Memento
JF-Expert Member
- Jun 13, 2021
- 4,423
- 9,962
Rais Samia kwanza kabisa Mimi sipo upande wa CCM na naichukia sana CCM, lakini kutokana na kusema tukukosoe kwa heshima basi nitafanya hivyo kwako.
Naomba nikukosoe kwa heshima kuhusu ili suala la corona. Mara nyingi umekuwa ukituoumbusha na kutuasa kuwa corona iliingia nchini mwetu na ipo na inaua.
Na ulitumabia kuwa tuchukue tahadhari zote kujilinda na ugonjwa huu hatari na ndio maana hata serikali ikaamua kuleta chanjo ili kuponya watu wake.
Ikiwa kila siku unatukumbusha kuhusu hatari ya corona na kufuata namna ya kujikinga, alafu hapohapo na wewe mama yetu unavunja hayo masharti ya kujikinga na corona basi unatuchanganya sana.
Ziara yako ya Jana kutoka Moro kwenda Dom, huko njiani ulikuwa ukisimama kuongea na wananchi ambao walikuwa wamejikusanya bila tahadhari yoyote. Na hapo hapo Kuna magari ya serikali yalikuwa yakipita kuwaambia watu wakusanyike njiani kukusubiri uongee nao.
Mnatuchanganya sana Mh.Raisi mnatukusanya alafu mnatuambia tuepuke mikusanyiko. Kwa maneno yako kuhusu corona na kwa hali ilivyo wala hakukuwa na ulazima wewe kusimama huko njiani au kama vipi uachane nalo hili maana unachozungumza na kinachofanyika ni tofauti.
Juzijuzi ulikuwa uwanja wa taifa kwenye mechi ya Simba va yanga, watu walikuwa maelfu bila tahadhari yoyote, tofauti kabisa na ulivyosema na unavyosema kuhusu corona.
Ushauri: hili suala ninakuomba mh.Raisi uachane nalo.
#katiba mpya kwanza#
#R.I.P Charles Mbowe# pole mwenyekiti wangu#