Mpwayungu Village
JF-Expert Member
- Jul 21, 2021
- 14,575
- 31,013
Nimekuwa nikifuatilia hotuba za Rais Samia, yaani muda mwingi anatumia kumpamba mwanamke na kutunyooshea vidole wanaume. Hii hali anayokuja nayo Rais siyo salama maana huko mbele itapelekea watanzania wasiwe na imani naye tena. Huwenda si yeye tu hata wanawake kwa ujumla atakuwa amewatia doa.
Mnataka wanawake mpendwe vipi? Tayari Mama Samia ni rais anataka nini tena? Yaani imefika hatua anateua viongozi wengi wanawake kutukomoa wanaume, badala ya kuteua viongozi kulingana na weledi, sifa na utashi. Siyo kuangalia jinsia kama unavyofanya.
Ninavyo muona huyu Rais Samia yaani anatamani hata leo Spika awe mwanamke, Jaji Mkuu awe mwanamke, Mkuu wa Majeshi awe mwanamke. Uteuzi wa hovyo wa Waziri wa Ulinzi pamoja na Mabalozi mbalimbali umeyathibitisha haya.
Achilia mbali majukumu aliyonayo mwanaume ndani ya familia, hebu tuangalie yafuatayo halafu tuone wanawake tunawanyanyasa kama Afghanistan
au tumewapa vipaumbele vya kutosha?
1. Nafasi za viti maalumu haziwahusu kabisa wanaume ni wanawake tuu, tena ni nyingi kiasi cha kukaribiana na viti vya majimbo. Yote haya Rais Samia hataki kuridhika, hivi wanawake mpendwe vipi?
2. Wizara nyeti nyingi zimekaliwa na wanawake. Mbali na kuwa Taifa la Marekani ni kongwe kidemokrasia lakini sijawahi kusikia mwanamke akaiongoza pentagon. Ila hapa tuna Waziri wa Ulinzi mwanamke na hakuna aliyehamaki.
3. Wanawake hupewa vipaumbele kuliko wanaume kwenye selection za shule, vyuo pamoja na ajira. Bila pingamizi inawezekana kabisa mwanaume akawa na daraja la kwanza lakini akaachwa akachukuliwa mwanamke mwenye daraja la Tatu. Hapa sasa tunafuata gender equity au?
4. Rais Samia nakuomba zingatia katiba na ilani ya Chama Cha Mapinduzi ambacho japo ni kichefuchefu mbele ya watanzania. Maana hakuna mtanzania anataka katiba hii wala CCM lakini, tunaomba ufuate ajenda zenye vipaumbele kwa taifa kuliko kujinadi ukike wako kila siku jambo ambalo halina tija kwa wananchi.
NB: Haya ni maoni tu maana nina haki kikatiba ya kumkosoa kiongozi yeyote na siku zote unapokosolewa ndiyo unakuwa imara.
Asante
Mnataka wanawake mpendwe vipi? Tayari Mama Samia ni rais anataka nini tena? Yaani imefika hatua anateua viongozi wengi wanawake kutukomoa wanaume, badala ya kuteua viongozi kulingana na weledi, sifa na utashi. Siyo kuangalia jinsia kama unavyofanya.
Ninavyo muona huyu Rais Samia yaani anatamani hata leo Spika awe mwanamke, Jaji Mkuu awe mwanamke, Mkuu wa Majeshi awe mwanamke. Uteuzi wa hovyo wa Waziri wa Ulinzi pamoja na Mabalozi mbalimbali umeyathibitisha haya.
Achilia mbali majukumu aliyonayo mwanaume ndani ya familia, hebu tuangalie yafuatayo halafu tuone wanawake tunawanyanyasa kama Afghanistan
au tumewapa vipaumbele vya kutosha?1. Nafasi za viti maalumu haziwahusu kabisa wanaume ni wanawake tuu, tena ni nyingi kiasi cha kukaribiana na viti vya majimbo. Yote haya Rais Samia hataki kuridhika, hivi wanawake mpendwe vipi?