Rais Samia Suluhu Hassan, amesema hayo leo Januari 13, 2026 wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Mahakimu na Majaji Tanzania (TMJA) katika viwanja vya Makao Makuu ya Mahakama (Judiciary Square), mkoani Dodoma.
"Nitoe msisitizo kwamba kwa upande wetu Serikali, tutatimiza wajibu wetu wakuendelea kuimarisha huduma za Mahakama, lakini niwatake nanyi kutimiza wajibu wenu ndugu zangu Majaji na Mahakimu ambao ni kusimamia HAKI kwa kuzingatia KATIBA, SHERIA na MAADILI bila hofu, huba wala upendeleo na hiki ndicho kiapo chenu"