Rais wetu mama Samia anapenda kusema yeye na Mwendazake ni kitu kimoja?, lakini kimatendo tunaona utofauti , mama kafanya mabadiliko kuanzia serikali yake hadi kwenye sekretari ya chama, tumeona watu waliokuwa vipenzi wa mwendazake kawaondoa kwenye nafasi zao, kwenye kodi anataka wananchi walipe bila mabavu, vyama pinzani vilivyokuwa havitakiwi kaahidi kukutana nao, mitandao kama twitter imefunguliwa, je mama anafanana wapi na mwendazake?