Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 4,393
- 14,500
Akizungumza kwenye Baraza la Eid El-Fitri kumbi wa JNICC Dar es salaam, leo tarehe 31 Machi, 2025, Rais Samia amesema nchi yetu (Tanzania) imeendelea kuwa na Umoja na Mshikamano kwasababu viongozi wa dini wamejiepusha na mahubiri yenye uchochezi na kuleta mafarakano.
Aidha ameongeza kuwa Serikali hatosita kuwachukulia hatua kali baadhi ya Viongozi wa dini walio na mwelekeo wa kuhubiri na kupandikiza chuki na uhasama dhidi ya Serikali.
"Tushikilie msimamo wa imani, udhibiti wa nafsi zetu na wajibu wetu katika kuikuza na kuitunza amani yetu nchini. Niwaombe katika madhehebu na makundi yenu mbalimbali muweze kuwadhibiti wale wachache miongoni mwenu walio na mwelekeo wa kuhubiri na kupandikiza chuki kwa wananchi dhidi ya Serikali yao. Waache kufanya hivyo. Ni vyema sote tujue kuwa katika mifarakano na hasama hakuna atakayeibuka mshindi, bali kutatokea hasara na majanga,"