Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 2,437
- 5,235
Msemaji wa Serikali, Gerson Msigwa amesema Rais Samia Suluhu Hassan ataowangoza Watanzania katika tukio la kumuaga marehemu Waziri Mkuu na Makamu wa Rais mstaafu, Cleopa Msuya.
Hafla hiyo itakayoambatana na ibada maalumu, inatarajiwa kufanyika Mei 11, 2025 katika viwanja wa Karimjee kuanzia saa 3 asubuhi na kuongozwa na viongozi wa dini, pia, kutakuwa na salamu za viongozi mbalimbali pamoja na kuaga mwili.
Msuya alifariki dunia Jumatano Mei 7, 2025 saa 3 asubuhi katika Hospitali ya Mzena iliyopo jijini Dar es Salaam, alikokuwa akipatiwa matibabu ya moyo. Amekuwa akipatiwa matibabu katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Mzena na huko London nchini Uingereza.
Soma Pia: Mzee David Cleopa Msuya afariki Dunia akipatiwa matibabu hospitali ya Mzena
Akizungumza na waandishi wa habari leo Mei 9, 2025, Msigwa amesema kamati ya kitaifa ya mazishi ya viongozi inayoongozwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, kwa kushirikiana na familia ya marehemu, imeendelea kuratibu hatua mbalimbali za msiba na kujumuisha kuhifadhi mwili wa marehemu.
“Uratibu umejumuisha uagaji, salamu za rambirambi, usafirishaji wa msiba na mazishi yatakayofanyika katika Kijiji cha Usangi,” amesema Msigwa ambaye pia ni na Katibu Mkuu wa Wizara Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Amesema kwa sasa maombolezo yataendelea Jumamosi Mei 10, 2025, mwili wa marehemu utafikishwa nyumbani kwake Upanga, jijini Dar es Salaam kwa ajili ya taratibu za kifamilia.