Rais Samia na CCM wenzangu, ni utamaduni wa siku nyingi kila Rais kuwa na Waziri Mkuu wake, tunaomba utamaduni huo uendelee!

chiembe

JF-Expert Member
May 16, 2015
11,959
20,530
Ni kawaida kwa Rais, mara tu anapoanza awamu yake ya uongozi, kuteua Waziri Mkuu wake,mtu anayemwamini,atakayeenda na falsafa yake, bila kumuwekea makundi.

Marais huwa wanaachana na Mawaziri wakuu wa watangulizi wao kuashiria zama mpya, pia kuvunja kundi la kisiasa la aliyemteua.

Ni wazi, lile kundi lililokuwa na imani na ndugu yule likiangalia katika safu ya uongozi, linaweza kujaribu kumtikisa mama kupitia kwa huyo. Maana safu nzima imebadilika. Na sasa wananchi wanamuelewa sana mama kuliko wakati mwingine.

Ni vyema wasimamizi wakuu wa Sera za mwendazake, sasa wampishe mama atusukie nchi ya kisasa ya kisomi na ya kitaasisi

#matege
Code-SSH-2025
 
Kubadili Waziri Mkuu bila ya sababu zisizoepukika ni gharama sana, kwani tunakuwa na msururu wa mawaziri wakuu wastaafu wanaohudumiwa na serikali.

Sasa hivi tuna Salim, Warioba, Malecela, Msuya, Sumaye, Lowassa, Pinda. Wote ni mawaziri wakuu wqnaohudumiwa kwa stahiki za wastaafu.

Unataka kuongeza Majaliwa naye?

Kwa sababu hii, hutaona Waziri Mkuu akibadilishwa.
 
Tuko
Kubadili Waziri Mkuu bila ya sababu zisizoepukika ni gharama sana, kwani tunakuwa na msururu wa mawaziri wakuu wastaafu wanaohudumiwa na serikali.

Sasa hivi tuna Salim, Warioba, Malecela, Msuya, Sumaye, Lowassa, Pinda. Wote ni mawaziri wakuu wastaafu.

Unataka kuongeza Majaliwa naye?

Kwa sababu hii, hutaona Waziri Mkuu akibadilishwa.
Tayari kumgharamia, lengo nchi isonge mbele
 
Tutambue kwamba tofauti na ma Rais wengine waliotangulia, SSH aliingia bila kujiandaa wala kutegemea. Yeye mwenyewe was in shock... Hakuwa na kambi. Katika mazingira kama yale ilikuwa busara kwanza kuendelea na mtu mzoefu
 
Tuko

Tayari kumgharamia, lengo nchi isonge mbele
Nakwambia hivi, mtapiga soga sana hapa JF, lakini Waziri Mkuu habadilishwi.

Haya ni mambo ambayo uongozi wa CCM ulishayapitisha, si maneno ninayosema mimi tu.

Kama unataka kuchangamsha baraza, endeleza soga.

Kama unataka kuelewa nini kitatokea na sababu zake, nishakueleza.
 
Sijakuelewa mkuu, ila Rais anapoapa, huwa anaapa kulinda mila na tamaduni, sisi tumeomba alinde utamaduni huu, wenyewe tumeshauzoea
Ok... Nimeona umebadilisha umeandika kuvunja badala ya kubunja.. nimeelewa Sasa
 
  • Thanks
Reactions: Paf
Naunga Mkono. Rais Samia teua Waziri Mkuu wako huyu alisimamia serikali iliyofanya uonevu mwingi sana kwa raia zaidi iliyowahi kuwepo hapa Tanzania hapo kabla. Mpumzishe kama ulivyofanya kwa Bashiru
Wakati wa uonevu Mama Yenu Samia alikuwa wapi??
 
Nakwambia hivi, mtapiga soga sana hapa JF, lakini Waziri Mkuu habadilishwi.

Haya ni mambo ambayo uongozi wa CCM ulishayapitisha, si maneno ninayosema mimi tu.

Kama unataka kuchangamsha baraza, endeleza soga.

Kama unataka kuelewa nini kitatokea na sababu zake, nishakueleza.
Mkuu, sisis wanachi tunataka utamaduni uendelee, mama asilazimishwe kuwa na mtu asiyemtaka
 
Waziri mkuu akiwa chini ya dikteta atamwakilisha Dikteta, na nchi ikiwa chini ya mtu mwema atafanya wema. Mwanasiasa wa Tanzania hufanya kwa ajili ya masilahi kwa sababu wengi tunatoka kwenye familia maskini mazingira hayaruhusu MTU yeyote kuishi aaminivyo.
Hata raisi tuliyenaye alikuwa makamu wa hayati raisi Magufuli na alikuwa mtii kwake. Lakini leo ndo unagundua kuwa msimamo wake ni tofauti. Huwezi mjua majaliwa bila Majaliwa kupata nafasi ya umajaliwa.
 
Aendelee na huyuhuyu hadi awamu yake itakapoisha.
Gharama za kulea msururu wa mawaziri wakuu wastaafu ni mzigo kwetu...
 
Back
Top Bottom