PostGE2025 Rais Samia, hebu chutama ukubali kukosea

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Black Legend

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2015
Posts
208
Reaction score
361
Katika hotuba zote za hivi jaribuni, Samia Suluhu Hassan,ambaye ni Rais aliyechaguliwa kwenye Uchaguzi uliogubikwa na sintofahamu nyingi, na kutokea MAUAJI makubwa ya Watanzania ameonekana kutoa kauli za kujierka pembeni katika makosa makubwa yaliyotokea.

Kama mtuhumiwa namba moja wa ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu nchini ikiwa pamoja na MAUAJI makubwa yaliyotokea katika kipindi cha Uchaguzi Ilikuwa ni heri kwake na busara ya hali ya juu kukubali makosa makubwa yaliyofanyika chini ya utawala wake.

Kitendo cha kuunda tume na kuwapa maelezo ya kufanya pasi kuelekeza tume kuchunguza vyombo vya ulinzi vilivyo fanya mauaji ya halaiki, ni jambo ambalo linaongeza maumivu makubwa ndani ya mioyo ya watanzania

. Kwa hali ya kawaida,yeye ndiye anatakiwa kuwajibika kwa yote yaliyotokea chini ya amri zake kama kiongozi wa nchi. Kabla ya hayo uvunjifu wa haki za binadamu ulikuwa mkubwa lakini kwa KIBURI CHA MADARAKA ALIFUMBIA MACHO.

"Rais Samia Suluhu Hassan unajukumu kubwa la kuwajibika kama kiongozi wa nchi ambapo haki za binadamu zimevunjwa chini ya utawala wako"βš“βš–οΈπŸ“Œ
 
Wahenga walisema Sikio la Kufa, Ndo Mama alipofikia
 
Wewe ndo unakosea kumkosoa asiyekosa wala kukosolewa bali kupongezwa na kusifia hata akitukana
 
Huyu kilaza amechagua kuondoka madarakani kwa njia ya fedheha kubwa sana.
 
Huyu mama hashauriwi vizuri. Ila atabinywa tuu na wazungu. Hakuna rangi ataacha kuona.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…