Rais Samia kuhusu 'SU Tv' umekosea, kwakuwa ni mwanzo tunakukumbusha na kukusamehe

SONGOKA

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
1,843
1,841
Katika Mkutano wa kikazi kati ya Mh Rais wa AWAMU YA SITA na Waandishi wa habari/wamiliki wa vyombo vya habari na wanahabari, Mh Rais labda kwa kufahamu au kutofahamu alifanya PROMOTION/MARKETING ya biashara yake mwenyewe/binafsi.

Promotion nini?? (the publicizing of a product, organization, or venture so as to increase sales or public awareness).

Watanzania bara na wengine visiwani, kwa wingi wetu hatukujua kuwa kuna kituo cha TV kinaitwa SU TV, tena hatukujua kuwa mmojawapo wa wamiliki wa kituo hiki ni Mh. Rais mwenyewe. Zaidi hatukujua kuwa kituo hiki hakina matangazo ya kutosha ? Zaidi ya hapo hatukujua kabisaaa kuwa Mh Rais anafanya biashara ya Habari.

Lakini katika wasaa wa kujibu maswali Mh Rais alitaja zaidi ya Mara Tatu kuhusu umiliki wake wa Kituo Husika, Lakini pia alitoa taarifa ambazo kwa namna moja au nyingine zinaelekea kama alikuwa anakinadi kituo hiki.

Mh Rais kwa wewe kusema tu unamiliki Kituo cha TV kwenye Public tena kwa kukitaja jina lake la kibiashara, unategemea taasisi za serikali wataacha kupeleka matangazo huko? Unategemea makampuni ya wawekezaji wataacha kufanya biashara na hicho kituo?

Kwa kusema tu kuwa kituo hakina uwezo wa kujiendesha na kuwalipa wafanyakazi mshahara, unategemea hapatatokea wafadhiri lukuki kukisaidia kituo hiki?

WAPI UMEKOSEA
  1. Kwa kuwa kikao kilikuwa cha kikazi na ulikua unaongea na watanzania kupitia wanahabari, cha kwanza hukupaswa kabisa kutaja kituo chako cha habari kwa kuwa hiyo tayari inakuwa Conflict of Interest.
  2. Kwa kutambua kuwa wewe ni Taasisi, na Kiongozi wa Kitaifa, katika matukio ya kikazi si sawa kutangaza au kutaja kwa jina (brand name or business name) biashara ya mtu au bidhaa kwa uzuri au ubaya, kwani promotion/marketing inaweza kuwa negative au positive. Na neno lako kwetu sisi ni maagizo.
  3. Ulipaswa tu kusema unamiliki kituo cha television tena bila kukitaja jina lake halisi, kwa kukitaja tu Jina hii ni Marketing/promotion direct, hivyo umetumia platform ya umma kufanya Tangazo Binafsi.
  4. Pia ni vyema ungeanza mkutano kwa ku declare interest kwa wamiliki wenzio na Watanzania kwa Ujumla, lakini bila kutaja jina la chombo.
  5. Kwa kuwa umetuambia kuhusu umiliki wako sasa ni vyema pia tukajua share zako binafsi ni ngapi?
Natumai ushauri huu utauelewa

KAZI IENDELEEEEEE
 
Rais kapotoka, aibu! Kwa nini rais amiliki chombo cha habari? Aweke mali zake zote hadharani? Watanzania tuna hasara sana na hawa waswahili waswahili na ujanja ujanja wao. Ndio sababu amegoma kuhamia Dodoma anaangalia interest zake zaidi.
 
Mama aliteleza alifanya kosa la kiufundi. Natumaini anaingilika na kushaurika.

Alidhani anaonyesha concern yake kwa wanahabari ambayo ni tabia ya Mama zetu kuonyesha kujali na kutambua shida za wengine.

Kumbe upande mwingine wa maongezi yale haupo vizuri kwa cheo chake.
 
Katika Mkutano wa kikazi kati ya Mh Rais wa AWAMU YA SITA na Waandishi wa habari/wamiliki wa vyombo vya habari na wanahabari, Mh Rais labda kwa kufahamu au kutofahamu alifanya PROMOTION/MARKETING ya biashara yake mwenyewe/binafsi....
Likely hana nia mbaya.

Just some naivety on her part
 
Katika Mkutano wa kikazi kati ya Mh Rais wa AWAMU YA SITA na Waandishi wa habari/wamiliki wa vyombo vya habari na wanahabari, Mh Rais labda kwa kufahamu au kutofahamu alifanya PROMOTION/MARKETING ya biashara yake mwenyewe/binafsi...
Jiue msukuma,

Na asingekitaja baadae mngekijua mngesema hela ya serikali kafungua kituo Cha Tv , Dikteta. mbona yeye alikuwa ana makampuni kibao anayapa tenda za serikali,kina Manyanga company,,
 
Mtoa hoja una unafiki mkubwa wa ukweli,tatizo lipo wapi hapo?kwanza ni vema viongozi wote watangaze mali zao hadharani including kama wana share kwenye biashara yeyote ili wananchi wajue,na sio mbaya kwa President kutangaza hadharani interest zake,hapo SA wana President ambaye ni billionaire but ametangaza zote hadharani na amejitoa kuwa director kwenye kampuni zake,ni vema all our leaders wakaweka hadharani hii issue,President Samia she is very honest katika maisha yake ,tusichukulie kuwa hii ni weaknesses yake,hii ni uaminifu wake.
 
Katika Mkutano wa kikazi kati ya Mh Rais wa AWAMU YA SITA na Waandishi wa habari/wamiliki wa vyombo vya habari na wanahabari, Mh Rais labda kwa kufahamu au kutofahamu alifanya PROMOTION/MARKETING ya biashara yake mwenyewe/binafsi...
Wewe tatizo lako ni nini? Mbona ueleweki!!
 
Wewe unajua form yake ya maadili ya viongozi hakukitaja hiki kama moja ya mali anazo miliki?

Ndio maana kwenye katiba mpya tutataka kuwepo sheria ya kuwatenganiasha viongozi na biashara zao. Wakipewa uongozi wazikabidhi kwa wahindi na waarabu kwa uwazi sio kama sasa kwa kificho. Na waliokabidhiwa watungiewe sheria ya kuwafuatilia na kudhibiti mienendo yao. Sheria yenye meno, macho na masikio.
 
Back
Top Bottom