Rais Samia kuhudhuria mkutano wa CHADEMA ni upendo na maana ya uongozi thabiti

Maryam Malya

Senior Member
Nov 29, 2021
115
258
3466f843-bf29-4c7c-bdbe-c1c7c1509602.jpg


Na Mwl Udadis, Tarime

Kwa mara ya kwanza katika historia ya vyama vingi nchini, Rais aliyepo madarakani atakuwa mgeni rasmi katika shughuli ya Baraza la Wanawake wa Chama cha Upinzani, Chama chenye nguvu na ushawishi. Sio Mashariki wala Magharibi, katika siasa za ushindani Rais Samia ameweka historia ya kipekee.

Bingwa wa mafundisho ya uongozi na falsafa Duniani, Hayati Myles Munroe alipata kueleza kuwa kiongozi ni yule anayeonyesha njia na kuiishi. Kitendo cha kukubali kuwaunganisha watanzania bila kubagua vyama ni maana halisi ya uongozi na mfano wa njia ambayo kama Taifa tunaifuata.

Tofauti na viongozi wengine waliowahi kuonyesha ushirika kati ya Chama Tawala na Vyama vingine, Rais Samia hayuko katika kampeni za uchaguzi na pia amefanikiwa sana katika utawala wake hivyo kitendo cha kukubali ni suala la upendo tu na nia ya kuliunganisha Taifa katika misingi ya siasa zenye tija.

Licha ya jitihada nyingi zinazofanywa katika kukuza uchumi, kuboresha miundombinu na hali ya maisha ya watu, kufungua fursa kwa vijana na wanawake, kufanya mapinduzi katika sekta kama Kilimo, Utalii, Ufugaji na Viwanda, Rais Samia ameona haja ya kuliunganisha Taifa kwa misingi ya upendo na umoja.

MUNGU MMBARIKI RAIS WETU, MUNGU IBARIKI TANZANIA YETU
 
Nawaza angekuwa kaalikwa na ACT kwenye shughuli yao, maneno ya wanachedema humu kuhusu usaliti wa Zitto yangejaza server.
 
Huwezi kutawala watu kama hujawakusanya pamoja.

Mheshimiwa anajua anachokifanya.
 
Back
Top Bottom