Rais Samia hongera sana kwa kuruhusu bidhaa za Kenya kuanza kuingia Tanzania

tunahitaji ngano ya bei nafuu maandazi na chapati tu afford kama zamani
Pole sana ndugu yangu, unajua serikali yenu ujamaa, si ndio ilitaifisha enzi zile mashamba toka kwa wazungu, waliokuwa wakilima mashamba makubwa ya ngano,kama kule Arusha,Mbeya na kwingineko,na baadae serikali ikaja shindwa kuyaendeleza...sasa inabidi tuwe wapole tu, manake kupata tena ngano hiyo ya hizo chapati na maandazi yako toka kwa hao 'mabeberu' itabidi sasa watuuzie kwa bei watakayo......kupanga ni kuchagua, nafikiri tuliyataka wenyewe... tujaribu kuinuka tulipokuwa na tusonge mbele.....au nadanganya ndugu zangu??........kazi iendelee.
 
Bei ndugu..bidhaa zetu ziko juu na ubora bado kidogo..Kenya watazalisha zaidi kuliko sisi...kwahio uchumi wao utakuwa kwa kasi zaidi wakati sisi tunajikongoja...tulianza kupiga hatua ila na wasiwasi tunarudi nyuma...unless vinavyokuja kwetu vipigwe kodi kubwa kuprotect soko la vitu vyetu..

Kwa mfano

Mo alikuwa yuko protected na product zake km margarine yake ilikuwa bei ya chini ila ni ngumu kidogo..na prestige ya Kenya ubora mzuri laini ila bei juu sana..sasa wanavyoruhusiwa bei ya prestige ikiwa sawa au chini kidogo au juu kidogo ya Mo margarine watu watanunua prestige maana ni laini na affordable na bidhaa ya Mo itabaki dukani muda mrefu mwishoe hatazalisha na Kenya watazidi kufyatua na kuuza and they will live happily ever after...

Sasa kuhusu Mo margarine kuuzwa Kenya...kuna shaka kidogo..km hapa Tanzania watu walikuwa wanaichukua sababu mbadala wake ni bei juu...inatakiwa kule Kenya itumike mbinu ya ziada ili itoboe...
Itasaidia sana kuboresha viwanda vyetu tulibweteka,bidhaa pia zitakuwa zenye ubora na bei nafuu kwa upande wa pili sera zetu ziwe shindani kimataifa 'our policies should be competitively harmonized'
 
Mna hangover za ujamaa ndo shida, ajira zipo viwandani tu? Sekta ya kilimo mnayoidharau inatoa 79% ya ajira zote hapa nchini, bado sekta ya uchukuzi is doing better, yaani we mwananchi unatengenezewa mazingira upate bidhaa bora kwa bei hafifu bado unalalamika? Watz nani kawaloga?
Kilimo bila viwanda ni kama unatwanga maji kwenye kinu mkuu....hao wakenya uchumi wao unafikiria umekua kwanini km sio viwanda...hio sekta ya uchukuzi inachukua nini?!

Mimi nashauri tukitaka maendeleo Tanzania washauri wa Raisi kwenye uchumi wawe wafanyabiashara km wakina Mo, Mzee wa Tanga Fresh etc...hawa wachumi wenye PHD za makaratasi ambao hawajahi kuuza hata kiberiti wapewe chaki wakafundishe vyuoni...
 
Hiyo ni kwa mujibu wako tu, tunaweza kukuza uchumi wetu kwa specialize na kilimo tu? Unauliza uchukuzi wa kuchukua nini? So kwa fikra zako sekta ya uchukuzi ipo kwa ajili ya bidhaa za viwanda tu? Bidhaa za mashambani ni marufuku kusafirishwa? Unataka rais mpaka awe mfanyabiashara ndo nchi inasonga? Kwa hiyo wanaosema urais ni taasis hao ni hamnazo ehh?
 
Pole sana ndugu yangu, unajua serikali yenu ujamaa, si ndio ilitaifisha enzi zile mashamba toka kwa wazungu, waliokuwa wakilima mashamba makubwa ya ngano,kama kule Arusha,Mbeya na kwingineko,na baadae serikali ikaja shindwa kuyaendeleza...sasa inabidi tuwe wapole tu, manake kupata tena ngano hiyo ya hizo chapati na maandazi yako toka kwa hao 'mabeberu' itabidi sasa watuuzie kwa bei watakayo......kupanga ni kuchagua, nafikiri tuliyataka wenyewe... tujaribu kuinuka tulipokuwa na tusonge mbele.....au nadanganya ndugu zangu??........kazi iendelee.
Kwahio tatizo ni ujamaa au akili yakivivu yakutochapa kazi na akili ya kifisadi ya kupiga madili na siasa zilizoleta tija..

