Abu Ubaidah Commando
JF-Expert Member
- Sep 8, 2016
- 7,590
- 6,957
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan mapema leo amesema yeye hapendi Ukanda ila yeye ni "Mzanzibar!"
Kiukweli Rais kakosea sana kukemea ukabila huku yeye akitamka bayana ni wa mahali fulani.
Samia umekosea sana!
====
Samia Suluhu ninapotoka hatuna makabila. Kwetu kule Zanzibar tunajuana kwa maeneo...
Kwenye system ya makuzi – shule na siasa – tunamshukuru sana Baba wa Taifa Mwl. Nyerere. Kwahiyo, tunapofanya kazi hapa, na mimi binafsi, ninafanya kazi bila kuangalia kabila fulani.
Sasa watu wakifanya makosa, “nimewajibishwa kwakuwa ni kabila Fulani”. Sina kabila. Mimi hapa ukiniuliza kabila lako nani nitakwambia ni Mzanzibari.
Hata wangekuwa 1%, wingi si hoja. Kinacho angaliwa ni mantiki ya hoja zao.Naona mama ana jaribu kuwajibu sana watu wa mitandao, mi nadhani ange wapotezea hawafiki hata 10% ya watanzania
Mimi ni Mtanganyika na si Mmakunduchi, Mtumbatu, Mngazija, Mshirazi n,k.Lakin ukweli utabaki kuwa ukwel tu yeye ni Mzanzibar hlo tunajua na halpngik na litabk kuwa hvyo. japo kama Rais hakutakiwa kusema hvyo[emoji120]
Nimejikuta tu nayakumbuka maneno ya Mwl, "Mimi ni mzanzibar na wao ni wazanzibara..."
Kujuana kwa maeneo ndio regionalism yenyewe kujuana kwa makabila ndio tribalism yenyewe , so hakuna tofauti kati anayejitapa kwa kabila na yule anayejitapa kwa kanda.....Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan mapema leo amesema yeye hapendi Ukanda ila yeye ni "Mzanzibar!"
Kiukweli Rais kakosea sana kukemea ukabila huku yeye akitamka bayana ni wa mahali fulani.
Samia umekosea sana!
====
Samia Suluhu ninapotoka hatuna makabila. Kwetu kule Zanzibar tunajuana kwa maeneo...
Kwenye system ya makuzi – shule na siasa – tunamshukuru sana Baba wa Taifa Mwl. Nyerere. Kwahiyo, tunapofanya kazi hapa, na mimi binafsi, ninafanya kazi bila kuangalia kabila fulani.
Sasa watu wakifanya makosa, “nimewajibishwa kwakuwa ni kabila Fulani”. Sina kabila. Mimi hapa ukiniuliza kabila lako nani nitakwambia ni Mzanzibari.
Wapo wahadimu, wamakunduchi n.k aache kupotosha watuZanzibar hakuna makabila eti?
Sijawahi ona uwezo wako wa kuona. Rais ndie alfa na omega, lolote alitamkalo linatatafsiriwa kwa mapana.Watanzania tuna Mambo mengi tena Muhimu tu ya Kufanya na siyo huu Upopoma ( Upuuzi ) wako uliouleta hapa.
Sijaona tatizo kwa Rais kutamka hivyo.
Hana kabila, lakini ni mdini mzuri.
Angejitambulisha kwamba yeye ni Mkojani au Mnungwi isingekuwa na tatizo lolote. Ni sawa na ilivyokuwa haina tatizo kwa JPM alivyokuwa akijitambulisha kwamba alikuwa Msukuma. Pamoja na kwamba tulikuwa tunafahamu kwamba JPM alikuwa Mtanganyika, lakini ingeleta kero sana kama kwa siku yoyote angejitambulisha kwamba alikuwa Mtanganyika. Hata Samia kwa kujitambulisha kwamba yeye ni Mzanzibar kakosea na nadhani haina afya kwa taifa. Kujitambulisha kwa kutumia utaifa wetu wa zamani ambao kimsingi ulishakufa siyo vyema sana.
Basi Samia ni mmakonde
Naona mama ana jaribu kuwajibu sana watu wa mitandao, mi nadhani ange wapotezea hawafiki hata 10% ya watanzania
Makbila ni mengine tena yakiwa na asili ya bara hasa unakuta Waha, Wamakonde, Wangoni, Wadigo, Wamanyema, Wasukuma, Wanyamwezi, na masalia ya mwambao wa Pwani na visiwa vya Komoro kwa hiyo kila mtu ana kabila la asili na dini aliyokuzwa nayo kama hakubadili mwenyewe.Zanzibar hakuna makabila eti?