Rais Samia na CCM wenzangu, ni utamaduni wa siku nyingi kila Rais kuwa na Waziri Mkuu wake, tunaomba utamaduni huo uendelee!

Kama sababu ipo hili sio tatizo. Kukiwa na tatizo kiutendaji ni hasara zaidi. Lakini kama hakuna shida ni vizuri kuendelea na aliyepo.
 
Uzandiki mtupu. Mmezoea serikali za majizi sasa kikwazo chenu mmeona ni Majaliwa, mmeshashindwa tayari. Wengi watageuka mawe ya Chumvi ila sio huyo mwamba.
 
Alikuwa njia panda, hawezi kukemea, hawezi kujitoa.
Hii inathibitishwa na hatua anazochukua.
Basi hana uzalendo wowote, ni unafiki tu. Kama angekuwa na uchungu kwa yale asiyoyapenda kwanini asijitoe?.
 
Watu wanaanza kumchimba Majaliwa

Majaliwa anaingia kwny record ya Cleopa David Msuya kuwa Waziri Mkuu wa Marais Wawili tofauti hapa nchini
 
2025 atateua mwingine baada ya uchaguzi mkuu
 

Wakati jaji Warioba na tume yake wanakusanya maoni juu ya katiba mpya, nilipendekeza kusiwe na kiongozi analipwa maisha yake yote. Nilipendekeza kiongozi akistaafu apewe nyumba sehemu atakayopendekeza, kisha malipo yaanze 200m-2b kulingana na nafasi husika kisha akapambane na hali yake. Huu mchezo wa kulipa mstaafu mpaka afe sio kabisa. Unamlipa mstaafu halafu unakuta alipokuwa madarakani alikuwa mwizi, katili na kuingiza nchi kwenye mikataba michafu, hii haikubaliki.
 
Majaliwa yupo vizuri, utawala wa mwendazake bashite alikuwa na nguvu kuliko hata Prime minister.

Li-makonda halifai kupewa nafasi yoyote serikalini ,Wala kupewa favor yoyote huko kwenye biashara zake
 
Naunga Mkono. Rais Samia teua Waziri Mkuu wako huyu alisimamia serikali iliyofanya uonevu mwingi sana kwa raia zaidi iliyowahi kuwepo hapa Tanzania hapo kabla. Mpumzishe kama ulivyofanya kwa Bashiru
Katika hiyo serikali samia hakuwepo?
 
Ungesimamia kwenye ile hoja ya kuongopea Taifa wakati ule hoja yako ingekuwa na uzito zaidi kuliko hiyo ya kusema kila rais na PM wake .

Kitendo cha kusema uongo ulokuja kuthibitika kwa jamaa kufa kingetosha kumshinikiza kujiuzuru hata kama kwa hiyari yake angekuwa hayuko tayari.

Kwamba ataaminikaje tena na wananchi?

Je inatakuwa na maana gani kuwa na kiongozi mkubwa ambaye hataaminika tena kwa wale anaowaongoza?

Kwamba kila atakachokisema au kukifanya wananchi watamchukuliaje baada ya kitendo kile?

Kwanini afanya vile?

Nini kilimsukuma kufanya vile?

Kwa manufaa au maslahi gani na ya nani?

Tunataka majibu.

Hapo mleta mada yamkini ungeeleweka vizuri na kuufanya mjadala wako kuwa na radha.
 
Tulisema tunapiga marufuku uchifu, tuwe na jamii ya watu walio sawa. Wasio na madaraja tofauti.

Lakini kiukweli bado tunaendeleza uchifu.

Watu wengine wanalipwa maisha yao yote hata baada ya kustaafu, wengine wanaachwa wapambane na hali zao.

Hii si jamii ya watu sawa wasio na madaraja. Hii ni jamii ya watu wenye madaraja tofauti.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…