Rais Samia hongera sana kwa kuruhusu bidhaa za Kenya kuanza kuingia Tanzania

Countrywide

JF-Expert Member
Mar 2, 2015
18,173
27,223
Mama Samia popote ulipo nakupa hongera Sana kwa hatua hii uliyofikia.

Mimi naweza kuwa tofauti na wengine kwenye kuliangalia hili suala. Bidhaa nyingi za ndani hazina ubora kabisa hivyo kuanza kuruhusu bidhaa za Kenya kuanza kuingia ni hatua kubwa na ambayo itawaamsha usingizini wafanyabiashara wa bongo kuanza kutengeneza bidhaa kwa ubora mkubwa sana.

Mfano hadi Sasa bidhaa kama juices, unga wa ngano n.k zimesharuhusiwa kuingia Tena bila inspection fee, maana yake ni kuwa hivyo vitu huku tutavipata kwa Bei ndogo na hivyo kufanya bidhaa zinazozalishwa nchini nazo kupungua Bei na hatimaye kupunguza inflation.

Hii ni hatua nzuri Sana Mama Samia, wenye viwanda ni wakati wao Sasa wa kunoa vichwa na kutengeneza bidhaa Bora ili kupambana na hizo za wakenya.

Hii ni survival of the fittest, wataoweza kupambana na bidhaa za Kenya wapambane na wataoshindwa basi ruksa kufunga hivyo viwanda.

Miaka mingi tumelia ubora wa bidhaa za ndani , Sasa Mama kaja kafungua nchi hivyo hii ichukuliwe Kama challenge kwenye nyie wenye viwanda ambao mlikuwa mnazalisha juice zisizo na ubora au mnazalisha unga kwa bei kubwa.

Kongole Mama Samia, kazi iendelee.

Screenshot_20210601-180113_1.jpg
 
Aondoe na ushuru kwenye bidhaa za maziwa kutoka nje ili wenye viwanda vya maziwa wakina ASAS, na wewnzie.....wajute na wakipate cha mtema kuni...... maana hawa wenye viwanda vya maziwa walikuwa ni mawakala wa mwendazake wametuchelewesha sana
 
Tatizo ya wafanyabiashara wa Tanzania Wana tamaa ya mafanikio ya haraka.

Wanatengeneza mavitu fake especially bidhaa za chakula kitu ambacho ni hatari sana kwa afya za walaji wakati huo huo tukijisifia kuwa na TBS na TFDA Taasisi ambazo hazitoi matokeo chanya
 
Wakenya walianza zamani kuleta bidhaa zao tena wakati sisi bado tumelala fofofo.

Miaka ya sabini zilikuwa zunakuja gari zao zenye bidhaa kila aina na pia madawa ya binadamu.

Walikuwa wanazunguka nchi nzima wakisambaza bidhaa zao

Kweli nimekumbuka mbali sana.

Kila jioni wanaonyesha sinema baada ya kukusanya hela siku nzima

Kama karuhusu ni mwendelezo tu
 
Ninacho jua mimi kila nchi ina sera ya kulinda soko la ndani, kiasi fulani ina achia bidhaa za nje kiasi flani una linda soko la ndani, Sasa wacha mama afungue bila mipango dhabiti baada ya 2 years viwanda vyote vitakufa na ajira zitakufa then tutakua soko la nchi jiran, hata ulaya hawa soko lisolo na kikomo kama mama yenu anavyotaka
 
Tatizo ya wafanyabiashara wa Tanzania Wana tamaa ya mafanikio ya haraka
Wanatengeneza mavitu fake especially bidhaa za chakula kitu ambacho ni hatari sana kwa afya za walaji wakati huo huo tukijisifia kuwa na TBS na TFDA Taasisi ambazo hazitoi matokeo chanya
Kweli ni fake mno na bila kusahau ubora na uzuri wa mwonekano, bei juu na taste kubadilika kila mara kwenye bidhaa hiyo hiyo, utamu pia Kama ni bidhaa ya kula haupo.
 
Back
Top Bottom