Rais Samia kufanya ziara ya kikazi Kilimanjaro

Sema miradi mingine sio ya rais kuweka mawe ya msingi na uzinduzi. Mawaziri, katibu na wakuu wa mikoa wanatosha. Rais sahivi imekua changamoto watu kumfatilia live akiwa anaongea majukwaani. Vyema urudi utaratibu wa rais kuhutubia taifa walau mara moja kwa mwezi.
 
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kufanya ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani Kilimanjaro, ambapo

Amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika mkutano wa hadhara kwenye viwanja vya Chuo kikuu cha Ushirika Moshi ambapo Rais Samia atahutubia.

Amesema Oktoba 16, Rais atashiriki jubilei ya miaka 50, ya Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini (KCMC).

Chanzo: Mwananchi
Asante sana kwa taarifa hii. Siku hiyo ya tarehe 16 Oktoba ndio Siku ya Kimataifa ya Chakula Duniani, na maadhimisho yanafanyikia katika viwanja vya Pasua, Mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro. Kitendo cha Jubilei ya miaka 50 ya KCMC, ku coincide na Siku ya Chakula Duniani, What a coincidence?. Ila pia ni tukio gani muhimu zaidi kwa rais, kuhudhuria kama mgeni rasmi, kati ya tukio la jubilei ya miaka 50 ya taasisi binafsi ya KCMC na tukio la kitaifa na la kimataifa la kilele cha maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Chakula Duniani.

Tayari nimeisha tuma ombi hili kwa RC, Kilimanjaro.
P
 
Una laana wewe na mama yako na babako, shangazi zako, na wajomba zako, na watoto wako, na wajukuu zako, na vitukuu , hata kizazi cha kumi cha jamaa zako walaaniwe sawa sawa na maneno wevjamawa midomo yako!!
we jamaa,msamehe raia mwezako kama amekuuzi maana maandiko yana sema wabarikini wanao wauzi.Kilimanjaro imebarikiwa Tanzania ndio maana ssh anaidhuru
 
Una laana wewe na mama yako na babako, shangazi zako, na wajomba zako, na watoto wako, na wajukuu zako, na vitukuu , hata kizazi cha kumi cha jamaa zako walaaniwe sawa sawa na maneno ya midomo yako!!
Duh sio kwa laana hizo hapo akiikosa ya baba inakwenda ya mama ,shangazi, watoto, wajukuu kha!
 
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kufanya ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani Kilimanjaro, ambapo atazindua miradi, kuweka mawe ya msingi na kuzungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara.

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari, leo jumatano Oktoba 13, 2021, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Stephen Kagaigai, amesema Rais Samia, atawasili mkoani humo Oktoba 14 jioni na kuanza ziara oktoba 15.

Amesema akiwa mkoani humo, atazindua barabara ya lami ya Sanya Juu - Elerai yenye urefu wa kilomita 32 iliyogharimu zaidi ya Sh60 bilioni na kuweka jiwe la msingi kwenye jengo la wodi ya Mama na Mtoto katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mawenzi ambayo inatarajiwa kugharimu Sh12 bilioni hadi kukamilika.

Kagaigai amesema, Rais pia akiwa Kilimanjaro ataweka jiwe la msingi ujenzi wa daraja la Rau ambalo lilisombwa na maji ya mvua mwaka juzi, linalojengwa kwa gharama ya zaidi ya Sh900 milioni.

Amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika mkutano wa hadhara kwenye viwanja vya Chuo kikuu cha Ushirika Moshi ambapo Rais Samia atahutubia.

Amesema Oktoba 16, Rais atashiriki jubilei ya miaka 50, ya Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini (KCMC).

Chanzo: Mwananchi
Kwani bavicha wao wanasemaje?
 
Back
Top Bottom