Rais Samia, Linda Mausha ya Watu: Itungwe Sheria ya Kuwaadhibu Viongozi wa Serikali Ambao Madereva Wao Wanaendesha Magari Hovyo

Bams

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
16,559
41,078
Tanzania ni miongoni mwa nchi zenye magari machache lakini ni miongoni mwa nchi zinazoongoza kwa idadi ya vifo vinavyosababishwa na ajali za barabarani.

Nchi nyingine, ukiwa kiongozi, unatakiwa kuwa mfano katika kutii na kufuata sheria, unatakiwa kuwa mtu wa mfano katika kutenda kila kitu kwa kadiri ya sheria na taratibu. Kwetu ni kinyume, yaani mtu akiwa kiongozi ni kama ameruhusiwa kutenda uovu wowote bila ya kubughudhiwa na yeyote.

Ukiwa barabarani, unachoweza kushuhudia ni kuwa magari yanayoendeshwa hovyo kabisa kuliko yoyote, yasiyofuata wala kutii alama yoyote barabarani ni magari ya Serikali. Mambo hayo ya hovyo barabarani, mara nyingi yanafanyika huku hao viongozi wakiwa ndani ya hayo magari.

Hivi tunaamini kwamba dereva anaweza kuendesha gari hovyo kiasi tunachoshuhudia bila ya kupata baraka ya huyo kiongozi anayeendeshwa? Haiwezekani. Lazima huyo kiongozi ameridhia gari lake liendeshwe kwa namna hiyo hatarishi au ndiye aliyemwelekeza aendeshe bila ya kufuata sheria za usalama barabarani kwa sababu yeye hana wa kumgusa.

Magari ya Serikali ni machache sana proportionaly ukilinganisha na magari mengine, lakini takwimu za ajali zilizosababishwa na magari haya, ni za kushangaza sana. Yaani waliotakiwa kuwa mfano kwa mema wamekuwa mfano kwa uovu. Na wengine, kwa sababu ya ujinga wao kudhania kuwa jkiwa kiongozi basi huwezi kufa kwa ajali, wamekufa kizembe kwa sababu ya uendeshaji mbaya wa magari yao.

Kuna wakati nilishuhudia gari la Serikali, landcruizer mkoani Musoma kuelekea Mwanza, ikienda mwendo wa kasi ya ajabu, huku pembeni ya barabara kukiwa na watoto wengi wadogo wa shule ya msingi. Haikupita muda, naenda mbele nakuta watu wamejazana, mtoto amelala barabarani amekufa. Amegongwa na dereva mpumbavu anayemwendesha kiongozi au mtumishi mpumbavu wa Serikali.

Leo hii, uwapo barabarani, potential hazards kubwa zinazoweza kukusababishia ajali ni magari ya Serikali na bodaboda.

Kama magari yote yangekuwa yanaendeshwa hovyo kama yanavyoendeshwa magari ya Serikali, kila siku tungekuwa tunasikia misiba ya viongozi. Ajali za magari ya Serikali zinapunguzwa na umakini wa madereva magari mengine. Magari ya Serikali yanaendeshwa kama vile hao viongozi hawajali usalama wa watu wengine, na wao wenyewe wamekabidhi uhai wao utunzwe na watu wengine.

PENDEKEZO

Tuondoke kwenye huu utamaduni wa viongozi kiwa mfano wa uovu, twende kwenye utamaduni mpya, wa viongozi kuwa mfano mzuri badala ya mfano mbaya, kuwa mwanga badala ya giza.

Kufanyike program maalum ya kufuatilia uendeshaji wa magari ya Serikali. Linaloendeshwa hovyo, dereva aadhibiwe mara mbili, kwanza kwa traffic office act, na pili kwa kukosa sifa ya kazi anayoifanya. Kiongozi ambaye yumo kwenye hilo gari afukuzwe au ajiuzulu kwa kuruhusu uovu kutendeka mbele yake au kwa kuchangia kutendeka kosa.

Wakifukuzwa viongozi watano 5, na madereva labda 20 tu, magari ya Serikali yataendeshwa vizuri, hayatakuwa visababishi vya ajali wala kuwa hatari kwa watumiaji wengine wa barabara.

RAIS SAMIA, ana kazi kubwa ya kuwa-shape viongozi wahuni, wasio na maadili, nidhamu, wala weledi.

Chanzo kikubwa cha kudumaa kwa Afrika ni uongozi duni. Siku Afrika itakapopata viongozi makini, werevu, wenye maadili, itapaa.


Mod, tafadhali nirekebishia Kichwa cha Mada. Isomeke maisha na siyo mausha.
 
Pia umesahau magari binafsi mengi huko highway yanaendeshwa na madereva wasio na uzoefu wa kutosha kuwa highway. Akipata changamoto kidogo, anaingia mtaroni...
 
Pia umesahau magari binafsi mengi huko highway yanaendeshwa na madereva wasio na uzoefu wa kutosha kuwa highway. Akipata changamoto kidogo, anaingia mtaroni...
Sijawataja hao siyo kwamba madereva wengine wote ni watakatifu lakini tunataka magari ya Serikali na viongozi wa Serikali wawe mfano mzuri kwa wengine, sivyo kama ilivyo sasa ambapo wao ndio wamekuwa wavunja sheria wakubwa, na wahatarishaji usalama wa watu wengine.
 
Tuondoke kwenye huu utamaduni wa viongozi kiwa mfano wa uovu, twende kwenye utamaduni mpya, wa viongozi kuwa mfano mzuri badala ya mfano mbaya, kuwa mwanga badala ya giza.

Kufanyike program maalum ya kufuatilia uendeshaji wa magari ya Serikali. Linaloendeshwa hovyo, dereva aadhibiwe mara mbili, kwanza kwa traffic office act, na pili kwa kukosa sifa ya kazi anayoifanya. Kiongozi ambaye yumo kwenye hilo gari afukuzwe au ajiuzulu kwa kuruhusu uovu kutendeka mbele yake au kwa kuchangia kutendeka kosa.
Wanaoongoza kwa kuvunja sheria za barabarani ni hawa
  1. JWTZ
  2. PT
  3. 01JU, 02JU, 03JU, 04JU
  4. SKG
  5. MT
  6. ZM
  7. Wasiojulikana
  8. DFP
  9. ST
  10. Wabunge
 
Back
Top Bottom