Rais Samia: Maridhiano si udhaifu

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,162
Reaction score
17,628
Rais Samia Suluhu amesema maridhiano ni ishara ya ukomavu wa kisiasa unaojenga umoja na kuheshimiana, akisisitiza kuwa siasa zinapaswa kuongozwa na hekima, utu na maslahi ya taifa badala ya mivutano isiyoisha.

Amesema wananchi wanahitaji amani, usalama na utulivu, akizungumza Julai 9, 2026, wakati wa kushuhudia Tamko la Pamoja la Maridhiano ya Kisiasa kati ya CCM na ACT-Wazalendo katika Viwanja vya Ikulu, Zanzibar.

Your browser is not able to display this video.
 
rais hassan anaonekana kuwa mtunzi mzuri wa mashairi kuliko kiongozi mkuu wa nchi
 
haya maneno ni ya kwake?

sisi tulioamini huwa tunajua kuwa ni jambo zuri na bora pale mtu anapojutia matendo yake na kutubu kwa kuyaungama. Akifanya hivi kwa moyo wa dhati huwa kuna tija
 
maisha ya kuishi kwa kuchukiana huwa ni magumu sana. Mioyo yetu haikuumbwa kubeba chuki, bali upendo
ccm ilishapanga toka mwanzoni kwamba watafanya uchafu wote halafu baada ya hapo wataomba maridhiano..

Walikuwa na nia ovu toka siku ya kwanza na walisuka mipango yote, ndio maana Polepole alisema mwanzoni kabisa na alijua huu mpango sababu alikuwa ndani ya mfumo akasema "msikubali".

Kuna kakikundi ka watu wachache ndani ya ccm ambapo ndio wanaratibu haya yote...
 
so, hako kakikundi tukafanyeje. Tukipata jawabu tutakuwa tumepiga hatua kubwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…