni kuwa, je, Nani atavaa VIATU VYA baba na vimuenee?

Kwa kuwa Mungu ndiye mpangaji basi ikampendeza Mungu kuwa mama ndiye atakae vaa hivi VIATU kwa namna yoyote ile ! Mimi sikuwaza mtu was kuvivaa VIATU ila niliwaza namna gani mvaaji atavitumia ktk matembezi yake ya kila siku.

Baba alizoea kupiga teke mawe na watu walifurahi sn, baba alizoea kukanyaga watu akiwa kwenye mechi na washabiki wa timu yake walishangilia sn, baba alikuwa anatembea na VIATU kipindi cha tope Kali na alikuwa hajali km vitabanduka soli au la! Watu wake walijipiga kifua kuwa wanalo dume la shoka! Baba aliwaweka watu tayari kuwa kila mechi anayopangwa Ni lazima timu ishinde bila kujali wametimia au hawajatimia.

Kwa bahati mbaya mashabiki wa baba waliaminishwa kuwa yeye ni muumini wa wachezaji wa baadhi ya kanda, na alionesha wazi wazi kwa kuwasajili kwenye timu na kuwatumia Mara kwa Mara.

Nini ninachotaka kusema, mama ana mitego mingi sn na anahitaji washauri sahihi ili airuke, moja ya eneo ambalo baba amempiga gepu kubwa Ni uwezo was kutatua migogoro ya papo kwa papo hasa akiwa ziarani. Kwa mfumo wa kiutawala wa nchi yetu Kuna muda rais Ni mtatuzi wa lazima wa Mambo.

Kwa mfano, mama alikuwa kwenye mchakato wake wa kurecord vivutio vya utalii, akapata bahati ya kuhitimisha kongamano la utamaduni mkoa wa Mwanza, akakusanya machief wote nchi nzima, watu wa mikoa jirani walikuja, kwa kawaida rais Ni overall kwa siyo rahisi upate umati wote ule uliojitokeza mwanza alafu usiseme chochote kinachowahusu! Mama alipomaliza kusimikwa u-chief akawasha gari akasepa. Hakuna kiongozi yeyote iliyeruhusiwa kusema japo hata kero kidogo! Hakuna lolote linalohusu mwananchi wa kawaida lilogusiwa.

Kibaya zaidi hata aliposimamishwa BUZURUGA na IGOMA hakuwa na tone ya rais! Mimi sikuwa muumini mkubwa wa j.p.m lakini nilitarajia kuona anaemfuata kwenye utawala atakuwa na kazi rahisi zaidi kwa kuwa ATAKUWA AMEJUA NYUMBA INAVUJA WAPI (wa-tz wanapenda nn na hawapendi kipi, wapi mwenzie alitumia VIATU vyake vibaya ili na yy asitumie hayo.)

Kwa wale ambao tunafuatilia siasa na tamaduni za tz. Kuna baadhi ya kanda nchi hii haziamini kuwa mwanamke anaweza kuwa kiongozi bora hata km huyo mwanamke atafanya vizuri, na moja ya kanda hiyo ni kanda ya ziwa! Ambayo pia mzee baba alikuwa anapendeka zaidi.

Ukizungumza nao wanakwambia huyu hamna kila kitu! Hawamini Kuna kitu mama atafanya! Kibaya zaidi hii tabia inaenda kuota mizizi Hadi kwa viongozi wenzie na mama.

Ushauri wangu, mama tafuta matumizi sahihi ya VIATU VYA baba hasa katika utatuzi wa kero katika ngazi ya CHINI, pia angalia usitumie VIATU VYA mzee kwenye maeneo aliyoonekana kuwa kero hasa suala la ku-deal na upinzani kibabe.tatu usimwamini mtanzania, jiridhishe na Mambo unayoambiwa kwa kuruhusu maoni huru ya wa-tz na kwa kutumia intelijensia binafsi. Vinginevyo Kuna maeneo kura utazipata kwa kutumia bunduki!

NKWENYE,

Mwananchi wa kawaida
 
Back
Top Bottom