Badala ya kupambana kumodernize kilimo, kuwezesha wananchi kufungua viwanda na kuprotect waliojitoa kimasomaso ili wapate nguvu ya kuexpand...sisi tuko busy tunatafutia masoko wengine..mtoto anaanza kujifunza kutembea unamvalisha raizoni
 
Hiyo ni kwa mujibu wako tu, tunaweza kukuza uchumi wetu kwa specialize na kilimo tu? Unauliza uchukuzi wa kuchukua nini? So kwa fikra zako sekta ya uchukuzi ipo kwa ajili ya bidhaa za viwanda tu? Bidhaa za mashambani ni marufuku kusafirishwa? Unataka rais mpaka awe mfanyabiashara ndo nchi inasonga? Kwa hiyo wanaosema urais ni taasis hao ni hamnazo ehh?
Soma vizuri tena
 
Hao wakenya wanataka kumpamba tu mama kishamba sijui wana agenda gani ya muda mrefu.

Jana tena tumesikia waziri wa biashara sijui wakilimo wamekutana na wenzao wa Kenya kujadili trade; hivi si tulisha sign ‘common market treaty’ ya EAC mwaka 2010 kufanya biashara zisizo na mipaka au.

Sasa hizi mbwembwe ni za nini as if ni jambo jipya kabisa.
Jiwe alivuruga kila kitu, tunaanza upya...
 
Kwa wale tunaoishi mpakani hii na nafuu kwetu kubwa sana, mipakani mfano Tarime Vijijini kukutana na vifaa vya Tanzania ni nadra sana. Hii itatusaidia upande wa ujenzi (cement), mafuta ya kula maana Kenya vina bei nafuu sana, sabuni, chumvi..!
Pia Kenya kuna soko nzuri sana la kuuza mahindi
Sahihi kabisa hata huku boda ya Taveta & Kitobo kwa kweli sasa watu wanapumua...
 
Tangia lini mtoto akatembea bila kutambaa

Nchi hii imefanyiwa figisu nyingi tangu ukoloni na wawekezaji wa kikoloni ili tuwe soko kwa bidhaa za Kenya

Nyie shabikieni ila madhara yake yatakutafuna wewe mpaka ukoo wako

Nchi hii tunahitaji kiongozi anaetambua wapo tumetoka na wapi tunaenda

Sasa nyie fungeni kanga kiunoni, chezeni kigodoro huku viwanda vya ndani vikifa na wananchi wakikosa ajira
Porojo tuuu...
 
Kwani tanzania hakuna viwanda vya juice na ngano vinavyoweza kuuza Kenya? Acheni hizo sera zenu za kizamani!

Sasa akina AZAM wataweza na wao kuuza juice zao na ngano Kenya. Bidhaa za AZAM zina ubora wa kushindana na kuzidi hata za Kenya.
Kabisa mkuu mfano Azam ana ngano grade one iko packed kwenye mifuko ya kijani ya kilo moja,na hapa nchini hiyo kilo moja ni sh 3,500... Aisee ni ngano bora sana kwa kuokea vitafunwa mbalimbali, yaani ubora wake hata Ulaya unauza sembuse Kenya??
 
Jiwe alivuruga kila kitu, tunaanza upya...
Waafrica tunapenda kuwa busy for nothing tuonekane tunarekebisha matatizo ya kutunga wenyewe.

Ukisha sign common market regional treaty kama ya EAC ambayo ina minajili ya super state; Kenya au Tanzania ikizingua hakuna kubembelezana.

Umepeleka bidhaa zako Kenya zimezuiwa mpakani swala ambalo limepelekea bidhaa kuaribika au kukuletea hasara ya aina yoyote iliyotokana na hayo maamuzi ya mpakani usisubiri serikali yako iingilie kati wewe mwenyewe unaweza kwenda mahakama ya EAC na kuishitaki serikali husika kudai fidia.

Juzi tu kuna watu wameshinda kesi sheria ya habari za Tanzania inakiuka makubaliano ya jumuiya Mahakama ya Afrika Mashariki yakataa rufaa ya Tanzania | DW | 10.06.2020

Hayo maamuzi yao kuanzisha common market na kila nchi kuridhia 2010 treaty kisheria yanatambulika kama ni mkataba, kuzuia bidhaa bila ya sababu maalum ni breach; nchi za wenzetu wazungu wana sue.
 
"Ukiona mke anadhurula hovyo lazima utakuta Nguo imechanika sehemu, hivyo safari zake ni kutafuta mafundi hodari ili waishone Nguo!!
 
Back
Top Bottom