Rais Samia na ndoto baada ya 2025

F-Merylin

Senior Member
Dec 26, 2016
128
177
Kwanza hakuamini (kwa unyofu wa moyo wake na upendo kwa kiongozi wake) kuwa mtangulizi wake hayupo tena na yeye sasa ana wajibu sio tu wa kutangaza msiba wake bali pia kuchukua nafasi yake. Hayakuwa maigizo alipochelewa kutoa taarifa ya msiba wala maigizo akiwa na macho mazito akiapa kuwa Rais March 19. Alionyesha alivyomthamini mtangulizi wake na alimtendea haki kwa kuongoza maomboleza ya heshima kubwa kwake.

Lakini kabla hata msiba haujaisha akichagizwa na wanasiasa wachambuzi kama akina Zitto, ukweli wa mambo ulifika akilini mwake Rais kuwa yeye sasa ni Rais. Kwa kuanzia akiwa Dodoma akatangaza mbela ya kadamnasi iliyojaa waheshimiwa kutoka kusini na kasikazini kuwa yeye ni Rais. Hakuishia hapo akawaambia wana CCM waliojinyima nafasi ya kugombea urais mwaka 2020 ili kumpa yeye na Magaufuli nafasi ya kugombea bila upinzani kuwa waache ndoto za urais za mwaka 2025. Kauli hii iliwashangaza wengi kwa vile ilikuwa mapema mno watu kuanza kufikiria kampeni za urais. Kumbe Mama Samia ni mtu wa maono kuliko tunavyodhani. Sio tu anapanga safu ya uongozi ya "kazi iendelee" bali anafikiria tayari 2025 na kuweka mazingira yatakayomsaidia kuondoa vikwazo vyote muda ukifika.

Mbali na kuzuia kampeni za chinichini kafanya yafuatayo:
1. Mawaziri maarufu waliokuwa karibu na JPM (ambao bila shaka walikuwa na ndoto za 2025) amewapiga lungu kwa kushusha status yao na kupewa wizara za kawaida (siitaji kuwataja wanafahamika). Amebaki Majaliwa na macho yatakuwa kwake kuona hatima yake chini ya Samia.

2. Ndani ya CCM alikuwa na uwezo wote wa kumbakisha Polepole na kumrudisha Bashiru. Hakufanya hivyo amehakikisha watu hawa wenye mlengo wa kushoto na ushawishi tayari katika chama kawaondoa katika maamzi ya juu ya chama. Itakuwa pia ajabu kama Mzee Mangula ataendelea na wadhifa wake baada ya 2022.

3. Sasa kuna pangua pangua ya viongozi ngazi zote. Ieleweke Samia na Majaliwa ndio waliounda inner party ya uongozi wa Magufuli. Viongozi wanaobadilishwa walipatikana kwa ushauri wa hao wawili. Lakini pia kuhamishahamisha ni gharama kubwa sana. Sasa julize kwa nini afanye hivyo wakati "Kazi Iendelee" inaishia 2025? Bila shaka anaandaa safu yake ya uongozi itakayomrahisishia mambo 2025. Na wapambe wake wameishaanza kusema anafaa mpaka 2030! Ukweli ni kuwa akitaka anaweza kuwa Rais mpaka 2035! Watu wanaogopa kusema hili lakini kifo cha Magufuli kinaweza kutupa Rais "Nkulunzinza" wa Tanzania. Aliyedai awamu ya kwanza aliipata bila uchaguzi. Na katiba iko kimya kuhusu hili.

Je, Mama Samia yuko sahihi kuwa na ndoto baada ya 2025? Hilo ni swali gumu kwa vile kuna faida na hasara zake. Akitaka kufanya hivyo awe makini sana kwa kila uamzi anaoufanya! Ajifunze makosa na matukio hasi ya kihistoria. Ajue kuwa hii nchi ina katiba isiyoandikwa na isiyongelewa hadharani! Umoja wetu na amani yetu kwa sehemu kubwa vinasababishwa na katiba hiyo kuliko mabavu ya urais. Hii nchi ina unyonge katika mambo kadhaa ña watangulizi wa Samia (kama JMK) walitumia hekima kubwa na hata kulaumiwa kwa kwenda kinyume na ahadi zao au ilani ya CCM ili kuibakisha hii nchi katika umoja na amani yake. Historia pia inaonyesha wana-CCM sio watu wakusukumwa kirahisi wasiporidhika na mambo yanavyoenda.

Kwa hiyo sio Urais wala Uenyekiti wa CCM unaoweza kumwakishishia Mama Samia uungwaji mkono wa kuendelea kutawala bali hekima kubwa katika uongozi wake. Bado yuko kwenye "honey moon" lakini ikiisha wataanza (na wameanza) kumhukumu kwa maamuzi yake. Kama hana hiyo hekima ni vema atangaze mapema kama Joe Biden kuwa hatagombea urais mwaka 2025. Kuna faida nyingi kuliko hasara asipongombea.
 
Back
Top Bottom