SI KWELI Rais Samia kwenye kampeni zake amesema ataigawa TANESCO kwa waarabu kuongeza ufanisi

SI KWELI Rais Samia kwenye kampeni zake amesema ataigawa TANESCO kwa waarabu kuongeza ufanisi

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Wakuu nimekutana na hizi taarifa je kuna ukweli wowote huko?
1759136702636.jpeg
 
Tunachokijua
Vyama mbalimbali vya Siasa nchini Tanzania vipo katika mchakato wa kampeni kuelekea uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika Oktoba 29, 2025. Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Rais Samia Suluhu Hassan alikuwa mkoa wa Pwani (Kibaha na Chalinze)

Madai

Kupitia mitandao ya kijamii ikiwemo Instagram, Septemba 29 zilisambaa grafiki zikiwa na utambulisho wa Clouds TV zikiwa zimebeba jumbe mbalimbali kumuhusu Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, Rais Samia Suluhu Hassan. Miongoni mwa ahadi hizo ni;

  • Kuwapa Bandari ya Bagamoyo DP World
  • Kuwapa Waarabu shirika la TANESCO ili kuongeza ufanisi
  • Hata wananchi wasipopiga kura CCM itashinda
Uhalisia wa Taarifa hiyo

JamiiCheck imefuatilia na kujiridhisha kuwa Taarifa hiyo Si ya kweli.

Kupitia mikutano ya kampeni ambayo Rais Samia aliifanya katika mkoa wa Pwani Septemba 28, 2025 hakuzungumza maneno hayo.

Akiwa Kibaha na Chalinze Rais Samia alinadi ilani ya chama chao na kueleza mambo watakayoyafanya katika mkoa huo ikiwa watapata nafasi. Miongonj mwa mambo waliyoya ahidu ni kuboresha miundombinu ikiwemo bandari.

Kuhusu umeme alisema kuwa wataweka vituo vya kupoza umeme Msufini, Mkuranga pamoja na Segereni Kibaha na Zinga, Kibaha.

Aidha grafiki zilizotumika kusambaza grafiki hizo ni za kughushi na hazijachapishwa na Clouds TV kama inavyoonekana. Hata hivyo ujumbe unaooenakana kutoka katika ukurasa wa X na kudaiwa kuwa umechapishwa na mgombea huyo ni wa kughushi na haujachapishwa katika ukurasa wake rasmi wa X.
samia-1-jpg.3480748
ujumbe-1-jpg.3480745
Kwani TANESCO haiwezi kubinafishwa kama inaleta hasara?
Kama BANDARI imepewa DP World Why not kwa TANESCO

Muda mwingine tupunguze kujielezea sana
Ni swala muda tu lolote linaweza tokea
 
Kuna mtu humu JF aliwahi kusema, ukiona mauzo/ubinafsishaji wowote kapewa Mwarabu basi ujue biashara hiyo ni ya Wanamtandao.
 
Back
Top Bottom