BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,007
JE NI KWELI KAAGIZWA? NI LAZIMA ASEME?
Sakata la CHADEMA na Polisi huko Mwanza lina harufu ya hujuma zifuatazo:
1. Je ni kweli Mh. Rais kaagiza kongamano lizuiwe?
2. Kama kaagiza kwa nini amuagize RPC badala ya IGP?
3. Je ni kweli RPC kasema hadharani kuwa kaagizwa na Rais au kachomekewa maneno na waandishi?
4. Kama ni kweli RPC amesema kuwa katumwa na Rais, kulikuwa na ulazima wa yeye kusema hivyo hadharani? Uwajibikaji wa pamoja uko wapi?
NIONAVYO MIMI:
Uhuru ni kitu pekee kinachotakiwa kulindwa kwa gharama zozote. Kwa hiyo:
1. Wanaokusanyika kupinga katiba mpya wawe huru kama wanaokusanyika kuunga mkono.
2. Vyombo vya ulinzi vilinde katiba visilinde watu, vyama, wala Viongozi.
3. Kuzuia watu kukusanyika ni kuandaa watu kutokusanyika watakapotakiwa kukusanyika. Matumizi ya nguvu ni tabia ya tawala zisizokubalika (Illegitimate). Utawala wetu unakubalika kwa hiyo ujitenge na matumizi ya nguvu.
4. Zipo dalili pevu za njama na hujuma za kufarakanisha utawala huu na wananchi katika sekta nyingi: uchumi, siasa, usalama, na Haki za Binadamu. Adui wa kwanza wa utawala huu si wapinzani, si awamu iliyopita, NI serikali yenyewe inayoelekea kufarakana na kujianika.
Mama asirithi marafiki wala maadui. Atengeneze marafiki na maadui wake.
Lisemwalo LINAWEZA kuwapo. Ondoa miwani utaliona.
Askofu Bagonza