Rais Samia na Familia yake Wachangia Milioni 100 Ujenzi wa kanisa la Mtakatifu Karoli jimbo kuu la katoliki Arusha

Tuna mheshimiwa rais madame Dkt. Samia Suluhu Hassan, rais tajiri kupita wote Tanzania.

Tusisahau mchango wa familia yake kule Rufiji pia

 
Acha kuweweseka na kuwa na wivu kama shetani. Kwa hiyo unataka Rais wetu mpendwa na Jemedari wetu kipenzi cha watanzania asishiriki katika shughuli za kijamii? Ni vipi amechanganya Dini na Siasa? Acheni wivu na roho mbaya.
Anajaribu kuwaziba mdomo RC wasihoji kuhusu kuhonga bandari zetu kwa waarabu.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Rais wetu mpendwa na Jemedari wetu kipenzi Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hasssan kwa kushirikiana na Familia yake wamechangia kiasi cha Millioni 100 yaani mia moja ,ujenzi wa kanisa la karoli Lwanga jimbo kuu la katoliki Arusha,Usa River wilayani Arumeru. Ambapo mchango huo kama sadaka umewasilishwa kanisani hapo na Mheshimiwa mkuu wa mkoa wa Arusha Mwamba Mwenyewe Paul Makonda.

Ambapo Mheshimiwa Makonda amesema ya kuwa Rais wetu Mpendwa katoa sadaka na mchango wake huo huku ukiambatana na maneno kuwa ukatumike kupatanisha,kuunganisha na kujenga umoja wa Taifa letu. Kwamba ukisimama katika ukuta au mabati basi ukawe kama sehemu ya upatanisho.

Ambapo kanisa zima lililipuka kwa shangwe na nderemo kushangilia na kuimba nyimbo za shukurani kwa Mheshimiwa Rais na kumshukuru Sana kwa moyo wake wa upendo na ukarimu ambao amekuwa nao wa kuchangia na kujitolea mara kwa mara.

Hii ndio sababu ya kuendelea kuungwa mkono na mamilioni ya watanzania bila kujali madhehebu yao ,kwa kuwa Rais wetu kipenzi ameweke mikono yake na kupeleka michango yake kila sehemu bila kujali dhehebu. kama ambavyo tuliona akitoa zaidi ya shilingi milioni mia moja hamsini pale Mheshimiwa Mbowe alipomuomba awachangie kkkt.Rais SAMIA ni Mama wa Taifa,mlezi wa Taifa ,Rais na kiongozi wa wote ndio maana anawapenda watu wote na kuwatumikia wote bila ubaguzi kwa misingi ya aina yoyote ile. Ni mama mwenye huruma, unyenyekevu,ukarimu na upendo mkubwa sana kwa watanzania na Taifa letu kwa ujumla.

Rais wetu anataka watanzania tuishi kama Taifa na kushirikiana katika mambo yote bila kubaguana kwa itikadi za kisiasa au misingi ya kidini au ukabila au ukanda wala jinsia.ndio maana mikono yake imegusa watu wa dini zote na madhehebu yote.hii ndio maana ya kuitwa kiongozi na Mkuu wa Nchi,hii ndio maana ya kuitwa kiongozi wa wote,mfariji wa Taifa Na kiungaishi cha Taifa.

Rais Samia Anastahili pongezi na kuungwa mkono na kila mtanzania mwenye mapenzi mema na Taifa letu. Tumtie moyo na kumpa ushirikiano wa kutosha Mama yetu.tusimkatishe tamaa wala kumvunja moyo huu wa upendo alionao kwetu watanzania na Taifa letu.

Kazi iendelee,Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa.Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Kuchangia ujenzi wa makanisa Tanganyika (Tanzania bara) haitoshi, akemee vitendo vya ubaguzi dhidi ya wakristo nyumbani kwako Zanzibar.
 
Back
Top Bottom