Rais Samia kuhusu 'SU Tv' umekosea, kwakuwa ni mwanzo tunakukumbusha na kukusamehe

Unajua huyu mama anafikiri urais ni kupata faida. Hii itatupa shida na tulivyozoea kuona rais anayechukulia kazi hiyo kujitolea maisha. Mama Aameanza hivyo utaona mambo ya kishikaji yanarudi kwa nguvu na rushwa itapanda tena kichwa. Natamani sana afanye term moja tu kisha tuombe mungu chama cha mapinduzi watuletee mtu mwanamapinduzi aina ya magufuli.
Hata hayati hakuwa msafi kama alivyotaka watu wamuone. Aliweza kutumia vizuri hekima ya kuwa na kauli yenye kumuonyesha kwamba na yeye ni sehemu ya wahangaikaji wengi.

Udhaifu wa Mama Samia ni kwamba wapo wanaume wawili ambao hawezi kuukwepa ushawishi wao, JK na mume wake. Kama mume wake ni mfanyabiashara mkubwa basi ule ushawishi wa wafanyabiashara mbele ya watendaji wa serikali na mamlaka zake utarudi kama awamu ya nne.

JPM aliweza kuwafanya watendaji wake wakawa na nguvu ya kimaadili, waliweza kukwepa vishawishi vya wenye pesa na hivyo mamlaka zao zikawa na jeuri ya kupeleka gawio hazina.
 
Kuna utaratibu wa viongozi kutangaza mali zao
na utaratibu huo haujumuishi kiongozi kutangaza kuwa HANA MATANGAZO KWENYE KITUO CHAKE, au HANA UWEZO WA KULIPA MISHAHARA
Hizi statement mbili zinammanisha yafuatayo
1. Kiongozi anaomba wafanyabiashara na umma kwa ujumla wakatangaze katika chombo chake
2. Kiongozi anaalika wawekezaji katika biashara yake ili iweze kujiendesha
Safi mkuu ila hii ni tafsiri yako sio yangu au ya mwingine
 
Rais kapotoka, aibu! Kwa nini rais amiliki chombo cha habari? Aweke mali zake zote hadharani? Watanzania tuna hasara sana na hawa waswahili waswahili na ujanja ujanja wao. Ndio sababu amegoma kuhamia Dodoma anaangalia interest zake zaidi.
Rais akikaa Dodoma anaongeza nini kwenye pato la nchi au lako?
 
Katika Mkutano wa kikazi kati ya Mh Rais wa AWAMU YA SITA na Waandishi wa habari/wamiliki wa vyombo vya habari na wanahabari, Mh Rais labda kwa kufahamu au kutofahamu alifanya PROMOTION/MARKETING ya biashara yake mwenyewe/binafsi.

Promotion nini?? (the publicizing of a product, organization, or venture so as to increase sales or public awareness).

Watanzania bara na wengine visiwani, kwa wingi wetu hatukujua kuwa kuna kituo cha TV kinaitwa SU TV, tena hatukujua kuwa mmojawapo wa wamiliki wa kituo hiki ni Mh. Rais mwenyewe. Zaidi hatukujua kuwa kituo hiki hakina matangazo ya kutosha ? Zaidi ya hapo hatukujua kabisaaa kuwa Mh Rais anafanya biashara ya Habari.

Lakini katika wasaa wa kujibu maswali Mh Rais alitaja zaidi ya Mara Tatu kuhusu umiliki wake wa Kituo Husika, Lakini pia alitoa taarifa ambazo kwa namna moja au nyingine zinaelekea kama alikuwa anakinadi kituo hiki.

Mh Rais kwa wewe kusema tu unamiliki Kituo cha TV kwenye Public tena kwa kukitaja jina lake la kibiashara, unategemea taasisi za serikali wataacha kupeleka matangazo huko? Unategemea makampuni ya wawekezaji wataacha kufanya biashara na hicho kituo?

Kwa kusema tu kuwa kituo hakina uwezo wa kujiendesha na kuwalipa wafanyakazi mshahara, unategemea hapatatokea wafadhiri lukuki kukisaidia kituo hiki?

WAPI UMEKOSEA
  1. Kwa kuwa kikao kilikuwa cha kikazi na ulikua unaongea na watanzania kupitia wanahabari, cha kwanza hukupaswa kabisa kutaja kituo chako cha habari kwa kuwa hiyo tayari inakuwa Conflict of Interest.
  2. Kwa kutambua kuwa wewe ni Taasisi, na Kiongozi wa Kitaifa, katika matukio ya kikazi si sawa kutangaza au kutaja kwa jina (brand name or business name) biashara ya mtu au bidhaa kwa uzuri au ubaya, kwani promotion/marketing inaweza kuwa negative au positive. Na neno lako kwetu sisi ni maagizo.
  3. Ulipaswa tu kusema unamiliki kituo cha television tena bila kukitaja jina lake halisi, kwa kukitaja tu Jina hii ni Marketing/promotion direct, hivyo umetumia platform ya umma kufanya Tangazo Binafsi.
  4. Pia ni vyema ungeanza mkutano kwa ku declare interest kwa wamiliki wenzio na Watanzania kwa Ujumla, lakini bila kutaja jina la chombo.
  5. Kwa kuwa umetuambia kuhusu umiliki wako sasa ni vyema pia tukajua share zako binafsi ni ngapi?
Natumai ushauri huu utauelewa

KAZI IENDELEEEEEE
Ni sahihi lakini hata asingekitaja kwa jina bado wasaka fursa tungechimba tukijue Ili iturahisishie kwenye michongo yetu 😄😄😄
 
Mtoa hoja una unafiki mkubwa wa ukweli,tatizo lipo wapi hapo?kwanza ni vema viongozi wote watangaze mali zao hadharani including kama wana share kwenye biashara yeyote ili wananchi wajue,na sio mbaya kwa President kutangaza hadharani interest zake,hapo SA wana President ambaye ni billionaire but ametangaza zote hadharani na amejitoa kuwa director kwenye kampuni zake,ni vema all our leaders wakaweka hadharani hii issue,President Samia she is very honest katika maisha yake ,tusichukulie kuwa hii ni weaknesses yake,hii ni uaminifu wake.
Huwezi kuweka noun na pronoun kwa pamoja yaani [\B]President Samia she is very honest[\] badala yake inatakiwa iwe President Samia is very honest

Sent from my TECNO F3 using JamiiForums mobile app
 
Likely hana nia mbaya.

Just some naivety on her part
Mmh. May be so may be not lakini kwenye business tunasema amedhamiria kupata unfair advantage over other media houses ambayo haina tofauti na cartels whether through sheer naivety or calculated manipulation..
 
Mbona mashamba yake ya mbogamboga na karafuu hamjadili.
TV yenyewe amesema inamtia hasara.Msimshambulie

Mmdai ripoti ya BOT na wale waliotaka kumuwekea Giza kuwa Rais kwa mjibu wa katiba.
 
Back
Top Bottom